Churchill Show ya Arusha jana ni comedy duni sana kuwahi kuiona. Hakuna comedy nzuri bila maudhui magumu ya siasa

Churchill Show ya Arusha jana ni comedy duni sana kuwahi kuiona. Hakuna comedy nzuri bila maudhui magumu ya siasa

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Nimeangalia Churchill Show iliyoandaliwa na mkuu wa mkoa wa Arusha, itoshe kusema comedy ya Tanzania ni mbovu sana, maudhui ni duni mno, unaona wazi watu wanatumia nguvu kubwa sana kucheka na kufurahia.

Ambacho waswahili wanapaswa kufahamu ni kwamba chanzo na kushamiri kwa tasnia ya comedy kuanzia huko ilipozaliwa Ugiriki ni kutokana na Siasa kwanza, ndipo mapenzi na content nyingine zikafuatia.

Siasa ndio ina maudhui makubwa zaidi na yanayobadilika kila siku yanaweza kutengeneza content nzuri ya comedy.

Soma Pia: Churchill show live in Arusha

Kikawaida binadamu wanafurahia zaidi wanapofanyiwa utani wa kuudhi watu wenye nguvu zaidi katika jamii kama tabaka la watawala, matajiri na viongozi wa dini.

Ipo sababu comedians wakubwa na maarufu wote duniani content yao kubwa zaidi ni siasa na mijadala migumu ya kijamii katika nchi zao.Pia censorship ndio sababu ya comedy kutoshamiri China, Urusi na nchi nyingine za aina hiyo. Hata Tanzania comedy itaendelea kubaki duni kwa muda mrefu sana, haina future nzuri.
 
Back
Top Bottom