Mkuu retired 'exisitential threat' kwa kiswahili ina maana gani?
Ila kuhusu corona Mungu atuepushie hili gonjwa tu, maisha yetu tunayoishi tunafaham wenyew sasa + corona ni balaa tupu kwa kwel
Sent using
Jamii Forums mobile app
Aina ya hatari kufuta uhai wa aina fulani ya binadamu au wanyama.
Kwa mfano itokee aina fulani ya swara wamebaki kama mia na wanaishi kaeneo kadogo wote kwa pamoja, halafu kundi la simba lizingire hao swara, hapo ndio tunasema aina hiyo ya swara wapo kwenye "existential threat", maana watauawa wote, ifahamike simba hawatakua wakiua tu wawafanye msosi, ila wataua kila swara atakayepatikana hai.
Mfano mwingine ni ule uvamizi wa taifa la Israel kutoka kwa mataifa ya kiarabu, wale Waarabu hawakua wanakwenda kupigana na Israeli kijeshi, nia ilikua ni kuchinja chochote na yeyote mwenye damu ya Kiyahudi kama alivyofanya Hitler. Yaani chochote chenye hatari ya kufutwa kwenye ramani ya dunia ndio huwa tunasema kipo kwenya hatari ya "existential threat".
Kwa kifupi, Corona ina uwezo wa kutufuta Afrika maana inachofanya wenye uwezo zaidi yetu, unajiuliza hivi nini tunacho cha maana hadi ikatukwepa.
Kama ni kunawa mikono, wale wananawa mpaka basi, ilhali huku bado kuna vijiji na mitaa haina hata maji. Kama ni kuepuka misongamano, wale wamejifungia ndani kabisa, Afrika bado tunasongamana kwenye madaladala na madhehebu. Yaani tahadhari kwa wale zinachukuliwa za hali ya juu ila bado wanadondoka kwa maelfu, huku sisi tupo tupo tu, lakini anakufa mmoja baada ya mwezi.