Napenda kumshukuru Mola kwa malezi niliyopewa katika kufundishwa mengi pia ya maishani na kuaminiwa na wazazi kuwa akili tulibarikiwa wote.. ni furaha sana kwangu.
Hii kitu nataka sana niipitishe kwa wanangu na kuhakikisha wao na cousins wao nao wanakuja kuacha mengi mazuri.
Hapa mfano mmoja ni sisi kuwa na marafiki wa kifamilia na kuheshimiana nao hadi leo hii kuishi vizuri katika shida na raha.. na wengine kwenye jamii na kutokuwa na maringo yotote ukibarikiwa au lolote kuishi vizuri na watu ambao huwezi kuona tofauti yangu kwao labda ujue. Na kuwaachia ya kuweza kujimudu mwenyewe kimaisha na kutokuwa mvivu na kujiamini kuanzia kwenye masomo, kikazi, kutokuwa na tamaa, kujali kujijengea jina kikazi na kibiashara bila kupitia mikato isiyo na maana na yakukushusha.
Bila kusahau kushindana na wanaume kwenye masomo kutafuta maksi za juu.. ha ha haaaaa niliwapa umiza vichwa.. kujiamini na kutokuogopa mtu huku ukiwa na heshima pia.