Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
We unaporojo tupu.
Cha kukushauri tu ni kwamba kuwa makini na unachokiandika.
Unapenda ubishi lakini hauwezi.
Kama nina porojo tupu ungeweza kuzionesha hizo porojo ziko wapi.
Kusema mimi nina porojo tupu bila kuzionesha ziko wapi ndiyo porojo tupu yenyewe.
Narudia kwa msisitizo ili wote waelewe.
Kwa kusema mimi nina porojo tupu bila kuonesha porojo ni zipi na kwa nini ni porojo, wewe ndiye unajionesha kuwa na porojo tupu.
Kati ya mimi niliyekupa nafasi ya kuthibitisha kwamba mungu yupo na wewe unayesema mungu yupo lakini hujaweza kuthibitisha kwamba yupo nani anahitaji kuwa makini na anachoandika? Nani ana porojo tupu?
Kati yangu mimi niliyekuonyesha contradiction ya mungu wako ambaye mnasema ana ujuzi wote, upendo wote na uwezo wote lakini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana, na wewe ambaye ymeshindwa kuitengua hiyo contradiction, nani anahitaji kuandika kuwa makini? Nani ana porojo tupu?
Kati yako wewe unayesema binadamu kaumbwa na mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote na mimi nikiyekuuliza kama binadamu kaumbwa na mungu mjuzi hivyo mbona anakunya mavi, a very inefficuent misuse of energy, ina maana mungu hakujua kuwa energy efficient, ukashindwa kunijibu, nani anahitaji kuandika kwa makini? Nani ana porojo tupu?
Kati yangu mimi niliyeuliza kama mungu wenu kweli anapenda watu wawe huru kuchagua mbona hajatupa uhuru wa kuchagua kama tunataka kuzaliwa au hatutaki kuzaliwa, na wewe uliyeshindwa kunijibu, nani anahitaji kuandika kwa makini? Nani ana porojo tupu?
Kati yangu mimi niliyekuuliza kama mungu wenu kweli anapenda watu wawe na uhuru wa kuchagua, mbona hajatupa uhuru wa kurudi nyuma kwenye muda tubadili makosa tuliyofanya, na wewe uliyeshindwa kunijibu, nani anahitaji kuandika kwa makini? Nani ana porojo tupu?
Kati yangu mimi ninayepoint out vitu specific katika arguments zangu na wewe unayeleta majibu ya jumla jumla kama "wewe una porojo tu" ambayo hata hayachambui kitu, nani anahitaji kuandika kwa makini? Nani ana porojo tupu?
To the very contrary.
Wewe ndiye unahitaji kuandika kwa makini zaidi ya umakini wa zaidi wowote ninaohitaji mimi.
Wewe ndiye mwenye porojo tupu.
Hata unaposema mimi nina porojo tupu, ni porojo tupu.
Nimekuuliza maswali, umeshindwa kuyajibu, huwezi kuniambia siwezi ubishi.
Wewe uliyeshindwa kujibu maswali ndiye usiyeweza ubishi.
