Clouds wamaliza adhabu ya TCRA warudi hewani kwa mbwembwe!

Clouds wamaliza adhabu ya TCRA warudi hewani kwa mbwembwe!

ILA MSHIKA RUNGU WA TCRA KWASASA ANAONESHA KAMA ANA HASIRA SANA NA CLOUDS, UTAFIKIRI NA YEYE ANA REDIO AU TV YAKE INAYOSHINDANA NAO KIBIASHARA.
 
Hatimaye Clouds Media Group wamemaliza kutumikia adhabu ya kifungo cha siku 7 waliyopewa na TCRA na wamerudi hewani rasmi.

Kinachoendelea sasa luningani ni sherehe ya wafanyakazi baada ya kutoka kifungoni, ni full shangwe.
CCM hoyeeee!

Maendeleo hayana vyama!
ushauri kwa clouds leo karushe live mkutano wa chadema dodoma basi ndani ya masaa matatu mtakua mmerudi kwenye form ya ajabu,
 
Ila Clouds bado ina wasikilizaji wengi sana aiseee.. huwezi amini kuna watu jana usiku walikesha kusubiri kile walichokiita "kuwasha mitambo"..
 
Sam alijiachia utadhani anatangaza kwenye sherwhe akasahau TCRA wanawachabo tuu... eti nape kapita bila kupingwa ...mama kasema
 
Ningekuwa Josefu Kusaga,ningetafakari upya mikataba waliyonayo baadhi ya watangazaji kama yule 'mvuta bangi',na wengine wanaobwabwaja hovyo kwakuwa hawa ndio wamekuwa chanzo cha CMG kuingia matatizoni mara kwa mara na TCRA.
Msingi mkubwa wa uamzi huu ingekuwa kwamba:
1_Mtangazaji asiye na maadili binafsi hawezi kufata maadili ya utangazaji.Hawa husababisha clouds kupigwa faini na kuleta hasara kwenye kampuni.Mara kadhaa clouds wamepigwa faini kwa sababu zinazohusiana na kupungukiwa maadili kwa baadhi ya watangazaji.
2_Baadhi ya watangazaji pale clouds wana political ambitions zao na wanakujanazo kazini.Wanawaza mno uteuzi kutoka kwa Rais hivyo wanalazimika kuweka ushabiki wa wazi kisiasa wakiwa kazini.Kama wangekuwa makini hakukuwa na sababu ya kushabikia watu kupita bila kupingwa,jambo lililosababisha kufungiwa.
 
Back
Top Bottom