Eleweni nyie ndugu zangu, CCM haiwezi kuingia mgogoro na vyombo vya habari kizembe zembe namna hii! Haswa kipindi hiki cha kampeni.
Hapo kuna mchezo mnachezewa, na mchezo wenyewe umesukwa kiakili ili msing'amue.
Huo mchezo ni wa blackmail kwa vyombo vya habari kuwa ni lazima viendelee kuwa vitiifu, vya kutoa ushirikiano mzuri kwa chama tawala kipindi hiki cha kampeni. Lakini pia kudeal na Chadema
Plot niliyoing'amua ni hii ifuatayo:
Kwa kuwa Lissu ataanzia kampeni DSM kesho ama keshokutwa, na atafanya mikutano Dar siku tatu mfululizo.
Vyombo hivi vya habari sasa hivi kwenye kipindi rasmi cha kampeni ni vigumu kuvidhibiti kutotangaza habari za wapizani 100%, yaani wataanza kutupia tupia, na hilo watawala hawalitaki! Na hata kama havitaki kuzungumzia kampeni za upinzani bado vitapata pressure kutoka kwa umma kuwa kwa nini havirushi taarifa za upinzani?- Vinaogopa kudharauliwa na watu
Kwa hiyo plan ni ifungie Cloud Media ambayo inasikilizwa na wananchi wengi zaidi kuliko vyombo vingine kwa wiki nzima ili kupisha kimbunga cha Dar ili kuzuia uwezekano wowote wa clods media kurusha mikutano au habari za mikutano hiyo ya Lissu. Kumbuka CHADEMA wamejiandaa kufungulia kampeni Dar. Na nina wasiwasi viongozi wa clouds ambao ni makada wa CCM huenda wametoa ushirikiano mzuri kwenye kuwezesha hili.
Sasa Dar ikikubali kwa Lissu, ni rahisi mikoa mingine kuitika!
Kwa hiyo watawala wanataka siku CCM wakiwa Dar, Cloud Media itakuwa imeshakuwa huru kurusha mikutano ya CCM na hivyo kuwapa CCM coverage kubwa.