CLOUDS: Mishahara ya walimu inadhalilisha utu wao

maisha ni mazuri kwa waalimu, mazingira ya kuishi na watoto yanawapa picha halisi ya asili ya tabia za mwanadamu, walimu wanasomesha, kujenga na kuwa na vitega uchumi mbadala wanaishi kwa furaha tu huku wakisubiri mafao yao uzeeni. point to take ni kwamba maisha ni mazuri pale utakapojua namna ya kumanage kile unachokipata
 
Kada zingine Zina allowance kibao, food allowance, house allowance, transport allowance, nk mbali na hayo wana vikao kila wiki tena vya pesa nzuri tu. Sasa njoo Kwa walimu manina anasahihisha mitihani ya ndani bureee, anasimama bureee, mitihani ya mock mkoa na wilaya bureeee, anafundisha mpaka jumapili bureeee, hawana hata vikao navikiwepo vya SMT ni bureeee, kila kitu halambi hata sumuni
 
Inaonesha wazi wewe ilikosa hii ajira. Waalimu hawa hawa au wengine ? Unafika shule ya Msingi kumefurika. Magari ndani ya parking ya Waalimu utafikiri showroom pikipiki hazina idadi .
Tatizo wako brainwashed sana huwaambii kitu.


Maticha siku hizi Wana harakati nyingi kitaa

Hio kazi ya kuzugia tu au kuchukulia mikopo kuweka kwenye harakati zao.

Mwalimu anategemea mshahara tu ni Fala tu.
 
Ukute we ni ticha 🤣🤣🤣
 
Hebu hiyo media ituambie kwanza mwalimu wa certificate diploma na degree wanalipwaje?

Tuanzie hapo kwanza halafu tufananishe na kada zingine kama vile manunuzi,utumishi,uhasibu,kilimo,mifugo n.k

Vinginevyo wana ajenda yao nyuma ya pazia
 
Haitakaa itokee
Sa we jamaa wa Matumburu ndanindani hukoo unadharau waalimu.

Ngoja nikupe historia yangu kidogo.

Nimeanza kazi TSD Mkoa Dodoma then nikahama Taasisi mbalimbali.

Mwalimu wa Degree anaishia TGTS-I levo ambayo kada zingine wanaishia TGS-H
So kama hujui kaa kimya
 
Huu sasa ni uchochezi; ila kwa upande mwingi, utafiti wangu umeshanionyesha kuwa tatizo la mishahara kwa ujumla wake na si kwa walimu tu, linachangiwa kwa kiasi kikubwa sana na watu wanaotafuta mamlaka makubwa kwa njia ya kuuhujumu uongozi uliopo madarakani
Watu hawa huwa wanakusanya pesa zao kwa njia ya mishahara. Sasa usiniulize huwa wanakusanyaje
 
Hebu hiyo media ituambie kwanza mwalimu wa certificate diploma na degree wanalipwaje?

Tuanzie hapo kwanza halafu tufananishe na kada zingine kama vile manunuzi,utumishi,uhasibu,kilimo,mifugo n.k

Vinginevyo wana ajenda yao nyuma ya pazia
Mwalimu mwenye shahada ya kwanza anayeeanza kazi huanza na 780, 000 hii inaitwa D1 . Kila baada ya miaka 3 hupanda daraja. Daraja la mwisho kabisa ni "I" ambayo ni 3.2M.

Hii mishahara siyo midogo ukilinganisha na kada zingine. Tofauti ni kwamba mwalimu hana mazingira ya kula rushwa au kupata posho zingine inje na mshahara.
 
Duh,kumbe hiyo media ni wapumbavu kiasi hicho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…