Clouds Media wafungiwa kwa siku 7, kwa kutangaza Takwimu za Uchaguzi ambazo hazijathibitishwa na Tume

Clouds Media wafungiwa kwa siku 7, kwa kutangaza Takwimu za Uchaguzi ambazo hazijathibitishwa na Tume

Ni kweli, ila ni sheria zenye nia ovu. Hata huko Afrika kusini enzi za makaburu kulikuwa na sheria zenye nia ovu kama hizi hizi. Clouds walikuwa na tabia ya kujipendekeza sana kaa serikali, acha wajue kuwa waliokuwa wakijipendekeza kwao sio watu wazuri. Cha ajabu wakurugenzi waliotangaza wagombea waliopita bila kupingwa bado wako ofisini.

usingie mkenge, hao wanakwepesha mikutano ya ufunguzi ya kampeni ya Lissu ya Dar aliyosema ataifanya siku tstu mfululizo ili isiweze kuwa mentioned kabisa. Pressure ya uchaguzi inalazimisha TV na redio vishindwe kumuignore Lissu kabisa, kwa hiyo wakubwa have to do something about it!

Sasa Dar ni jiji kubwa, Lissu akiwa received positively halafu habari yake ikatrend, wakubwa wanahofu itaaffect campaign zao!

Kumbuka Clouds media ndo inangoza nchini kwa idadi ya watu wanaosikiliza nchini hii ni kwa mujibu wa tafiti
 
Mkuu bila kupinga maelezo yako mazuri, kwani huyo Tundu Lisu huwa anapata coverage sana huko clouds, mpaka wachukuliwe hatua wao tu? Sio kwamba sioni hofu yako, ila kufungiwa hao clouds sio kwa sababu hii uliyosema ww.
 
Muda mwingine anayefunga huwa anaujaribu mlango kama una uwezo wa kufunga na kufungua [emoji41]
 
Dah clouds wanapitia hali ngumu sana.

Kimyaaaaaa.... tunasikia kumradhi tu ya mauzui ya tume.

Acha waisome namba eeee..
 
Eleweni nyie ndugu zangu, CCM haiwezi kuingia mgogoro na vyombo vya habari kizembe zembe namna hii! Haswa kipindi hiki cha kampeni.

Hapo kuna mchezo mnachezewa, na mchezo wenyewe umesukwa kiakili ili msing'amue.

Huo mchezo ni wa blackmail kwa vyombo vya habari kuwa ni lazima viendelee kuwa vitiifu, vya kutoa ushirikiano mzuri kwa chama tawala kipindi hiki cha kampeni. Lakini pia kudeal na Chadema

Plot niliyoing'amua ni hii ifuatayo:

Kwa kuwa Lissu ataanzia kampeni DSM kesho ama keshokutwa, na atafanya mikutano Dar siku tatu mfululizo.

Vyombo hivi vya habari sasa hivi kwenye kipindi rasmi cha kampeni ni vigumu kuvidhibiti kutotangaza habari za wapizani 100%, yaani wataanza kutupia tupia, na hilo watawala hawalitaki! Na hata kama havitaki kuzungumzia kampeni za upinzani bado vitapata pressure kutoka kwa umma kuwa kwa nini havirushi taarifa za upinzani?- Vinaogopa kudharauliwa na watu

Kwa hiyo plan ni ifungie Cloud Media ambayo inasikilizwa na wananchi wengi zaidi kuliko vyombo vingine kwa wiki nzima ili kupisha kimbunga cha Dar ili kuzuia uwezekano wowote wa clods media kurusha mikutano au habari za mikutano hiyo ya Lissu. Kumbuka CHADEMA wamejiandaa kufungulia kampeni Dar. Na nina wasiwasi viongozi wa clouds ambao ni makada wa CCM huenda wametoa ushirikiano mzuri kwenye kuwezesha hili.

Sasa Dar ikikubali kwa Lissu, ni rahisi mikoa mingine kuitika!

Kwa hiyo watawala wanataka siku CCM wakiwa Dar, Cloud Media itakuwa imeshakuwa huru kurusha mikutano ya CCM na hivyo kuwapa CCM coverage kubwa.
Upuuzi mtupu, CCM inazindua kampeni zake 29, chenyewe hakiitaji coverage ya clouds?
 
