Na hakika hiyo umeipata bila kudhani? Kumbuka suala si hakika tu, bali hakika iliyopatikana bila kudhani.
Kwa maana umeshakubeza kudhani kwa kusema kwamba anayedhani hana hakika na hivyo hana ukweli.
Unaweza kudhani na baadae ukawa na uhakika
Unaweza ukadhani bila kuwa na uhakika hadi wakati unajadili hilo
Lipi kati ya hayo mawili unayomaanisha wewe?
Unaweza kudhani na baadae ukawa na uhakika
Unaweza ukadhani bila kuwa na uhakika hadi wakati unajadili hilo
Lipi kati ya hayo mawili unayomaanisha wewe?
Una moyo sana! bado tu unapoteza mda kujadili na huyu GOD hater
Kama unaweza kudhani na baadaye ukawa na uhakika, then your earlier dismissal of kudhani as kutokuwa na uhakika is moot, and made with a myopic logic.
Moreover, hujajibu swali langu kama uhakika wa kujua kwamba wewe upo umeupata bila ya kudhani au la.
I suspect that that is deliberate, as the obvious contradiction is indefensible.
Una moyo sana! bado tu unapoteza mda kujadili na huyu GOD hater
Usiwe na haraka unaposoma unachoandikiwa ...
Nimekuwekea uchaguzi wa aia mbili hapo ambao kimsingu hafanani kwasababu kuna time frame ya kudhani
Ya kwanza unadhani kwa muda halafu baadae unatoka kwenye kudhani kisha unaingia kwenye uhakika
Ya pili unadhani hadi wakati unajadili jambo husika,yaani hadi unajadili jambo lenyewe bado unakuwa kwenye kudhani bado
Umeona tofauti?
Sentensi ya maana kwenye maelezo yako yote hayo ni hiyo ya mwisho tu na ninajibu kwasababu ya hiyo hiyo na sio hayo mashauzi yako mengine ambayo hayana maana zaidi ya kuonesha kitu kimoja kinaitwa "lumbogo"Kama kuna anayefanya haraka kusoma anachoandikiwa ni wewe, hukuhitaji kurudia kwani nimekuelewa tangu mwanzo.
Kipi kimekufanya ufikiri sijaelewa? Nimelielewa hilo, na mapungufu yake, tangu namsoma St. Augustine 1999.
Hujajibu swali langu.
Una hakika gani ambayo umeipata bila kudhani?
Na kama kuna hakika inayokuja baada ya kudhani, unawezaje kubeza kudhani kama kukosa hakika?
Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao unaruhusu mabaya wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauruhusu mabaya?
Hujajibu hili swali.
Unasema mungu kaumba mabaya kwa wabaya.
Kwa nini karuhusu ulimwengu ambao mabaya yanaweza kuwezekana at alll wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Hujajibu swali hili.
Sentensi ya maana kwenye maelezo yako yote hayo ni hiyo ya mwisho tu na ninajibu kwasababu ya hiyo hiyo na sio hayo mashauzi yako mengine ambayo hayana maana zaidi ya kuonesha kitu kimoja kinaitwa "lumbogo"
Nilisema na ninasema ukiwa na hakika huna kudhani hivyo kudhani sio kuwa na hakika
Huwezi kupata uhakika bila kuanza kudhani lakini kudhani sio kuwa na hakika ...!
Hili swali ulishaliuza sana na mimi nimeshawahi kukujibu sana tu.
Swali lako linaanzia kuuliza katikati ya mada.sidhani kama unajua lolote kuhusu ADAM au kwanini wewe kiranga unaamini kwamba wewe ni Mwana wa Adam.Jibu la swali lako lipo ktk historia.
Kwamfano wewe nikuulize kwanini kunaongezeko la joto duniani? huwezi kunijibu kwa mkato.
ulimwengu wa mabaya ni historical impact.ndio maana naendelea kusimama palepale MABAYA NI KWAAJILI YA WABAYA.TUTAKAPOACHA UBAYA HAKU UBAYA.
Kwanza unajuaje kwamba mimi naamini kwamba mimi ji mwana Adam?
Sali langu linaanziaje kuuliza katikati ya mada wakati linauliza principles alizotumia mungu kuuumba ulimwengu kabla ulimwengu haujaumbwa?
Nimekuuliza, mungu alipokuwa anaumba ulimwengu, kabla ya chochote kiwapo, alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu wowote ambao aliutaka.
Aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.
Hakuumba ulimwengu huo.
Akaamua kuumba ulimwengu huu ambao mabaya yanawezekana.
Huwezi kusema aliamua kuumba hivyo kwa sababu ya wabaya, kwa sababu wabaya hawakuwapo. Kumbuka swali linahusu kabla ulimwengu haujaumbwa.
Hujajibu swali.
Kabla ulimwengu haujaumbwa, kwa mapokeo yenu, mungu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu wowote alioutaka.
