makaveli10
JF-Expert Member
- Mar 27, 2013
- 31,583
- 92,670
Nimesoma komenti kadhaa za ndugu zangu wakristo, wengi wenu nyie mna nongwa, mna upofu wa udini 😂🤣😂🤣.
We kula saa 10 usiku, usile tena wala kunywa maji na jua la dar, na mihangaiko yetu ya kila siku utaweza.
Jaribu tu wikiendi ambayo huna pilika pilika, kula saa 10 alfajiri, kisha usile tena mpaka saa 1 usiku ndio utaona uzito wake.
Mnajua lengo la funga,
1.Kufunga pekee ni utiifu kwa mola wako(ndio maana utasikia masheikh wanasema inakuweka karibu na mola wako) ni kama vile baba/mama yako akupe 5000 ya shule kisha akwambie humo tumia 500 tu, ama usitumie kabisa.
Ndani unachakula, mfukoni una hela, una mke lakini mungu anakwambia hakuna kula wala kunywa mchana, na wala kupiga miBAM BAM kwa mkeo.
2. Lakini pia funga inaongeza imani na huruma, ndani una kula kitu, mfukoni una pesa lakini hauli na njaa unaisikia, sasa unajiuliza wale masikini ambao hawana kitu wana njaa katika siku ambazo wanaruhusiwa kula, lakini hana cha kukila anakuwa katika hali gani.
Ndio maana katika mambo yanaleta thawabu nyingi basi moja wapo ni kulisha masikini ama yatima, ama kumkirimu msafiri(hii kwa zama hizi si sana, kutokana na maendeleo)
Shida waislam wengi hatuuinshi Uislamu wenyewe, na kuna watu wameuframe uisalm uonekane ndio dini ya hovyo, unaonekana hovyo sababu na sisi hatuuishi uislam.
Uislamu ni kuhurumiana, kusaidiana na kupendana
3. Funga ni afya, mtume alisema, fungeni mtapata afya, alijuaje hali yakuwa hakuwa mwanabaiolojia, mungu ndio mjuzi zaidi.
Ila sayansi ya siku hizi inakubali hii kauli ya kufunga ni kutengeneza afya.
Na faida nyingine nyingi nyingi, naweza nisizijue sababu ya uchache wa elimu yangu.