CNN, Sky news, Aljezeera, BBC, New York Times, Daily Mail, CBS, DW, Finacial Times vyaunga mkono hotuba ya Magufuli kuhusu Test kits

Inaelekea imepenya; pole sana, sina namna ya kukusaidia cuz' it's your choice!
Nipe logic ya point yako are you sure wewe uko sahihi??? Wewe si mjinga??? Toa proof kupitia statement ya rais kuonyesha alichosema ni ujinga na wewe una akili kuliko wale wanaoiunga mkono
 
Msimamo usioyumbishwa! Hiyo ndiyo picha aliyoitengeneza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, baada ya kueleza waziwazi mashaka yake juu ya mashine zinazotumika kupima sampuli za wagonjwa wa Corona.

Akizungumza kutokea Chato, mkoani Geita wakati wa hafla fupi ya kumwapisha Waziri wa katiba na Sheria, Mwigulu Nchemba, Rais Magufuli alieleza wasiwasi wake juu ya mashine hizo huku akitolea mfano jinsi sampuli kutoka kwenye papai, mbuzi na ndege aina ya kware zilivyotoa majibu kuonesha kwamba wahusika wana maambukizi ya Corona.

Kauli yake hiyo, imeripotiwa na vyombo vikubwa vya habari duniani, kuanzia televisheni za BBC, DW, CBS, VOA, AL Jazeera, Sky News, CNN na kadhalika, huku magazeti ya New York Times, Financial Times, Daily Mail, The Guardian, Times of India yakiipa uzito habari kuhusu alichokizungumza.

Shirika la Habari la Reuters, nalo pia limeiripoti habari hiyo kwa ukubwa katika vyombo vyake mbalimbali, na kuzidi kuifanya hotuba ya Magufuli kuwa mjadala unaoumiza vichwa vya wanasayansi duniani kote kuhusu ubora na ufanisi wa vifaa vinavyotumika kupima Corona duniani kote.

Vyombo hivyo vya kimataifa, ambavyo mara kwa mara hushutumiwa kuandika habari mbaya pekee kutoka barani Afrika, safari hii vimejikuta vikiizungumzia habari ya hotuba ya Rais Magufuli kwa uzuri kwa sababu alichokibaini kuhusu ufanisi wa mashine hizo, kinahitaji mjadala mpana wa kitaalamu.

Katika hafla ya kumwapisha Mwigulu, Rais Magufuli alieleza jinsi sampuli kadhaa zilivyopelekwa kwenye Maabara Kuu ya Taifa, bila ya wataalamu wa maabara hiyo kujua kuwa si za binadamu, kisha majibu yakatoka kwamba sampuli hizo zilizokuwa zimepewa majina ya binadamu, zilikuwa na Corona wakati kiuhalisia zilikuwa ni sampuli za papai, ndege kwale pamoja na mbuzi.

“…Papai lile lipo halijafa linaiva tu. Mbuzi yule yupo tu hajafa, fenesi lile lipo tu labda lije kuoza… kwa hiyo natoa wito kwa Watanzania msiwe na hofu…mbona mafua yamekuwepo lakini haya ni makali, nayo yatapita…,” alisema Rais Magufuli katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla hiyo.

Vyombo hivyo vimeendelea kumnukuu Rais Magufuli akisema: “…Lazima ugundue kuna mambo ya ajabu yanafanyika nchi hii. Ama wahusika wa maabara wamenunuliwa na mabeberu, ama hawana utaalamu jambo ambalo si kweli kwa kuwa maabara hii imetumika sana katika magonjwa mengine. Ama zile sampuli zinazoletwa maana vifaa vyote vinatoka nje, hivyo lazima kuna kitu fulani kinafanywa.”

Rais Magufuli, ambaye hadi sasa anatajwa kuwa rais kutoka nchi za Kiafrika anayeheshimika duniani kote kutokana na kuwa na misimamo isiyoyumbishwa, alisema kutokana na taarifa hizo anaamini kuna watu ambao walipewa majibu yasiyo sahihi kwamba wameambukizwa Corona wakati si kweli na kuongeza pengine kuna waliopoteza maisha kwa sababu ya hofu.

