Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) chamsimamisha Mhadhiri kwa tuhuma za ngono

Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) chamsimamisha Mhadhiri kwa tuhuma za ngono

Mnavitetea hivi vibinti vya chuo nawashangaa!

Wako over 20 year wana maamuzi ya kukataa au kukubali

Huo ulikuwa ni mtego na ulifanywa makusudi tu kwa sababu maalumu
 
THURSDAY OCTOBER 28 2021

Dodoma. Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kimemsimamisha kazi mhadhiri wa chuo hicho, Basil Mswahili kufanya majukumu yake yote ikiwa ni pamoja na kufundisha kwa tuhuma za rushwa ya ngono.

Tangu jana katika mitandao ya kijamii kumekuwa na ujumbe mfupi wa maneno ukionyesha kuwa mtumishi huyo kanaswa na mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho akitaka kupewa rushwa ya ngono ili amnasua katika mitihani ya marudio anayoifanya baada ya kufeli.

“Sio mmoja kuna wahadhiri kibao wanaofanya michezo michafu,”imeeleza sehemu ya ujumbe uliotumwa katika mtandao wa Twiter.

Katika taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano kwa umma ya chuo hicho leo Alhamisi Oktoba 28, 2021 imesema kuwa Mswahili alisimamishwa tangu Oktoba 25 mwaka huu baada ya kupokea tuhuma hizo.

Amesema mhadhiri huyo amesimamishwa kufanya majukumu yote ikiwemo kufundisha hadi uchunguzi wa tuhuma hizo utakapokamilika.

“Chuo kimekuwa kikichukua hatua stahiki za nidhamu kwa mujibu wa sheria na taratibu za kiutumishi bila kumwonea mtu,” amesema.

Mwananchi
 
Siyo kama nafagilia maovu, hivi hakuna sheria ya kumkomoa huyu dogo kabla hajanyongwa? Yaani serikali itoe tu tamko anayetaka kumfila huyu jamaa ruksa, tuko tayari!
 
Mimi nashangaaga sana mtumishi ambaye ni kijana na sio mzee kupata msala wa ngono na mwanafunzi wake wa chuo.

Msomi mzima mwenye kazi yenye mshahara net around milion 2. Unashindwa kumtongoza binti under 25 akupe mwenyewe. Yaani huwezi kumpata binti uliyemzidi akili, pesa, umri na kila kitu mpaka umtishie kwa sup...
Sijajua shida ni nini? Mbona wanalipwa mpaka na madereva wa bajaji na hiace tena wanatoa mpaka kule kwa kwananiii.Wasomi mnakosea wapi?
 
Chuo kikuu cha Dodoma kimeanzisha mchakato wa hatua za kinidhamu na maadili kulingana na Sheria na kanuni za utmishi wa umma.

UDOM imesema mtumishi Petro Bazil alisimamishwa majukumu yake tangu Oktoba 25, 2021 hadi uchunguzi utakapokamilika. Udom imesikitishwa na usumbufu uliojitokeza.

Pia, soma=> UDOM: Wanafunzi wamkamata mkufunzi anayewapa 'Sup' ili afanye nao ngono

View attachment 1989670
tumblr_mzu45y3U2C1s91yx0o1_1280.jpg

Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru.
 
Vyuo vingi nchini huu uhuni upo sana tu.
Badala ya kufanya tafiti za maana za kulipeleka taifa mbele wamekalia ulevi na ngono. Newton, Schrodinger, et. al wangewekeza kwenye hayo mambo leo ndege zingekuwa zinaruka kweli?
 
Wadada wasiokuwa na akili wanajirahisisha mno. Akili hauna na unataka marks, biashara haiepukiki.
 
Mambo mengine ni ya kujitakia tu. Halafu alivyo bwege, ameshindwa hata kufunga mlango!
 
Vp kama kale kadent kalimwaambia mwalimu " mwalimu nakupenda sana leo usiku husipokuja gheto najiua na kuacha barua"?, jamaa ana kosa gani hapo
 
Mkuu Replica salam kwako. Hivi huyu Petro Bazil si bado ni mtuhumiwa? Mbona hili tangazo limewekwa hadharani? Anyway, labda uongozi wa UDOM umefumbia macho taratibu (Steps) za kinidhamu ILI kufikisha ujumbe Mzito kwa Wakufunzi au kuwafanya wanafunzi husika wasiendelee kuongea yale ambayo hawataki jamii kwa ujumla iyasikie.

Ahsante
Tangazo limewekwa hadharani kwa sababu bwana Petro nae ameonekana hadharani akiwa na Boksa tu sasa lazima chuo kitoe tamko la ufafanuzi kulinda image yake
 
Mswahili mkuda sana, alinaswaje kiboya? Twendelee kuwachata jamani.
 
Rushwa ya Ngono vyuoni na Maofisini imetamalaki.

wanawake wananyanyaswa sana kingono, wake za watu na hata wasio olewa, maboss wanawalaghai na kufanya ngono kwa lengo la kupata upendeleo.

TAKUKURU wanapaswa watupie jicho ktk eneo hilo
 
Back
Top Bottom