kwa Tanzania kipindi kikubwa cha michezo kinachojitahidi kwenda na muda ni Sport HQ cha E FM .kuhusu kupiga nyimbo katikati ya kipindi ni kwaajili ya watangazaji kupumzisha akili na kwenda kupata kifungua kinywa maana Wasafi na E FM vipindi vyao vya asubuhi vina masaa mengi kuliko Clouds,mi naamini Wasafi wanapiga hela nyingi sana kutoka kwa wadhamini wa kipindi chao cha michezo na ndomaana Clouds wamestuka wameona waongeze muda kwenye kipindi chao cha asubuhi.Lwambano ni mtangazaji mzuri ila kwenye habari za kibongo tu kwa mimi ambae sipo Simba,Yanga wala Azam huwezi kuniambia kwamba ni mtangazaji bora wakati hiyo tuzo ya mtangazaji bora kachukua Kitenge.