Rais Magufuli pia alivishutumu vyombo vya habari vya kimataifa kwa namna vinavyoripoti kuhusu janga hilo nchini Tanzania licha ya kuwa vyombo hivyo vipo katika maeneo ambayo yameathirika na ugonjwa huo kuliko hata Tanzania

Zaidi, soma: Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria - JamiiForums
Leo ni siku ya saba hakuna kisa wala kifo kipya
 
Umenikumbusha mbali sana na hiyo stori ya mchizi wangu, ni yeye mwenyewe niliyemwambia nitampigia simu alinifuata akaniambia "we mbona unaharibu, oale kuna watu kwao wanaona simu kitu cha fahari sana halafu wewe unaongea kama utanipigia tu tupige story?

Kuhusu Sozigwa na backhanded compliment, inawezekana ali politicize, inawezekana alibaini mambo muhimu.

Lakini, kuhusu Magufuli, sidhani kwamba rahisi kujigamba kapima mapapai na mafenesi kwenye kipimo cha Covid-19 ni jambo la kusifia.

Kwanza kawavuruga watu kichizi, rais unaposema hizi tests mbovu, unatakiwa kuwapa watu alternative ya hizi test nzuri tumieni. Au tunaweka wanamaabara wazuri zaidi. Yeye kavuruga tu.

Mpaka kawapa sababu Wakenya wanakataa kuingiza ng'ombe wa Tanzania Kenya, wanasema mifugo ya Tanzania imepimwa na Magufuli na kukutwa na Covid-19. By the way kuna domestic cats wanepimwa wamekuwa wana hivi virusi.

Rais hata kama ana fanya uhakiki wa hizi testing procedures, anatakiwa kufanya methodically, kwa njia ambayo haitaleta mtafaruku, ananyata polepole, anaweka mtego, anagundua udhaifu, anauindoa udhaifu, anatangaza habari wakati kashamaliza kazi.

Siyo huyu anabwatuka tu, mara mabeberu, mara vipimo vibovu, mara kaugonjwa, anaonekana anataka ku confuse watu tu kwa kuwa hana mpango thabiti wa kukabiliana na janga hili.

Sent using Jamii Forums mobile app

Magufuli ni kama Trump tu. Wote hawa hawana filter.

Wanaongea tu kinachowajia akilini.

Hawapimi [athari] za maneno yao.

Unakumbuka juzi Trump alipozungumzia kuhusu mambo ya disinfectant?

Hakusema kwamba watu wanywe hizo dawa za kusafishia vyoo na mabafu na wala hakusema watu wadungwe sindano za hayo madawa.

Yeye alikuwa anazungumzia moja ya tafiti nyingi zinazoendelea kufanyika ili kupata dawa au kinga ya Corona. Mojawapo ya hizo tafiti ndo ilikuwa inahusisha hizo disinfectant. Ila kwa namna alivyoongea ndo akaishia kuonekana kituko.

Nashawishika kuamini kuwa serikali ya TZ ilifanya vile ilivyofanya [kupima mapapai na mbuzi na oili] kwa nia njema ya kujua kama mashine za kupimia corona zina dosari.

Ila sasa kwa jinsi Magufuli alivyoongelea ndo naye akaishia kuonekana kituko.

Ukiwa kiongozi ni muhimu sana kupima maneno yako. Ni muhimu sana kujua wapi, nini cha kusema, na namna ya kukisema ili usichanganye watu maana watu wengi wanakuchukulia wewe kuwa ni authority.

Hakukuwa na sababu ya Magufuli kusema kuwa wamepima hadi mapapai. Kwa walio wengi hilo lingeonekana ni kituko tu, hata kama sababu ya kufanya hivyo ni ya maana.
 
Nigrastratatract
CCM Mpya inafurahia mtaji wa ujinga ndiyo nguvu yake, imewafanya watu mateka kwa kuwaaminisha uhuru ni sawa na utumwa na mwisho kabisa CCM Mpya inaamini utulivu na amani lazima watu wafe na siyo kupitia njia ya amani ya ushawishi au nguvu ya hoja.
  • ignorance is strength
  • freedom is slavery
  • war is peace
Above Quotes from George Orwell's book titled 1984.
we mwenyewe umesoma kutokana na amani iliyojengwa na TANU na CCM kudadadeki.. halafu unatuletea Sijui umbumbu wako wa Nigrastractatract... acha ulofa ww!!
 
