Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Madrasa ndio mfumo mkongwe zaidi wa kutoa elimu ambao umedumu kwa karne kadhaa kabla hata Ulaya hawajajua kusoma na kuandika na Marekani haijajulikana kuwepo kwenye uso wa dunia.
Katika kufuatilia historia ya ukuwaji elimu utapata kujua kuwa chuo kikuu cha mwanzo duniani ni kile kilichoanzia ndani ya msikiti huko Fez nchini Morocco ambao ulijengwa na mwanamke aitwaye Fatima al-Fihri baina ya mwaka 857–859.
Chuo hicho kinaitwa "University of Al Quaraouiyine" kikihusisha jina la kijiji alichozaliwa Fatima cha Kaioruan ambacho kwa sasa kimo ndani ya nchi ya Tunisia.Mwanamke huyo aliyezaliwa mwaka 800 na kufa mwaka 880 alikuwa wa kabila moja na Mtume Muhammad (rehma na amani zimfikie) la Quraysh.
Chuo hicho kilijengwa takriban karne mbili kabla kulinganisha na chuo kikuu cha mwanzo barani Ulaya cha Bologna nchini Italy kilichojengwa mnamo mwaka 1088 ambacho baadhi ya wanahistoria hukitaja kimakokosa kama cha mwanzo pia.
Chuo kikuu cha Al Quaraauiyine kilitambuliwa rasmi katika mifumo ya kisasa mnamo mwaka 1963.
Kitabu cha rekodi za kihistoria cha Guiness pamoja na shirika UNESCO baada ya kuangalia historia yake wamekitambua rasmi kama ndio chuo kikuu cha mwanzo duniani na ambacho kimebaki hai mpaka sasa bila kukatisha mafunzo yake na bado kikifundisha katika mfumo wa madrasa ambapo mwalimu hukaa katikati na kuzungukwa na wanafunzi wake.
Miongoni mwa watu mashuhuri wanaotajwa kupitia mafunzo katika chuo hicho ni Papa Sylvester(2) ambaye pia anaweza kutajwa kama mkristo wa mwanzo aliyevutika sana na elimu ya waislamu na aliyeingiza elimu Ulaya kupitia taasisi ya kanisa.
Pope Sylvester II aliliongoza kanisa katoliki kuwanzia mwaka 999 mpaka mwaka 1003 miladiya.