The closest opposite to Satan is not God, but Gods servant, Michael the archangel.if their is evil and wrong doings then an equal and greater opposite exists and that is God
Very good answer.Una moyo sana! bado tu unapoteza mda kujadili na huyu GOD hater
Nimekupa jibu zuri kwamba ni suala la historia.
Na historia yoyote tunayoisoma ni lazima uhusishe imani hata kama historia husika itafanyiwa scientific proofe/evidence,kwakuwa hatuwepo lazima ubaki na imani.
Sasa kiranga hutaki kusema chochote/kuamini kuhusu Adam.
Umejiridhishaje kwamba fafanuzi zilizopo ni ulimwengu kuumbwa na mungu au kutokea wenyewe tu?
Unajuaje kwamba wewe fikra zako za kwamba ama ulimwengu umeumbwa na mungu ama kutokea wenyewe si fikra za kufuata kitu kama line ya reli inayoweza kwenda mbele na nyuma tu bila kujua kwamba kuna juu na chini?
Unajuaje kwamba hakuna fafanuzi nyingine zaidi, fafanuzi ambazo labda hata hatujapata elimu ya kuzielewa kwa sasa?
Na kama ulimwengu huu kwa jinsi ulivyo, in terms of order/intelligence, ni lazima uwe umeumbwa na mungu, then hilo linatueleza kwamba order/intelligence huwa haitikei tu, ni lazima ipangwe/iumbwe.
Kama ni hivyo, mungu aliyeumba ulimwengu yeye ana order/intelligence zaidi ya ulimwengu aliouumba.
Kama ni hivyo, ufafanuzi wako unazalisha swali lingine, ikiwa intelligence/order ninlazima oumbwe na haiwezi kutokea yenyewe (ndiyo maana unasema ulimwengu ni lazima uwe umeumbwa na mungu, na hauwezi kiwa umetokea wenyewe tu) je huyo mungu aliyeumba ulimwengu na mwenye intelligence na order kuliko ukimwengu naye kaumbwa na nani?
Maana kwa mujibu wa kanuni yako inayosema kwamba hakuna order/inyelligence inayoweza kutokea yenyewe tu, ni lazima iwe na muumba, hata mungu wako atahitaji muumba, na muumba wake atahitaji muumba, na muumba wake atahitaji muumba, ad infinitum, ad absurdum.
Unajikuta umemfanya mungu wako kuwa si mungu at all, bali ni a small cog in an infinite machine.
Unaona habari zako zinavyojichanganya na kujipinga zenyewe sasa?
Kwa jusema ulimwengu hauwezi kutokea wenyewr bula kuumbwa na mungu, undirectly umesema hakuna mungu.
Kwa maana mungu utakayemsema kauumba ulimwengu naye atahitaji mungu, na mungu wake atahitaji mungu, ad infinitum, ad absurdum, kama nilivyotaja hapo juu.
Habari ya mungu inajikanganya kwa mara nyingine tena.
Pia unasema ameuumba ulimwengu hivi kwa sababu, na angetaka kuuumba ukimwengu bula maovu angeumba.
Kusema hivi hakujibu swali langu.
Swali langu halikusema kwamba kaumba ilimwengu inaoruhusu maovu bila sababu, limeuliza kwa sababu gani?
Hujajibu swali.
Hujanipa sababu iliyomfanya mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwebgu ambao inaruhusu maovu yasiyosemeja wakati alokuwa na uwezo wote wa kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezekani.
Hujalijibu swali hili.
Nikikuuliza, kwa nini unatembea hivyo? Ukinijibu "kwa sababu", unakuwa hujajibu swali kimantiki.
Kwa sababu hujanipa sababu inayokufanya utembee hivyo.
Ndicho ulichofanya hapa.
Badala ya kunipa sababu iliyomfanya mungu aumbe ulimwengu unaoruhusu uovu, unaniambia kaumba ulimwengu hivyo jwa sababu.
Umekimbia swali, hujajibu swali,
Nipe japo mfano tu ambao ulimwengu pengine unawezapatikana kwa njia tofauti na kutokea tu wenyewe au kuumbwa na mungu?
Let's be focused on whether god created the universe or not.
If you make that claim, then you have to justify it by showing how this universe was created by god.
Which you haven't.
In fact, I have made a logical point that the universe couldn't have been created by god. Which you haven't refuted.
Mimi hata nikishindwa kuonesha njia yoyote ile ambayo ulimwengu umeanza hakuthibitishi kwamba mungu yupo.
Thibitisha kwamba mungu yupo na kaumba ulimwengu.
Mkuu hivi huwa unauliza maswali ili upate kueleweshwa au unauliza kwa kukomoa? Hebu rudia kutizama maswali na maelezo yako ambayo yaliyopelekea mie kukuomba unipe mfano,halafu tizama na ulivyokuja kunijibu.