Ningekuwa Josefu Kusaga,ningetafakari upya mikataba waliyonayo baadhi ya watangazaji kama yule 'mvuta bangi',na wengine wanaobwabwaja hovyo kwakuwa hawa ndio wamekuwa chanzo cha CMG kuingia matatizoni mara kwa mara na TCRA.
Msingi mkubwa wa uamzi huu ingekuwa kwamba:
1_Mtangazaji asiye na maadili binafsi hawezi kufata maadili ya utangazaji.Hawa husababisha clouds kupigwa faini na kuleta hasara kwenye kampuni.Mara kadhaa clouds wamepigwa faini kwa sababu zinazohusiana na kupungukiwa maadili kwa baadhi ya watangazaji.
2_Baadhi ya watangazaji pale clouds wana political ambitions zao na wanakujanazo kazini.Wanawaza mno uteuzi kutoka kwa Rais hivyo wanalazimika kuweka ushabiki wa wazi kisiasa wakiwa kazini.Kama wangekuwa makini hakukuwa na sababu ya kushabikia watu kupita bila kupingwa,jambo lililosababisha kufungiwa.