Clouds FM kuwatema watangazaji PJ, Gerald Hando na Abel Onesmo wa Power Breakfast

Clouds napend sana magazeti lkn awe PJ na Hando.... Jioni ni zamani alivyo kuwepo Gadna na Anold Kayanda.... Hao ndo saizi yangu. ....diva ...ndo uuuuuuiiiiii simuwezi... Milad namfatilia mitandaoni na mara chache j2....
 
Clouds fm wanaumwa ugonjwa unaitwa E fm ambao ushakuwa homa ya jiji soon utasambaa hadi mikoani
 
Mimi sijaelewa hapo wanaosema clouds "inazingatia neutrality" labda wangesema itazingatia.
 
Waje DIRA Media kazi zipo watasumbua tu....


 
Mbona Kibonde hatumbuliwi? Bora waanze na huyo asiye na chembe ya maadili ya uandishi wa habari. Kazi yake kubwa ni kujifanya anajua sana wakati ni mbumbumbu mkubwa.
 
Mbona anajiheshimu sana mkuu, au una ugomvi naye?
 
Hujaulizwa yote hayo lakin
 
Yuda Hando hajapata mrithi bado kipindi kita flop
My dear,kwa maandishi haya nachelea kusema huna uthubutu.
Kwanini unafikiri bila ya Hando kipindi kitaflop?
Kwani endapo ikitokea Hando kafariki kipindi kitafutwa?
C'mon kedrick.....
 
Weledi wa Kazi ni kufanya Kazi Kwa nidhamu na kufuata kanuni za Kazi, hakuna mwajiri yeyote anayeweza kuvumilia uzembe na utovu wa nidhamu katika Kazi,

kwenye Kazi kuna kanuni hakuna mwajiri yeyote anayeweza kuvumilia vitendo vya utovu wa nidhamu katika kazi, ni mwehu au mwendawazimu atayefurahia kufanya kazi na wafanyakazi wasiomuheshimu na wasiofuata kanuni za kazi.

katika kumbukumbu September 1, 2003 wapenzi na mashabiki wa Man U waliingiwa na simanzi baada ya Alex ferguson kumuonyesha mlango wa kutoka David Beckham kipenzi cha waingereza na mashabiki wa Timu ya Manchester United wengi hawakuamini jambo Hilo kwamba ipo siku Beckham ataondoka Manchester wakati Mashabiki wa Manchester wanamuhutaji na kumpenda wanauliza kwanini Alex unamuachia Beckham aondeke?

Kuna muda inabidi usimame Kama kiongozi kila mmoja aeshimu taratibu za kazi Beckham alikuwa amevuka mipaka hakuweza Kuwa na heshima ndani ya klabu ingawa alikuwa mchezaji mzuri na kipenzi cha wana Machester nukuu ya Alex Ferguson.

Katika taasisi yeyote misingi inapokiukwa inakuwa ni uhaini ni baba gani atakayeweza kuvumilia vitendo vya utovu wa nidhamu Kwa mwanae pasipo kumkanya? Akamuacha afanye atakalo ndani ya Nyumba ipi itakuwa thamani ya baba Kwa malezi ya mtoto.

Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa siku zote alikuwa anaamini katika maamuzi magumu na sahihi katika kupata maendeleo alinadi kuchukia uzembe na utovu wa nidhamu bila maamuzi magumu maji ziwa victoria yasingefika shinyanga na chuo kikuu Dodoma kingekuwa ndoto.

Uzembe na utovu wa nidhamu ktk kazi vikiachwa na kukua hujenga mazoea Rais John Pombe Magufuli anapata Kazi kubwa leo katika kuiongoza serikali kutokana na uzembe na utovu wa nidhamu pamoja na mazoea ya kubebana hakukuwa na utaratibu mzuri katika utendaji Kwa baadhi ya watendaji hapo nyuma kwakuwa walijua Hata wakitenda makosa hakuna hatua zozote zitakazochukuliwa.

Uzembe huu na utovu wa nidhamu uliisababishia hasara serikali jambo ambalo Rais Magufuli anapambana nalo mmpaka Sasa,

Katika pita pita zangu Leo kuachana na habari ya Marekani kutunyima msaada pale maskani kwetu nikapata taarifa kwamba Mkurugenzi wa vipindi Clouds Fm Bwana Ruge Mutahaba amewatimua Kazi watangazaji wake Gerad Hando na Paul James (PJ) na sababu ni kuwa watovu wa nidhamu

Nikatafakari kwa kina kuhusu kipindi cha PowerBreakfast na uwepo wa Hawa watu anyway nikawakumbuka watu Hawa

•Alex Ferguson
•Edward Lowassa
•John Pombe Magufuli

Kufanya maamuzi magumu na sahihi, uamuzi ambao utagharimu vingi lakini mwisho wa siku mambo yatanyooka.

Hongera Ruge Mutahaba naamini Sasa ni wakati wa Maamuzi magumu na sahihi tumbua jipu Kwa yeyote atakayeshindwa kufuata kanuni na taratibu zake mwajiriwa aje kazini amelewa afanye anavyotaka huko hatutafika natumaini umefanya hili baada ya kutoridhishwa na mwenendo wao licha ya kuwakanya Mara nyingi.

Mwaka huu nchi itarudi kwenye mstari Kama Kila mmoja ataamua kusimamia maamuzi magumu Na sahihi na hii iwe fundisho Kwa wafanyakazi wa kampuni nyingine waige mfano wako Ruge Hata uwe na mfanyakazi bora kiasi gani bila nidhamu ni sawa na Yai viza likipasuka litakukera tu.
 
Freduwa kahamia clouds?
 
Anasikiliza Mkuu wa Nchi we Kapuku wa Nchangimbore unatusumbua huku eti hausikilizi kojoa ulale hebu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…