PostGE2025 CNN: Mwanamke huyu aliyepigwa risasi alikuwa na ujauzito wa miezi 3

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Dah so sad, mkuu hii video ni wapi mi nilidhan ni Crokon pemben
Ni pale mianzini msikitini barabara ya kupanda kiding'a pembeni ya duka la vipodozi, fremu ya pili kuna jamaa anauza matunda

Mara nyingi nakuwepo hapo sema ule muda alipopigwa risasi nilikuwa kwenye baa 1 hapa kona nairobi ya chini ambapo napo zilirushwa risasi nne tulipokuwa tumekaa bahati nzuri hazikumpata mtu bali ziliharibu ukuta na viti.... Hadi muda huu ukija kwenye hii baa kuna matundu ya risasi
 
Hii video ya huyu mama inasikitisha sana
 
Hii video ya huyu mama inasikitisha sana
Kwa sisi watu wake wa karibu tunaumia zaidi mkuu, huyu mama nachezaga nae karata, tunataniana na ni mteja wangu kwa bidhaa ninazouza.
Ana watoto wawili wote wanasoma
 
Watoto wake walichukua mwili wake?
Ndio, wadai haki walichukua mwili wake wakishirikiana na familia na wameshazika. Pia walijitolea wakachanga wakaijengea familia nyumba nzuri sababu walikuwa wakitumia nyumba ya udongo

Kwao ni barabarani kabisa ukiwa mianzini ukiulizia wanakuonesha
 
anaitwa nani?nani alithibitisha kuwa ni mjamzito wa mapacha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…