Clouds wananufaika vipi na mgogoro wa chama cha walimu? Naona wamekusanya chawa studio, TUCTA iliuawa kwa njia kama hizi

Mleta uzi umezunguka Sana, jibu wewe ni pro Maganga au anti Maganga?
 
Nashukuru sana,sikatwi tena CWT,CWT wamelaaniwa wao na vizazi vyao vyote kwa kutumia VIBAYA hela za wafanyakazi maskini Walimu. MLAANIWE MILELE.
Duh mwalimu [emoji12][emoji12][emoji12][emoji12][emoji12]
 
Mkuu TUCTA ilikufa lini?
Ninavyojua TUCTA ni shirikisho la vyama vyote vya wafanyakazi unasemaje imekufa wakati vyama vipo..
Rais Wa TUCTA bado yupo na anasimamia vyama vyote ikiwemo hiyo CWT,TUGHE ,Na TALGWU
TUCTA ni Marehemu, lini umewasikia?
 
Bullying.
Black Propaganda.
Characters Assassination and Smear Campaign.
Lengo ni kumchafua mhusika ili aonekane kwenye jamii kuwa ni mtu asiyefaa. Hao unaowaona wanaunga mkono suala hili huenda pengine ni mamluki wao au wapigadebe wao wa kusukuma ajenda.
 
Hiki chama kimepoteza ushawishi ,afadhali kipindi kile anakiongoza mkoba kilikuwa imara
 
Kwahyo shida ni Viongozi na Sio Taasisi?
Kikubwa katika TUCTA ni kumuondoa Rais na katibu wake vingine vitakuwa sawa..

Ila kusema TUCTA imekuwa wakati huo TUCTA ndo inasimamia hata hiyo CWT yenu na TUGHE na TALGWU sio sawa
Ndiyo shida ni viongozi kushindwa kusimamia na kuboresha malengo yaliyokusudiwa kuanzishwa kwa vyama au haya mashirikisho. Kwa sehemu kubwa viongozi waliopo wanatumiwa na wanasiasa (muajiri mkuu) kuhujumu jitihada za wafanyakazi kuwasilisha madai yao. Kudai haki kunaitaji kiongozi jasiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…