Short and clear, HAKUNA media yoyote kati ya hizo iliyomuunga mkono JPM! Zote zimeripoti alichoongea JPM; na pekee kilichoongozewa mbali na liyoongea JPM ni jinsi watu wanavyo-criticize suala zima la ufichaji takwimu, na jinsi Afrika ilivyo na maambukizi madogo huku waki-conclude vile vile kuna low testing level

Na kingine ni jinsi inavyoonekana tusivyo serious kulinganisha na majirani! In short, ukisoma katikati ya mstari utaona kilichopo ni kejeli kwa JPM kuliko kumuunga mkono!
2391313_FB_IMG_15887785827744689.jpg
 
Hizi habari za ubovu wa vipimo ,ilikuwepo kabla ya Magufuli kusema kapima mbuzi.

Tatizo ni pale mtu anapopima mafenesi, mapapai, mbuzi, ili kupima kipimo ambacho hakijatengenezwa kupima hivyo vitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ila kwa nchi walizoendelea kama South Korea na India nao wamevishtukia vipimo vya China.Unaweza ukakuta walitumia kama njia walizotumia Watanzania.

Nyie endeleeni kubisha,ila yeye aliamua kufanya upande wake kwa kutumia mbuzi,mapapai kujilizisha,mana mlivyo na NONGWA kama huko mbele ingekuja kugundulika vipimo vibovu mngeongea vilevile na kujipa unabii TULIJUA TULIJUA zingekuwa nyingi.

Hata USA nao walitumia kumpima Chui wakagundua ana Corona au kwa sababu kafanya Magufuli ndio isha kuwa nongwa au nao USA watakuwa wamekosea au vilaza ?

Tiger at New York's Bronx Zoo tests positive for coronavirus
 
Sawa, kupima mafenesi na mbuzi labda ni extreme.

Lakini pia, hiyo mitambo kutoa majibu kwa sample ambazo hata si za binadamu, ni ithibati tosha kabisa kuwa hiyo mitambo au sijui hiyo mashine, ni bomu kabisa na haifai hata kidogo.

Yaani hiyo mashine ilishindwa kugundua kuwa hizo sample si za binadamu?

Wazirudishe tu huko walikozinunua.
 
we mwenyewe umesoma kutokana na amani iliyojengwa na TANU na CCM kudadadeki.. halafu unatuletea Sijui umbumbu wako wa Nigrastractatract... acha ulofa ww!!

Hasira za nini, Hivyo ni hadaa kubwa kusema amani ililetwa na TANU au CCM. Historia niliyoisoma inatabainisha ni asili ya waTanzania kuwa watu wa amani hata hii CCM Mpya itapongolewa madarakani na kusaulika amani itakuwepo Tanzania. Huu mtaji wa Ujinga kuwa ni Nguvu ya CCM Mpya haukubaliki.
Nigrastratatract
CCM Mpya inafurahia mtaji wa ujinga ndiyo nguvu yake, imewafanya watu mateka kwa kuwaaminisha uhuru ni sawa na utumwa na mwisho kabisa CCM Mpya inaamini utulivu na amani lazima watu wafe na siyo kupitia njia ya amani ya ushawishi au nguvu ya hoja.
  • ignorance is strength
  • freedom is slavery
  • war is peace
Above Quotes from George Orwell's book titled 1984.
 
Laana katika nchi hii ilijificha mpaka ilipofika Oct 25, 2015
 
Ila kwa nchi walizoendelea kama South Korea na India nao wamevishtukia vipimo vya China.Unaweza ukakuta walitumia kama njia walizotumia Watanzania.

Nyie endeleeni kubisha,ila yeye aliamua kufanya upande wake kwa kutumia mbuzi,mapapai kujilizisha,mana mlivyo na NONGWA kama huko mbele ingekuja kugundulika vipimo vibovu mngeongea vilevile na kujipa unabii TULIJUA TULIJUA zingekuwa nyingi.

Hata USA nao walitumia kumpima Chui wakagundua ana Corona au kwa sababu kafanya Magufuli ndio isha kuwa nongwa au nao USA watakuwa wamekosea au vilaza ?

Tiger at New York's Bronx Zoo tests positive for coronavirus
Unaelewa kwamba vipimo vilitakiwa v8hakikiwe na serikali kabla havijaanza kutumika, na si baada ya kuanza kutumika.

Na katika hilo rais ameshindwa kutimiza kazi yake ya kuwalinda Watanzania?

Unaelewa kwamba hata kama unavihakiki vipimo, kuna njia za kitaalamu, sio kwa kutumia mafenesi na mapapai?

Unaelewa kwamba, rais kulialia huku anawalaumu wengine bila ya kutupa utatuzi wa tatizo la kupima Covid-19 ni kukataa wajibu wake na kuvuruga wananchi kwa kuwaambia vipimo vibovu bila kueleza vizuri wananchi watavipataje?

Unaelewa kwamba mtu mwenye Ph.D ya Chemistry kutumia mafenesi na mapapai kwenye kipimo ambacho hakijatengenezwa kwa lengo la kupima mafenesi ma mapapai ni kuidhalilisha hiyo Ph.D yake ya Chemistry?

Unaelewa Magufuki kashawapa sababu Wakenya wakatae mifugo ya Tanzania kwa kigezo kwamba mifugo ya Tanzania ina virusi hivi?

Unaelewa biashara ya mapapai na mafenesi inaanguka, watu wanaogooa mapapai na mafenesi yana coronavirus hii?

Unaelewa kwamba Tanzania inaficha idadi halisi ya watu wanaokufa kwa Covid-19, na Magufuli kamteua Mwigulu Nchemba, mtu aliyesema wazi kwamba anapendekeza serikali isitangaze wagonjwa na watu wanaofariki kwa Covid-19?

Unaelewa kwamba wananchi kuoewa habari muhimu za nchi yao inavyoendeshwa ni haki ya kikatiba, na kuficha huku habari ni kuvunja katiba ya Tanzania?

Unaelewa rais kaapa kuilinda katiba, na kuvunja katiba ni kuvunja kiapo cha urais?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msimamo usioyumbishwa! Hiyo ndiyo picha aliyoitengeneza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, baada ya kueleza waziwazi mashaka yake juu ya mashine zinazotumika kupima sampuli za wagonjwa wa Corona.

Akizungumza kutokea Chato, mkoani Geita wakati wa hafla fupi ya kumwapisha Waziri wa katiba na Sheria, Mwigulu Nchemba, Rais Magufuli alieleza wasiwasi wake juu ya mashine hizo huku akitolea mfano jinsi sampuli kutoka kwenye papai, mbuzi na ndege aina ya kware zilivyotoa majibu kuonesha kwamba wahusika wana maambukizi ya Corona.

Kauli yake hiyo, imeripotiwa na vyombo vikubwa vya habari duniani, kuanzia televisheni za BBC, DW, CBS, VOA, AL Jazeera, Sky News, CNN na kadhalika, huku magazeti ya New York Times, Financial Times, Daily Mail, The Guardian, Times of India yakiipa uzito habari kuhusu alichokizungumza.

Shirika la Habari la Reuters, nalo pia limeiripoti habari hiyo kwa ukubwa katika vyombo vyake mbalimbali, na kuzidi kuifanya hotuba ya Magufuli kuwa mjadala unaoumiza vichwa vya wanasayansi duniani kote kuhusu ubora na ufanisi wa vifaa vinavyotumika kupima Corona duniani kote.

Vyombo hivyo vya kimataifa, ambavyo mara kwa mara hushutumiwa kuandika habari mbaya pekee kutoka barani Afrika, safari hii vimejikuta vikiizungumzia habari ya hotuba ya Rais Magufuli kwa uzuri kwa sababu alichokibaini kuhusu ufanisi wa mashine hizo, kinahitaji mjadala mpana wa kitaalamu.

