Anamaanisha vyombo vya habari mbali mbali vya dunia vinaongelea habari za Rais wa Tanzania kuwa mtu intelligent na smart sana. Hivyo kwa hotuba yake inayohusu mashaika ya vaipimo vya Corona na matokeo yaliyopatikana baada ya kupima makamasi ya mbuzi, majimaji ya papai, maji maji ya fenesi, kware n.k na kutoa majibu chanya kwa Covid 19, imbayo mataifa anuai wameitafsiri kilugha chao imeamsha dunia na kumfanya rais na TZ kuwa gumzo duniani.
Kwamba imewasthua mataifa mbali mbali na watu binafsi kuanza kufanya uchunguzi wa majaribio zaidi ya vipimo hivyo. Hata wale watengenezaji wa vipimo, hawajakikimbilia kukanusha kama vile wabongo wa mitandani wanavyokimbilia kuita vipimo fake, matokeo fake, mashine iko sahihi imepikwa kuona korona tu kama hakuna kipimo cha mtu, nk.
Kwa Lugha nyepesi, wasiomwelewa Rais wetu katika hili wanahitajika kulinda heshima zao kwa kukaa kimya kwanza. Hii ngoma ni daraja lingine!. Tumuunge mkono rais wetu kwa kuendelea kuwa makini na kuchukua tahadhari kwa mambo yote! Yaani Corona, maisha yetu hadi misaada n.k.