Responded Chuo Kikuu Huria (OUT): Tunachunguza tuhuma za Wahitimu wetu wa Mahafali ya 44 kudaiwa kufoji matokeo ya mitihani

Responded Chuo Kikuu Huria (OUT): Tunachunguza tuhuma za Wahitimu wetu wa Mahafali ya 44 kudaiwa kufoji matokeo ya mitihani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Muda mfupi baada ya kusambaa kwa andiko la Mdau akielezea tuhuma zinazohusu Chuo Kikuu Huria (OUT) kwamba kuna baadhi ya Wahitimu wamefoji matokeo na vyeti, ufafanuzi umetolewa na chuo hicho.

Kusoma hoja ya Mdau bofya hapa - Zaidi ya Wahitimu 300 wa Mahafali ya 44 ya Open University (OUT) wanasadikika wamefoji Matokeo ya Mitihani

Ufafauzi wa Chuo huu hapa
TAARIFA KWA UMMA.#affordablequalityeducationforall #elimuborananafuukwawote #ODL#out #openandonl.jpg

TAARIFA KWA UMΜΑ​
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kimebaini uwepo wa machapisho na taarifa zisizo rasmi zinazojitokeza katika mitandao ya kijamii na majukwaa mbalimbali ya umma, zenye madai yanayohusiana na uhalali wa matokeo ya baadhi ya wahitimu wa Mahafali ya 44 ya Chuo. Kufuatia machapisho hayo, Chuo kinapenda kutoa ufafanuzi rasmi kwa umma.

Kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji, uadilifu wa kitaaluma na kulinda imani ya wadau wa elimu, Chuo kilianzisha mchakato wa tathmini na uchunguzi wa kitaalamu ili kubaini uhalisia wa taarifa hizo. Mchakato huo tayari unatekelezwa kwa kushirikisha mamlaka husika za ndani ya Chuo pamoja na taasisi nyingine zinazohusika, kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Chuo kinapenda pia kuufahamisha umma kuwa baadhi ya takwimu na maelezo yanayosambazwa kuhusu ukubwa na uzito wa madai hayo havilingani na taarifa za awali zilizopo, hivyo kuhitaji uthibitisho wa kina kupitia mchakato unaoendelea.

Baada ya mchakato wa uchunguzi kukamilika, wahusika watajulishwa na hatua stahiki zitachukuliwa kwa kuzingatia misingi ya haki, uwazi na taratibu za kitaaluma.

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinasisitiza kuwa kitaendelea kusimamia viwango vya juu vya ubora katika taaluma, uwajibikaji na uadilifu.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
16-01-2026
 
Ila hizi kashfa za kufoji matokeo mkubali tu ndugu zangu wa OUT mlizianza muda mrefu! Na kuna kundi kubwa tu la wahitimu wamenunua elimu kwenye hicho chuo chenu.

Yaani hiyo biashara ya kununua matokeo haijaanza leo! Na huenda ukweli mnaufahamu, ila tu mnaoneana aibu kwenye kuwajibishana! Na matokeo yake ndiyo haya sasa ya kuchafuka.
Binafsi kwa kweli siwezi kusoma OUT!
 
Siyo OUT tu. Vyuo vingi wakufunzi wanakula rushwa sana
 
Ila hizi kashfa za kufoji matokeo mkubali tu ndugu zangu wa OUT mlizianza muda mrefu! Na kuna kundi kubwa tu la wahitimu wamenunua elimu kwenye hicho chuo chenu.

Yaani hiyo biashara ya kununua matokeo haijaanza leo! Na huenda ukweli mnaufahamu, ila tu mnaoneana aibu kwenye kuwajibishana! Na matokeo yake ndiyo haya sasa ya kuchafuka.
Binafsi kwa kweli siwezi kusoma OUT!
Dah ndiyo maana sisi wengine tukigoma kutoa hela wanatufanya maadui. Hiki chuo sawala la research limekuwa mradi wao wa upigaji
 
Back
Top Bottom