Katika hafla ya kumwapisha Mwigulu, Rais Magufuli alieleza jinsi sampuli kadhaa zilivyopelekwa kwenye Maabara Kuu ya Taifa, bila ya wataalamu wa maabara hiyo kujua kuwa si za binadamu, kisha majibu yakatoka kwamba sampuli hizo zilizokuwa zimepewa majina ya binadamu, zilikuwa na Corona wakati kiuhalisia zilikuwa ni sampuli za papai, ndege kwale pamoja na mbuzi.

“…Papai lile lipo halijafa linaiva tu. Mbuzi yule yupo tu hajafa, fenesi lile lipo tu labda lije kuoza… kwa hiyo natoa wito kwa Watanzania msiwe na hofu…mbona mafua yamekuwepo lakini haya ni makali, nayo yatapita…,” alisema Rais Magufuli katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla hiyo.

Vyombo hivyo vimeendelea kumnukuu Rais Magufuli akisema: “…Lazima ugundue kuna mambo ya ajabu yanafanyika nchi hii. Ama wahusika wa maabara wamenunuliwa na mabeberu, ama hawana utaalamu jambo ambalo si kweli kwa kuwa maabara hii imetumika sana katika magonjwa mengine. Ama zile sampuli zinazoletwa maana vifaa vyote vinatoka nje, hivyo lazima kuna kitu fulani kinafanywa.”

Rais Magufuli, ambaye hadi sasa anatajwa kuwa rais kutoka nchi za Kiafrika anayeheshimika duniani kote kutokana na kuwa na misimamo isiyoyumbishwa, alisema kutokana na taarifa hizo anaamini kuna watu ambao walipewa majibu yasiyo sahihi kwamba wameambukizwa Corona wakati si kweli na kuongeza pengine kuna waliopoteza maisha kwa sababu ya hofu.

Rais Magufuli pia alivishutumu vyombo vya habari vya kimataifa kwa namna vinavyoripoti kuhusu janga hilo nchini Tanzania licha ya kuwa vyombo hivyo vipo katika maeneo ambayo yameathirika na ugonjwa huo kuliko hata Tanzania

Zaidi, soma: Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria - JamiiForums
Eti ni Rais anayeheshimika Duniani pote,
Ama kweli wewe ni zero hasa, Rais anayeishi kwa kujificha eti anaheshimika labda na giza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaelewa kwamba vipimo vilitakiwa v8hakikiwe na serikali kabla havijaanza kutumika, na si baada ya kuanza kutumika.

Na katika hilo rais ameshindwa kutimiza kazi yake ya kuwalinda Watanzania?

Unaelewa kwamba hata kama unavihakiki vipimo, kuna njia za kitaalamu, sio kwa kutumia mafenesi na mapapai?

Unaelewa kwamba, rais kulialia huku anawalaumu wengine bila ya kutupa utatuzi wa tatizo la kupima Covid-19 ni kukataa wajibu wake na kuvuruga wananchi kwa kuwaambia vipimo vibovu bila kueleza vizuri wananchi watavipataje?

Unaelewa kwamba mtu mwenye Ph.D ya Chemistry kutumia mafenesi na mapapai kwenye kipimo ambacho hakijatengenezwa kwa lengo la kupima mafenesi ma mapapai ni kuidhalilisha hiyo Ph.D yake ya Chemistry?

Unaelewa Magufuki kashawapa sababu Wakenya wakatae mifugo ya Tanzania kwa kigezo kwamba mifugo ya Tanzania ina virusi hivi?

Unaelewa biashara ya mapapai na mafenesi inaanguka, watu wanaogooa mapapai na mafenesi yana coronavirus hii?

Unaelewa kwamba Tanzania inaficha idadi halisi ya watu wanaokufa kwa Covid-19, na Magufuli kamteua Mwigulu Nchemba, mtu aliyesema wazi kwamba anapendekeza serikali isitangaze wagonjwa na watu wanaofariki kwa Covid-19?

Unaelewa kwamba wananchi kuoewa habari muhimu za nchi yao inavyoendeshwa ni haki ya kikatiba, na kuficha huku habari ni kuvunja katiba ya Tanzania?

Unaelewa rais kaapa kuilinda katiba, na kuvunja katiba ni kuvunja kiapo cha urais?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo sasa hivi ni mapapai na mafenesi na si mbuzi uliyemtaja mwanzoni?

