Cocacola kubandika majina ya watu bila ruhusa/malipo, Jacline Wolper aomba wanasheria kuingilia kati

Cocacola kubandika majina ya watu bila ruhusa/malipo, Jacline Wolper aomba wanasheria kuingilia kati

Ndo maana akasema baada ya kupelekewa kopo hakupiga picha badala yake alianza kutafakari mazingira aliyopelekewa zawadi na hii kutafakari ni pamoja na kutafuta ushauri na sio SYMPATHY juu ya haki yake aliyonayo kwa jina lake kutumika katika tangazo la kibiashara kama alivyoomba wanaharakati wampe msaada wa kujua haki zake katika hili suala...

Yeye anapelekewa kopo hata haulizi ni la nini? Anapokea tuu. Likimlipukiaje?

Aende zake huko. Ruge angemwekea pesa za Escrow kwenye account yake angeenda kutafuta ushauri huko Insta?

Ushauri akatafute kwa wanasheria siyo insta.
 
mkuu sasa hapa unachanganya mambo, wao hapa wanahitaji msaada wa kujua haki yao ni ipi kuhusu majina yao kutumika katika matangazo ya kibiashara probably kisheria ambayo sio proffesional yao, sasa unaposema watumie impact yao naona kama unachanganya mambo hapa...haimaanishi kwamba kwakua Wolper ni msanii superstar kibongo bongo ofcourse, basi atakua anajua haki zake zote na hana haja ya kuomba msaada kwa masuala asiyokua na ufahamu nayo!!, hapa utakua unakosea boss...

Sasa kama sheria siyo professional yao waende kwa wanasheria kutafuta ushauri wa kisheria badala ya kulialia kwenye mitandao.

Kwani Rihanna ni mwanasheria? Mbona hakulialia kwenye mitandao baada ya image yake kutumika bila ridhaa yake?

Yeye alitafuta lawyer kesi ikaenda mahakama akashinda akafidiwa mkwanja wake.

Hivi Wolper anaweza kuunga foleni na watoto yatima kwenye mlango wa mwananaharakati kuomba ushauri au tuseme legal aid?
 
Yeye anapelekewa kopo hata haulizi ni la nini? Anapokea tuu. Likimlipukiaje?

Aende zake huko. Ruge angemwekea pesa za Escrow kwenye account yake angeenda kutafuta ushauri huko Insta?

Ushauri akatafute kwa wanasheria siyo insta.

Suala la pesa za Escrow kuwekewa kwenye account ni tofauti kabisa na zawadi ya kopoz, pia wanasheria wapo insta vilevile inaweza kuwa sehemu mojawapo ya kupata contacts zao wanasheria...
 
Suala la pesa za Escrow kuwekewa kwenye account ni tofauti kabisa na zawadi ya kopoz, pia wanasheria wapo insta

Haya basi tunasubiri tuone kesi yao mahakamani kama wana huo ubavu.

Wasitegemee wanaharakati wawasadie kwa sababu wako bize kuwasaidia the most disadvantaged people in the society na siyo hawa maselebu wanaotamba kuwa wanaishi large.

Mtu unaletewa kopo hata hujiulizi, inawezekana hata maji yaliyokuwa mle ndani keshayanywa halafu ndo anakuja kulalama mitandaoni?

vilevile inaweza kuwa sehemu mojawapo ya kupata contacts zao wanasheria...

Kama wana "heshima kubwa" kama anavyodai hana haja ya kutafuta wanasheria insta.
 
Sasa kama sheria siyo professional yao waende kwa wanasheria kutafuta ushauri wa kisheria badala ya kulialia kwenye mitandao.

Kwani Rihanna ni mwanasheria? Mbona hakulialia kwenye mitandao baada ya image yake kutumika bila ridhaa yake?

Yeye alitafuta lawyer kesi ikaenda mahakama akashinda akafidiwa mkwanja wake.

Hivi Wolper anaweza kuunga foleni na watoto yatima kwenye mlango wa mwananaharakati kuomba ushauri au tuseme legal aid?

kwahiyo unamaanisha watoto yatima pekee ndio wanastahili kwenda kwa wanaharakati kuomba ushauri!!??, wanasheria wapo kwenye mitandao pia hata humu JF lipo jukwaa la SHERIA ambalo linatoa ushauri kwa watu mbalimbali wenye kuhitaji ushauri au unadhani na JF sio mtandao!!???
 
Haya basi tunasubiri tuone kesi yao mahakamani kama wana huo ubavu.

Wasitegemee wanaharakati wawasadie kwa sababu wako bize kuwasaidia the most disadvantaged people in the society na siyo hawa maselebu wanaotamba kuwa wanaishi large.

Mtu unaletewa kopo hata hujiulizi, inawezekana hata maji yaliyokuwa mle ndani keshayanywa halafu ndo anakuja kulalama mitandaoni?

