Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Hayo yote ya uweza wote na ujuzi wa Mungu nayajua,lakini sijaona ukieleza ni vp iwe kwa huyo mtu tu ndiyo iwe inawezekana kuwa na moja ktk mawili yasioendana(usafi na nyumba chafu).
Kwa sababu huyo mtu kuwa haiwezekani kuwa na sifa ya usafi halafu akawa na nyumba, si kwamba hana ujuzi wote na uwezo wote.
Kama nilivyosema mwanzo, unataka kujadili vitu vikivyokuzidi kimo, hapo ndipo tatizo lako linapoanzia.
Twende polepole.
Kwanza kabisa sijaonhelea popote mtu kuwa na ujuzi wote na uwezo wote.
Sijui hilo unalitoa wapi.
Nilichoandika hapa ninkwamba, mungu, narudia, mungu -si mtu, mungu, soma tena, mungu, si mtu- mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote ambaye pia kaumba ulimwengu huu ambao mabaya yanawezekana, hayupo. Kwa sababu hayo mawili (mungu mwenye uwezo, ujuzi na upendo wote kwa upande mmoja, na ambaye kaumba ulimwengu huu unaowezekana mabaya hata pale alipokuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani) yanapingana kama moelekeo ya pande mbili za shilingi, yote kuwezekana pamoja ni sawasawa na mtu kurusha shilingu juu halafu iangukie kwa pande zote mbili kuangalia juu.
That is two mutually exclusive events happenning at once!
Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kwa nini aumbe ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo na sababu zote za kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?