Kwahiyo wanapotakiwa Kuomba Radhi Siku nzima ya leo TCRA wanamaanisha Kwanza Kuanzia Mmiliki Kusaga, Mkewe, Wahariri na Watangazaji pengine hadi Wafanya Usafi wa CMG wanatakiwa kupeana zamu kila Mmoja kwa Masaa yaliyobaki Siku ya leo Kumalizika kwa Kufululiza kwenda Makao Makuu yao Kuwapigia Magoti ya Msamaha au? Kuna mahala katika Taarifa yao nimeona wanatakiwa Kuomba Radhi kwa Siku nzima hii ya leo.
 
Mkuu bila kupinga maelezo yako mazuri, kwani huyo Tundu Lisu huwa anapata coverage sana huko clouds, mpaka wachukuliwe hatua wao tu? Sio kwamba sioni hofu yako, ila kufungiwa hao clouds sio kwa sababu hii uliyosema ww.

Kipindi hiki cha kampeni ni vgumu kuvibana vyombo vya habari visirushe taarifa za mikutano ya kampeni za vyama kabisa kabisa.
Wakubwa wanajua effect ya kurusha nyomi za uzinduzi wa lissu Dar, jiji kubwa, inaweza ikaathiri nchi nzima, So wametarget radio na TV yenye kusikilizwa na wengi zaidi
 
Shida nini tena
Wameendeleza kutangaza kwamba kuna wagombea wamepita bila kupingwa wakati hilo ni jukumu la Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Tume haipendi shobo na waliolikorogo safari hii ni Clouds 360

AIDHA
Kipindi Cha JAHAZI kwa takribani wiki Sasa kimepigwa bani kwenda hewani kwa kosa la kuhamasisha watu KUPIGA PUNYETO (KUJICHUA)

VILEVILE Adam Mchomvu wa kipindi Cha XXXL akiwa host wa Tamadha la CCM mwezi August 15 alimchapa mtama Mtumishi wa Mungu na Mwimbaji wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha kwa kosa la kumuita hadharani ADAM MIBANGE.

Hiyo ndio redio ya wafu bana...
 
Sam Sassali na Babe Kabae wanapaswa kuongeza umakini kwenye kazi. Mambo ya kuendesha kipindi kama kijiwe cha kahawa kitawa- cost big time!
 
Kwahiyo wanapotakiwa Kuomba Radhi Siku nzima ya leo TCRA wanamaanisha Kwanza Kuanzia Mmiliki Kusaga, Mkewe, Wahariri na Watangazaji pengine hadi Wafanya Usafi wa CMG wanatakiwa kupeana zamu kila Mmoja kwa Masaa yaliyobaki Siku ya leo Kumalizika kwa Kufululiza kwenda Makao Makuu yao Kuwapigia Magoti ya Msamaha au? Kuna mahala katika Taarifa yao nimeona wanatakiwa Kuomba Radhi kwa Siku nzima hii ya leo.
Wote kwa pamoja wanatakiwa kuwa hewani huku wakisema tusamehe ewe Fisiemu tumekosa sana
 
Mbona TCRA imemwacha Millard Ayo maana yeye ndio alitangaza wagombea kupita nakuwa wabunge ikiwemo Kasimu Majaliwa, na wale Morogoro
Baada ya kosa Lile kufanyika TCRA walitoa onyo na leo hii tena Asubuhi kupitia kipindi Cha Clouds 360 wakaliamsha tena dudee.
 
Umeona sasa!!! only smart people will understand this hivi lini chadema wanakuja na chombo chao??

Hata hicho chombo chao bado kitakuwa chini ya tcra kwa sheria zile zile za kizamani. Refer kilichotokea TanzaniaDaima.
 
Shamba boy atawafungulia akiwa jukwaani siku anafungua kampeni. kwamba oooh watu wanakosa burudani n.k
 
Hawa clouds kila TCRA ikitoa adhabu lazima wawemo mbona hawajifunzi!!!
 
Mbona TCRA imemwacha Millard Ayo maana yeye ndio alitangaza wagombea kupita nakuwa wabunge ikiwemo Kasimu Majaliwa, na wale Morogoro
Hawa nao mbona hawajafungiwa?
Screenshot_20200827-193849_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom