CNN and Coronavirus: Africa in existential threat

CNN and Coronavirus: Africa in existential threat

Aina ya hatari kufuta uhai wa aina fulani ya binadamu au wanyama.
Kwa mfano itokee aina fulani ya swara wamebaki kama mia na wanaishi kaeneo kadogo wote kwa pamoja, halafu kundi la simba lizingire hao swara, hapo ndio tunasema aina hiyo ya swara wapo kwenye "existential threat", maana watauawa wote, ifahamike simba hawatakua wakiua tu wawafanye msosi, ila wataua kila swara atakayepatikana hai.

Mfano mwingine ni ule uvamizi wa taifa la Israel kutoka kwa mataifa ya kiarabu, wale Waarabu hawakua wanakwenda kupigana na Israeli kijeshi, nia ilikua ni kuchinja chochote na yeyote mwenye damu ya Kiyahudi kama alivyofanya Hitler. Yaani chochote chenye hatari ya kufutwa kwenye ramani ya dunia ndio huwa tunasema kipo kwenya hatari ya "existential threat".

Kwa kifupi, Corona ina uwezo wa kutufuta Afrika maana inachofanya wenye uwezo zaidi yetu, unajiuliza hivi nini tunacho cha maana hadi ikatukwepa.
Kama ni kunawa mikono, wale wananawa mpaka basi, ilhali huku bado kuna vijiji na mitaa haina hata maji. Kama ni kuepuka misongamano, wale wamejifungia ndani kabisa, Afrika bado tunasongamana kwenye madaladala na madhehebu. Yaani tahadhari kwa wale zinachukuliwa za hali ya juu ila bado wanadondoka kwa maelfu, huku sisi tupo tupo tu, lakini anakufa mmoja baada ya mwezi.
Mkuu ni hatari tupu kwa kwel ila nilichogundua huu ugonjwa unaitaji ukute mfumo wa mapafu yanafanya kazi vizuri, kwaiyo tuanze mazoezi ya kukimbia kila tupatapo nafasi pia kwa wale wavutaji wa sigara kipindi hiki wahache tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo chanjo wanayoitengeneza ndio hatari zaidi ya huu ugonjwa wenyewe kwa maana hii itakayoletwa huku kwenye Continent itachanganywa na depopulation agents
Halafu Serikali zetu uchwara zitalazimisha kila mmoja wetu adungwe.

Halafu wanaume kwa wanawake tunajikuta hatuna tena uwezo wa kuzaa Think man
 
Binadamu ana mucus kwenye njia ya hewa, hii ni sehemu ya kinga ya mwili. Hewa ikiingia na uchafu unakamatwa na mucus na uchafu ule unautoa kama kohozi.

Mucus goblets zikishambuliwa na virus ndiyo mafua yanachuruzika na huweza kukohoa. Maambukizi yakitokea kwenye mucus membrane husababisha kikohozi. Ndiyo maana unatumwa kikohozi ili wataalamu wagundue ni maambukizi gani.

Covid-19 hushambulia njia ya hewa na maambukizi huleta joto mpaka centi grade 38-39. Mucus goblets zinashambuliwa kwa kasi na Hutoa makohozi. Mapafu hukosa oxygen.

Afrika maisha yetu ni ya kufanya maoezi muda wote. Si kwa kupenda ni lazima utembee kwakuwa huna nauli ya basi na Gari huna. Mapafu yanakuwa imara. Pia vyakula tunavyokula ni organic.
Hujawahi kuniangusha kwenye mambo haya dada yangu kipenzi.
Hakika mzee Asprin a.k.a shemejiii kapata muke ya kitabu kweli kweli na akili mukichwa.
 
Africa, kama zilivyoathirika nchi za Ulaya na Asia, nayo itaathirika, lakini yawezekana pia kwa namna tofauti.

Nilicho na uhakika nacho, Waafrika hatutapotea Duniani kwa sababu ya Covid 19. Labda kama ugonjwa huu utaondoa watu wote.

Mwanasayansi Mkuu ni Mungu. Ndiye anayeilinda ecosystem ya Dunia.

Miaka ya 1970, Marekani walifanya utafiti, na wakawa na program ya kufuta magonjwa yanayosababishwa kwa kiasi kikubwa na umaskini. Kutokana na study hiyo, wakawa na projections ya vifo vitakavyopungua. Kufikia mwaka 1985, walifanikiwa kuondoa karibia vifo vyote vinavyotokana na bacteria, amoeba na protozoa. Lakini cha ajabu proportion ya vifo ilibakia palepale. Wakati vifo walivyopanga kuviondoa vikipungua, vile vilivyosababishwa na matatizo ya moyo, cancer na kisukari viliongezeka. Mwenyezi Mungu wakati wote huiweka Dunia kwenye equillibrium.

Kwenye hili janga la corona, wazungu wamepunguza vifo kwa kutumia njia za kitaalam kama matumizi makubwa ya respiratory ventilators, huku Afrika kwa vile vifaa hivyo ni haba sana, vifo vitapunguzwa kwa nguvu za asili kama vile natural immunity au uhimilivu unaotokana na Afrika kuwa na kundi kubwa la vijana.

Mpaka sasa kuna pucha fulani inaonekana kwa Dunia nzima. Nchi kama Italy, ndiyo yenye huduma bora kabisa za afya. Ndiyo sababu ya watu wao kuishi miaka mingi. Imeathirika sana na ugonjwa huu. Nchi kama Marekani, Ufaransa, UK, ni mataifa yenye teknolojia ya hali ya juu katuka tiba, yameumizwa vibaya. Huko huko Ulaya na Asia, kuna mataifa ambayo kiulinganifu, ni maskini na yana teknolojia duni lakini hayajaumizwa kwa kiasi kikubwa kuoindukia. Je, mataifa hayo yamechukua tahadhari kubwa sana au nature inafanya kazi yake?

Naamini tayari Mungu amekwishaweka mizania ya aina fulani. Ugonjwa umeanzia kwenye mataifa yenye uwezo ili mataifa hayo yatumie uwezo wao katika kutafuta nguvu za kukabiliana na janga hili. Ugonjwa umefika Afrika wakati tayari unafahamika. Ni jukumu letu kutumia nafasi ya kuufahamu ugonjwa huu katika kujikinga kwa namna tunazoweza.

Kwa Wakristo - Mtoto Yesu alipotakiwa kuuawa na Herode, Mariam na Yusuf waliambiwa wakimbilie Afrika. Yesu alipobebeshwa msalaba, na Wayahudi kuwa na wasiwasi kuwa hatafika nao eneo la kumsulibisha, Simon (Mwafrika) alilazimishwa aupokee msalaba. Afrika iliyo duni kwa mambo mengi, ni makimbilio ya wakati wa dhiki.

Spannish flu, mwaka 1920 iliambukiza robo ya watu wote Duniani. Watu wapatao 500 waliugua, na watu kati ya 25 - 39m walikufa. Nchi kama India 5% ya watu wake wote walikufa kwa ugonjwa huu. Na kwa mataifa mengine 1 - 6% ya watu wao wote walipoteza maisha. Afrika pamoja na uduni wake wa huduma mbalimbali, bado wameendelea kuwepo.

Tutapukutika lakini hatutapotea. Tutaendelea kuwa sehemu ya population ya Dunia.

Tuendelee kujikinga kwa namna ile iliyopo ndani ya uwezo wetu. Wapo wanaosema kuwa kila baada ya miaka 100, Dunia inatafuta equillibrium - inatafuta ulinganifu kati ya resources na watumiaji wa resources:
1720 Plague iliua zaidi ya 100,000
1820 Cholera iliua zaidi ya 100,000
1920 Spanish Flu iliua 25 - 39m
2020 Covid 19 itaua ???
 
Mabeberu wameshaongea mara kadhaa.

Kifupi hawafurahishwi na uwepo wa bara hili. Watafanya kila wanaloona linafaa kutupoteza then watasingizia Corona.

Tujihadhari sana..

Bill G kashaongea several times.. Africans will die in billions.. They don't like our presence in this planet. Aarssholes
Kufuta uwepo wa watu weusi ni jaribio lisilo jepesi
 
Ukimfahamu adui yako ni rahisi kumwepuka. Watanzania tumeshagundua huu ugonjwa unaenezwaje hivyo ni jukumu letu kujikinga kwa njia zozote zile ili tusidhurike. Nawa mikono na sabuni, usishike mdomo, pua macho na uso wako wakati mikono yako sio safi. Usikumbatiane na mtu yeyote ambaye huishi naye anaweza kukuambukiza. Sasa tukishindwa kufanya hivi then tunasubiri mujiza? Watanzania tumeweza vingi itatushinda Corona? Tuache ujinga? Hii ni self hygiene ambayo tulifundishwa tangu tupo primary!
Hili swala ni kujikabidhi kwa mungu tu hizo kinga zote USA, itaria spain na nyingineso wanazijua na pia wanajikinga more expensive tofauti na kinga hizo mchwara iko hivi mungu atusamehee tu na hii corona atuache tu maana hii kula kwa jasho ni adhabu tosha ila sio corona ikifika tumeisha wote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuh hawa cnn wanatutafuta nin wafrika ila leo asubuh nimetazama aljazira wanasema UK kuna shortage ya medical equipment na New Yorke ICU zipo down zimelemewa, mpaka napatwa na woga