Na hao waliompima Chui USA hawajaelimika?

Na yule Chui aligunduliwa na Corona ina maana biashara ya utalii itaanguka?

Corona mpaka sasa haina utatuzi zaidi ya Trial and error zinazofanyika,utatuzi ni kufuata ushauri kutoka kwa wataalamu kama huna shughuli ya kufanya katulie nyumbani na kwa bahati nzuri unatolewa kila siku kwenye vyombo vya habari na wataalamu.

Tanzania inaficha idadi ya waliokufa kwani uliyokuwa nayo wewe wamekufa wangapi?

Au mnataka msikie leo wamekufa mia,kesho 200 ndio mjue serikali inayoyasema ni kweli.
 
You guys are very funny! Unajua Kiongozi wewe ni wa mtu wa tatu unakuja na similar argument kujibu post yangu!

Guys, mada inasema media tajwa hapo juu zimemuunga mkono Magufuli wakati ukweli ni kwamba, hakuna media yoyote kati ya hizo iliyomuunga mkono Mgufuli! Walichofanya ni kazi ya media... kuripoti kile kile alichosema Magufuli!

Sasa Timu Magu kwao hiyo ndo wanaita kumuunga mkono Magufuli!

Sasa mbona mnatumia hoja ya mashine kuwa na fault kama defensive mechanism wakati hoja ni Magu kuungwa mkono wakati hakuna alipoungwa mkono?!

Kuhusu suala la mashine kuwa na faults kwangu sio hoja... inaweza kuwa hoja kwa mtu ambae hafuatilii habari za nje! Kwangu sio hoja kwa sababu issue ya fault imeanza kuripotiwa tangia mwezi March!

Suala la Magu lime-trend sana sio kwa sababu inaonekana ni habari mpya bali ni kwa sababu approach aliyotumia kufkia conclusion inaonekana ni kiroja!!

Lakini kwa upande mwingine, hapa naomba tusichanganye mambo!! Tusichanganye mambo kwa sababu wakati Magufuli alizozilisha maboga na maparachichi ni Laboratory Test Kits, kwa upande mwingine test kits zilizolalamikiwa sio Laboratory Test Kits bali Rapid Diagnostic Kits!
 
Kwa hiyo sasa hivi ni mapapai na mafenesi na si mbuzi uliyemtaja mwanzoni?

Na hao waliompima Chui USA hawajaelimika?

Na yule Chui aligunduliwa na Corona ina maana biashara ya utalii itaanguka?

Corona mpaka sasa haina utatuzi zaidi ya Trial and error zinazofanyika,utatuzi ni kufuata ushauri kutoka kwa wataalamu kama huna shughuli ya kufanya katulie nyumbani na kwa bahati nzuri unatolewa kila siku kwenye vyombo vya habari na wataalamu.

Tanzania inaficha idadi ya waliokufa kwani uliyokuwa nayo wewe wamekufa wangapi?

Au mnataka msikie leo wamekufa mia,kesho 200 ndio mjue serikali inayoyasema ni kweli.
Serikali inayosema ya kweli yapi?

Wewe unakubaliana na namba za Ummy Mwalimu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya rais Magufuli kuwahutubia Watanzania na kuwajulisha kuwa vipimo vya COVID-19 vina mashaka na kuelezea hatua za kiintelijensia zilizochukuliwa kuyabaini mashaka hayo na mapapai, mafenesi na hata mbuzi "kukutwa" na COVID 19.

Hotuba hiyo haikushia kuwa ni kwa ajili ya Watanzania tu, ime "trend" na kuwa ni hotuba kwa dunia nzima, kuanzia vyombo vya habari vikubwa vya kimataifa mpaka kwenye "social medias" vinaizungumzia habari hiyo.

Nchi zingine serikali zao zimeshaanza kuchukuwa hatua za kufanya majaribio kivyao na kuchunguza, na watu binafsi na wao hawakubaki nyuma kuanza kuchunguza kila sina ya vipimo vya kichina, hata vile vya kupima joto.

Hongera Magufuli Hongera Tanzania.

Kwa hili naona hata wachongaji wetu maarufu wa mitandao ya kijamii wameufyata.
 
Back
Top Bottom