CIA HUWA HAWABISHIWI. UKISHINDANA NAO BASI KABURI LITAKUHUSU

Kuna shughuli wameifanya pale Bogota, Colombia na Gustavo Petro aelekea kushindwa uchaguzi mkuu labda atumie mbinu za medani.

Waliamua wamalizane nae kwa njia hiyo na wakifanikiwa basi kijana Abelardo de la Espriella anakuwa raisi kwenye mzunguko wa pili wa kupiga kura tarehe 21 Juni.

Traore pale Burkina Faso nae kasalimu amri kawaangukia Marekani na sasa msaada waingia Ouagadougou kwani nchi hiyo pamoja na maendeleo anoyafanya Traore lakini asilimia 60 na nchi hiyo yakaliwa na magaidi.

Mambo ni mengi na muda ni mchache.
 
Hii safari ya Moscow ina maana gani kwa mstakabali wa siasa za sasa na hapo baadae.
 
Traore alikuwa anajichanganya, unaendaje URUSI?

Mrusi hajawahi kuisaidia Afrika kwa lolote zaidi ya kumtia kibri mtawala kwa muda mfupi

Historia kwa Patrice Lumumba, Muamari Ghafafi, Tomas Sankara, Maduro, Mugabe, Hailey wa Ethiopia na wengine wengi Urusia haikuwasaidia.
 
Hii safari ya Moscow ina maana gani kwa mstakabali wa siasa za sasa na hapo baadae.
World Order haipo tena na Marekani wamechanganywa na Iran huku NATO ikiwa imegawanyika kuhusu Ukraine.

Na baada ya Marekani kuondoa vikwazo kwa Russia kwenye mafuta, nchi hiyo sasa yapata faida kubwa yaani moja ni dola milioni 150 kwa siku. Na mafuta hayo mteja mkubwa ni India.

Marekani kwa sasa yashindwa kumudu changamoto za kidiplomasia ambazo zatokea kila pande ya Dunia, ndo siasa za kijiografia hizo.

Ni wazi kwamba Russia ndio itakuwa yaongoza kundi la wanopinga sera na malengo kikoloni ya nchi za Magharibi na Marekani na itakuwa ni mfano mwingine wa vita baridi.
 
Una akili sana uwezo wa USA umeoneka kwenye vita ya Iran kiufupi hii vita USA angepata faida kama asingejiingiza kwenye hii vita ya Iran na heshima Sana akachemka zama za kuvamia nchi za watu kujenga Uchumi wako zimepitwa na wakati mchawi china anajenga Uchumi bila kuvamia nchi za watu USA amezingua sana
 
Hofu yangu ni Kwamba usije ikatokea Hawa USA wakawa activate Sleepers Agents wao hapa nchini.

Maana hao sleepers agents wakiwa activated hakuna atakayebaki salama itakuwa kama Yale ya Maduro ingawa hatuombei yatokee.
Kwenye hili kama nchi itapata shida sana maana hao wamo sehemu nyingi mno.

Wanikumbusha akina Jack Barsky na Anna Chapmann.

Barsky alikaa Marekani kwa miaka 10 kama "sleeper agent".

Anna Chapmann alikuwa "deep cover sleeper agent".

Hatari sana.
 
Putin ni tapeli km matapeli wengine, hana lolote yulee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…