Kama wana "heshima kubwa" kama anavyodai hana haja ya kutafuta wanasheria insta.

sawa sawa mkuu kama watakua wanasoma humu watakua wamekuelewa na nadhani ushauri wako wataufanyia kazi...
 
kwahiyo unamaanisha watoto yatima pekee ndio wanastahili kwenda kwa wanaharakati kuomba ushauri!!??,

Nimetumia watoto yatima kama one of the most disadvantaged people in the society.

Sasa unaweza kusema mlalamikaji ni one most disadvantaged people in the society kiasi cha kuhitaji kusaidiwa na wanaharakati?

Kwamba tumfanyie huyu mlalamikaji a "professional work undertaken voluntarily and without payment or at a reduced fee as a public service"? No way!! Alipe.

wanasheria wapo kwenye mitandao pia hata humu JF lipo jukwaa la SHERIA ambalo linatoa ushauri kwa watu mbalimbali wenye kuhitaji ushauri au unadhani na JF sio mtandao!!???

Kama kweli upo serious, kama kweli unahitaji ushauri wa kisheria the best option ni kutafuta mwanasheria na kukushauri professionally.

Yes, kwenye mitandao kuna wanasheria, lakini vipi kama wakimpa ushauri mbaya na yeye aka-act upon to her detriment, ataweza kuja kuwashtaki wanasheria wa mitandaoni for their negligence?

Wafanye kama alivyofanya Rihanna. Watafute mwanasheria awashauri kama wana case. Kama wana kesi waipeleke kampuni ya Coca Cola mahakamani na kudai fidia kwa kutumia "majina" yao bila "ridhaa" yao.

Narudia tena https://www.jamiiforums.com/celebri...ngo-acheni-kulilia;-fanyeni-kama-rihanna.html
 
Tatzo unaongea tu wala hujiongezi kusoma.soma bandiko kisha rudi

utaratibu waliokuwa wakitumia walikuwa wanafuata msanii,wanamweleza kuwa wametumia jina lake,wanampatia soda ya jina lake na kumpiga picha na kuingiza mtandaoni sasa unakurupuka huko unaandika ujinga. tazama hapa chini. unadhalilika kwa kuandika ugoro hapa
E.png

F.png
G.png

Kujielewa na kujua thamani yako ni kitu muhim sana maishani. So sad these people don't know their values. This is and wil definetely promote coca cola. Maskin, wanawafanyia kazi bure, coca cola wanaingiza hela kupitia haya matangazo, wao wanachopata ni kuuza sura. So sad, wamefanya matangazo kwa kulipwa soda moja lenye jina lao tu.

Eti "thanx coca I got myn", mwingine "ahsante coca na mimiapa", masikin hata kiswahil chenyewe kuandika shida.

Poor them, wasanii wetu wengi hawajitambui.

Pamoja na kutojitambua kwao, coca cola kwa hili wamefanya uhuni mkubwa. Wametumia udhaifu wao wa kutojitambua kuwanyonya, wamewafanyisha matangazo ya bidhaa yao ya coca cola bila kuwalipa. Huu ni wiz wa mchana kweupe. Kuwashtaki itakuwa ngumu coz wengi hawajasajil majina yao km brand, but coca cola wanatakiwa waambiwe walichofanya wamekosea na ni unyonyaji mkubwa. Somebody must tell them.
 
sawa sawa mkuu kama watakua wanasoma humu watakua wamekuelewa na nadhani ushauri wako wataufanyia kazi...

Alitakiwa awe ameshashariwa na mwanasheria au PR wake kwanza kabla ya kukimbilia Inta kuandika aliyoandika.

Kuuza CD feki ni kosa na la jinai. Lakini kampuni kutumia jina lake bila ridhaa yake ni suala la madai.

Ajaribu kwenye kuripoti polisi kuwa Coca Cola wametumia jina lake bila ridhaa yake aone kama watamsadia.
 
Mkimaliza kubishana mniambie niwapatie coca zenye id zenu
 
kwanza unajichanganya sijazungumzia kwamba waliopewa zawadi ni wasanii tu la hasha, waliopewa zawadi ni watu wenye majina maarufu katika jamii ambayo ni target ya kutangaza katika soko bidhaa hii,

Sasa nilipojichanganya ni wapi? Unaweza kunionyesha?

halafu pia sijaona watu wa kawaida wakisema wamepewa zawadi za kopo kama walivyofanya hao super stars!!!

Kwa vile tu wewe hujaona hiyo haina maana kuwa hakuna. Usichanganye mambo.
 
wolper bana... Njaa kali.. Sasa simple kweshen ana hati miliki ya hilo jina???? From there ndo unaweza ku'claim... Ingekuwa picha sawa.. Ila jina.. No way.. Sio registered brand.. Hakuna mwana wa sheria atakayeshulika na upuuzi huo.. Ndo maana kila siku mnashauriwa fanya jina lako kuwa brand na lisajili.. Kama unaoona wolper wapo wengi we ongeza tu iwe woolper kuleta utofauti then sajili... Mbweha wewe!!!!

