Clement Mzize umemkosea heshima sana wakala wako, wachezaji wazawa ndio mana wengi hawafanikiwi kucheza nje ya nchi

Clement Mzize umemkosea heshima sana wakala wako, wachezaji wazawa ndio mana wengi hawafanikiwi kucheza nje ya nchi

Mnataka aende uarabuni kuua kipaji kwa kukalishwa bench kama ilivyotokea kwa Miqson siyo na wengine siyo? Na kwamba aache mshahara mpya wa Mil. 35 aliopewa na yanga huku akiwa karibu na biashara zake na familia ili aende kwenye mshahara wa Mil. 40 za Kitanzania kule nje kwenye gharama kubwa za maisha siyo? Mwacheni Mzize aamue. Siyo mtoto yule. Mnaotaka kwenda uarabuni nendeni uwanjani mkacheze ili muende nje.
Wachezaji wanaleta mapenzi kama mashabiki.. huku wao mpira ndio kazi yao.

Kazi ya kupenda timu sio ya mchezaji. Mchezaji unapaswa tazama timu zinazokupa exposure kubwa na mshahara mkubwa

Unakataa Esperence inayogombea ubingwa wa africa kila mwaka. sababu ya ushabiki, unabaki kwa timu ambayo ikifika robo fainali tu inafanya sherehe wananchinja ng'ombe na supu

mzize Hawaoni hata mfano kwa kina Mayele, Aziz kii leo hii wapo wapi?
 
Ubora kwenye kucheza mpira. Je mzize anamzidi nini Mayele ama Aziz kii? Mpaka wao wakubaliwe kuuzwa kwa hela ndogo na kukataa ofa kubwa ya mzize?
Vitu haviuzwi kwa kuangalia factor moja ru mzee utachekwa!
 
Kwa kitendo cha Clement Mzize kukubali aliekua msimamizi wake kukejeliwa na klabu pamoja na viongozi waliopo kwenye idara ya habari ya klabu ni kumkosea heshma na nimeshangazwa sana kuona Mzize anakubali hili wakati amewahi kusaidiwa na yule Mama

Bila shaka wachezaji wetu mbeleni watapitia maisha magumu na watakosa watu wa kuwasimamia kwasababu ya makosa yanayofanywa na wazawa wa sasa kisa uswahili na kukosa heshima na kutokua na msimamo pia kutanguliza mahaba badala professionalism na pesa.

Pole sana dogo kwa kutema big G kwa karanga za kuonjeshwa.
Point of correction Jasmine sio wakala hivyo kwa sheria za mpira hawezi kunegotiate au kuwa mwakilishi wa Mzize isipokuwa wachezaji wanachofanya ni kuwapelekea mikataba ili kupata ushauri wa kisheria.Mzize kunegotiate na Yanga sio kosa ila atapeleka mkataba kwa Jasmine ili kuona kama kuna vipengele visivyo rafiki
 
Yanga imemuuza aziz kii kwa dola laki 8, halafu maajabu inakataa dola milioni moja kwa mzize?

Je aziz kii na mzize nani ana ubora na thamani kali?

Kama sio kumbania mzize tu.

Hata kina mayele wameondoka bila kuuzwa kwa hiyo bei ya kufikia 1 million dollar
Mkuu Yanga ni taasisi inayojiendesha kwa hesabu zake na sio mihemko ya watu. Lengo la Yanga ni kufanya vizuri kimataifa. Haiwezi kusonga mbele kama itakua inauza key players wake.

Jinsi Yanga inavyofanya vizuri, ndivyo thamani ya wachezaji inavyopanda. Tusubiri msimu ujao tuone itakuaje
 
Elimu elimu elimu exposure exposure exposure!!!!!! Angekuwa ni kutoka Nigeria au Senegal angekuwa next level ila huyu mpe miaka mitatu utamkuta buguruni au keko au manzese ni suala la muda!! Just hold on
 
Back
Top Bottom