Kuhusu Afrika nafikir Mungu kaweka mkono wake tu coz endapo tungekua na maambukiz kama western countries basi mtaani kungekua na vifo vingi visivyoeleweka

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa sasa tusiseme sana maana ule muda uliotarajiwa kwa Afrika kuangamia haujafika bado.

Hao wanaopukutika sasa, maambukizi kwao yaliingia mwishoni mwa mwezi January. Wakaanza kupukutika mwezi March. Sisi Afrika umeingia mwanzoni mwa mwezi March, kama kutakuwa na kupukutika, tutarajie kuanzia mwishoni mwa April. Tukivuka mwezi May bila ya maambukizi makubwa na vifo vingi, basi Muumba wetu kaamua kutuwekea kinga ya muujiza na wala siyo jitihada zetu.
 
Waafrica ...corona ingetusamehee tu maana , nikiona watu wanavyoishi maisha ya kuunga unga + corona naumia sana roho.

Usiende mbali..ni wangap wana bima?..yaani bima tu kwetu ni shida...kutibiwa ni km betting vile .!dah..itupitie kushoto aisee
 
Binadamu ana mucus kwenye njia ya hewa, hii ni sehemu ya kinga ya mwili. Hewa ikiingia na uchafu unakamatwa na mucus na uchafu ule unautoa kama kohozi.

Mucus goblets zikishambuliwa na virus ndiyo mafua yanachuruzika na huweza kukohoa. Maambukizi yakitokea kwenye mucus membrane husababisha kikohozi. Ndiyo maana unatumwa kikohozi ili wataalamu wagundue ni maambukizi gani.

Covid-19 hushambulia njia ya hewa na maambukizi huleta joto mpaka centi grade 38-39. Mucus goblets zinashambuliwa kwa kasi na Hutoa makohozi. Mapafu hukosa oxygen.

Afrika maisha yetu ni ya kufanya maoezi muda wote. Si kwa kupenda ni lazima utembee kwakuwa huna nauli ya basi na Gari huna. Mapafu yanakuwa imara. Pia vyakula tunavyokula ni organic.
Hii sio logic wenzetu wangu ndio wanaongoza kufanya mazoezi na wanadondoka daily kule watu asubuhi na jion ni tizi tu na wengine wanashinda gym lakini wanadondoka sisi ndio kabisa hakuna desturi ya mazoezi na pia kumbuka takwimu inasema USA brack america ndio wanaongoza kufa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Corona ikiamua kuua hapa africa.hakuna atakayeweza KUTUOKOA..
sasa hizo tahadhari zao wanazozitoa ni kama kututisha.
ebu jiulize MBONA WAO WALISHINDWA KUJITABIRIA?..
Kwanini wao wawe na uwezo wa kututabiria sisi kuwa tutakufa sana wakati wao ndo wanaongoza kwa vifo?
tumekusikia.... kama wao na world class health care wamekamatwa hivi, ikifika kwetu per se tutafanya nini? weka kando neno wasitutishe...

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
Usiende mbali..ni wangap wana bima?..yaani bima tu kwetu ni shida...kutibiwa ni km betting vile .!dah..itupitie kushoto aisee
Hata kama una Bima lakini ventilators hazitoshi
Look sisi tunajiingiza kwenye Mega projects lakini hospitali zetu utasema ni machinjio ya wagonjwa
Maji safi na salama hakuna ila tunaenda kununua Ndege kubwa na ghali sana kwa cash
 
sijawahi kwenda Mloganzila. Ila najua ventilator hawana na hata kama zipo, wakikuwekea akaletwa "kigogo" wanaondoa kwangu wanampa kigogo.
Umeona hiki kitanda. Hapo ukipelekwa oxygen imepungua mwilini ujue utapona kwa kudra za Mungu tu.
20200412_120247.jpg
 
Kwanini wao wawe na uwezo wa kututabiria sisi kuwa tutakufa sana wakati wao ndo wanaongoza kwa vifo?
walifanya makosa kama tunayoyafanya now! Wanatutahadhalisha tusifanye makosa hayo
 
Back
Top Bottom