Clouds Media wafungiwa kwa siku 7, kwa kutangaza Takwimu za Uchaguzi ambazo hazijathibitishwa na Tume

Clouds Media wafungiwa kwa siku 7, kwa kutangaza Takwimu za Uchaguzi ambazo hazijathibitishwa na Tume

Hii redio toka marehemu ruge aondoke naona inaelekea kufa na wasafi fm inachukua nafasi yake
 
Japokuwa ni haki ya mwananchi kupata habari ila hilo Rungu aliloshushiwa Clouds Media naona ni dogo sana mana mtu anajipendekeza mpaka kuharibu miiko ya kazi yake na kazi za wengine, kiherehere kitapungua wakirudi
 
Duh! Bila kujali upande wao wa kisiasa hili sio sawa. Wananchi wana haki ya kupata habari regardless
Ukifanya kazi ya shetani tarajia malipo ya hivyo hao jamaa hukuti watu wa upinzani kuhojiwa kwenye Media zao ukikuta habari inayohusu upinzani nilize zinazoonesha mabaya tu
 
Hizi sheria za kikoloni sio kabisa japo Mimi niliacha kusikiliza radio toka 2014 huko,. Karne ya 21 bado tunafungia fungia media!

Tume ingekanusha tu hizo habari jambo lingeisha, hii itasababisha media house zote ziache kuripoti habari za uchaguzi kwa hofu ya kufungiwa.
 
CCM haitaki rafu zinazofanyika majimbino au zinazotarajiwa kufanywa dhidi ya vyama vya upinzani zitangazwe na vyombo vya habari.Inataka isifiwe ili wananchi wasijue maivu yake Tanzania nakulilia
 
Dah sijui kwanini nimemkumbuka Marehemu Ruge Mutahaba..! Clouds wamepoteza kabisa weledi,wanaendeshwa zaidi na ushabiki! Ruge alikua mastermind,alikua anajua kucheza na matukio.

Siku saba kwa chombo cha habari kwa maana ya TV na redio ni hasara kubwa..yawezekana walitangaza ili wapate attention,lakini lazima wafike hatua wasome alama za nyakati.
 
Kwa hiyo wataomba radhi kila saa ? yaani kila wakirusha matangazo yatakuwa matangazo ya kuomba msamaha?
Bora ingekuwa kila saa,kila baada ya nyimbo 1 wanaomba. Imebidi nibadili station tu mana naona michosho
 
hapo Clouds anayejielewa ni Kipanya tu na ataendelea kufikisha ujumbe kupitia Katuni.

NB:
Wapinzani walivyokua wanalalamika kua hii sheria mpya inakandamiza uhuru wa habari, hawa watu wa media walikaa kimya kama kuku wenye kideri sasa leo yamewakuta.
Wale wapuuzi wa kipindi cha 360 waendelee kumshangilia Pombe na sheria zake kandamizi ili wapate uteuzi.
 
Wana funika kombe [emoji3][emoji3][emoji3].
Ili watu wasiamke..
Kama hakuna mpinzani katika hilo jimbo wa kushindana nae si ina maana mbunge wa ccm kashinda?.
Anasubiri nini sasa?

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
IMG_20200827_162334.jpg
IMG_20200827_162330.jpg
 
Back
Top Bottom