Clouds Media wafungiwa kwa siku 7, kwa kutangaza Takwimu za Uchaguzi ambazo hazijathibitishwa na Tume

Clouds Media wafungiwa kwa siku 7, kwa kutangaza Takwimu za Uchaguzi ambazo hazijathibitishwa na Tume

Wafungiwe tu kama watangazaji wenyewe kina Mwijaku unategemea nn?[emoji13][emoji13]
 
Hivi yale magazeti pendwa ya chama na musiba hayakuonekana kama yamekosea kurusha habari hizo hizo zilizorushwa na Clouds?

Sababu clouds walisoma magazeti yaliyoandika hivyo lakini mwisho wa siku Clouds ndio imewajibishwa, ebu tusubiri labda uhuru na jamvi nao watachukuliwa hatua
 
Mimi Clouds huwa siwasikilizi hata siku moja na siwapendi kwani ni vibaraka. Ile Clouds ya mwanzoni kabisa ndiyo ilikuwa pure entertainment studio na hata siku moja walikuwa hawaweki mambo ya siasa. Ila natoa tahadhari. Hata kama adui yako akipatilizwa na hizi sheria za kikandamizaji zilizobuniwa na hawa watawala waoga, usifurahie. Hao wamefungiwa siku saba tu, lakini target yao ni kufanya media ziogope na inaonekana kuna maandalizi ya kuja kufungia chombo huru tena kwa muda mrefu.
Upo sahihi sana kiongozi
 
Hata kama wanakubali kuwa wanasesere wa CCM wasifikiri ccm ina rafiki ccm inachotaka ni kututawala kwa mabavu na kutukandamiza
Waambie wamuulize Mbatia.
Maana walimvuta kaingia 18 akaanza kutamba ana kwenda kuwa KUB. sasa hata viti maalum hajui kama atapewa.
 
Hawa wanaofungia vyombo vya habari wangetafakari kwanza wanapoteza ajira za watanzania wangapi? Au hao walishatengeneza ajira ngapi? Au hao hawaoni hii changamoto ya ajira?

Wakati mwingine watanzania tunakatishana tamaa wenyewe, hili suala la kutangaza matokeo kabla ya tume ni suala la kupewa onyo tu ingetosha kuliko kutukosesha habari wiki nzima.

Wajue pia kuna vipindi vya kuwasaidia watu kama njia panda, je wanajua kua wameharibia watu kusaidiwa?
 
Hahahahah waandishi wa habari huu mwaka wenu hadi mkome..

Lissu njoo utukomboe baba tulipofikia inatosha.
 
Nasikilizaga Power breakfast mara nyingi asubuhi Clouds FM ila sijawahi kuona affiliation ya kipindi na CCM, kina Masoud huwa wanaongea indirect. Clouds 360 pale Clouds tv ndio wazee wa kujipendekeza

Na hii habari ya kupita bila kupingwa si iliandikwa hadi kwenye magazeti? Je na wao wamefungiwa?
 
Naomba kuelimishwa nanyi wabobevu wa sheria, hivi katika shauri hili nani ni MLALAMIKAJI na nani ni MLALAMIKIWA? Je hizo pande mbili zimekutanishwa na TCRA (Mamlaka) kabla ya kutoa hukumu?

Naomba kuelimishwa kidogo.

Ahsante
 
Nyie hamjagundua plan

Lissu ataanza kampeni DSM

Vyombo hivi vya habari sasa hivi kwenye kipindi rasmi cha kampeni ni vigumu kuvidhibiti kutotangaza habari za wapizani 100%, yaani wataanza kutupia tupia, na hilo watawala hawalitaki!

Kwa hiyo plan ni ifungie Cloud Media ambayo inasikilizwa na wananchi wengi zaidi kuliko vyombo vingine ili kupisha kimbunga cha Dar, maana CHADEMA wamejiandaa kufungulia kampeni Dar

Sasa Dar ikikubali kwa Lissu, ni rahisi mikoa mingine kuitika!

Kwa hiyo watawala wanataka siku CCM wakiwa Dar, Cloud Media itakuwa imeshakuwa huru kurusha mikutano ya CCM na hivyo kuwapa CCM coverage kubwa.

Eleweni hii michezo ya kisiasa inavyochezwa nyie
[emoji106] [emoji106]
 
Hawa wanaofungia vyombo vya habari wangetafakari kwanza wanapoteza ajira za watanzania wangapi? Au hao walishatengeneza ajira ngapi? Au hao hawaoni hii changamoto ya ajira?

Wakati mwingine watanzania tunakatishana tamaa wenyewe, hili suala la kutangaza matokeo kabla ya tume ni suala la kupewa onyo tu ingetosha kuliko kutukosesha habari wiki nzima.
Wajue pia kuna vipindi vya kuwasaidia watu kama njia panda, je wanajua kua wameharibia watu kusaidiwa?
kweli
 
Back
Top Bottom