Ushauri ni nzuri sana ...lakini matusi ya nn ndugu? Naamini hajui na anahitaji msaada wa kueleweshwa bila jazba....
 
Kujielewa na kujua thamani yako ni kitu muhim sana maishani. So sad these people don't know their values. This is and wil definetely promote coca cola. Maskin, wanawafanyia kazi bure, coca cola wanaingiza hela kupitia haya matangazo, wao wanachopata ni kuuza sura. So sad, wamefanya matangazo kwa kulipwa soda moja lenye jina lao tu.

Eti "thanx coca I got myn", mwingine "ahsante coca na mimiapa", masikin hata kiswahil chenyewe kuandika shida.

Poor them, wasanii wetu wengi hawajitambui.

Pamoja na kutojitambua kwao, coca cola kwa hili wamefanya uhuni mkubwa. Wametumia udhaifu wao wa kutojitambua kuwanyonya, wamewafanyisha matangazo ya bidhaa yao ya coca cola bila kuwalipa. Huu ni wiz wa mchana kweupe. Kuwashtaki itakuwa ngumu coz wengi hawajasajil majina yao km brand, but coca cola wanatakiwa waambiwe walichofanya wamekosea na ni unyonyaji mkubwa. Somebody must tell them.

CC to Nyani Ngabu
 
Last edited by a moderator:
WOLPER5566.jpg

Kampeni mpya ya Vinywaji Baridi ya Coca cola Kutumia Majina ya watu maarufu na Mastaa wa filamu Nchini na Kuipa jina la #shareacokeTz imeanza kulalamikiwa baada ya mmoja wa wigizaji Maarufu hapa Nchini Tanzania JACKLINE WOLPER ambaye jina lake limewekwa katika makopo hayo kudai ni utapeli kwani hakujulishwa na hakulipwa lolote.

Hapa chini ni Andishi lake katika mtandao.

"habari Followers pamoja na wa Tanzania wote ambao naamini huwa mnaingia katika page yangu ya insta.Nimepokea zawadi hii ya coca cola kwa siku 6 ,Na sio kwamba sikutaka kupiga picha kama wenzangu au ku post kama wenzangu ,nilikuwa natafakari Kweli Kampuni kubwa ya Kitaifa Na Kimataifa inaweza kutumia gharama kubwa kuandika majina Yetu bila kuchukuwa hata nafasi na heshima kubwa tuliyonayo kutushirikisha tu katika makubaliano ya kuandika majina Yetu Katika Makopo Yao.

Maana Naamini maFan's wa woolper wangeweza kushare na coca cola kutokana Jina Langu kuwa label katika makopo yao.Sasa Naamini tuna wanaharakati,wabunge,wanaSheria pamoja na serikali ambao huwa wanafwatilia wale wauza CD wa kariakoo basi Naomba Juhudi hizi mzihamishie huku katika kampuni hii kubwa ya Kimataifa coca cola ili kutetea haki za Wasanii na sio kudhalilishwa kwa kiasi hiki jamani.sijui kama wasanii wenzangu walilipwa siwezi kuwasemea lakini haya ni mawazo yangu binafsi. #shareaCokeTz"

CHANZO: Harakati news

- For sure ametumwa kuandika kitu asichokijua amelipokea kopo amelipiga picha na kulitundika Instagram halafu anasema hakutaka, kweli akili ni mali sana kabla hawajamletea wamempigia simu wakamwambia wana kopo lenye jina lake wanagependa kumletea akakubali bila ya kumuwekea bunduki kwa mbali, wakamfuata akawasubiri akalipokea akalipiga picha nalo akaweka Instagram leo analia hakutaka, hahahahahahahahaha hawa ndio wasanii wa yule jamaa yenu wa Njiro, hahahahahahahahaha

Le Mutuz
 
we ulilipwa sh ngapi? au na wewe umetumika tu
 
wolper bana... Njaa kali.. Sasa simple kweshen ana hati miliki ya hilo jina???? From there ndo unaweza ku'claim... Ingekuwa picha sawa.. Ila jina.. No way.. Sio registered brand.. Hakuna mwana wa sheria atakayeshulika na upuuzi huo.. Ndo maana kila siku mnashauriwa fanya jina lako kuwa brand na lisajili.. Kama unaoona wolper wapo wengi we ongeza tu iwe woolper kuleta utofauti then sajili... Mbweha wewe!!!!

Ni kweli kabisa inabidi hawe na intellectual property lasivyo anajiaangaisha tu,hopeless elimu inahitajika kwa hawa watu.
 
Back
Top Bottom