COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu

COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu

Kiranga hujui kama unakufuru Ila Mungu Mwenyez Muumba wa vitu vyote amekuona na amekusikia utajibu on the judgement day!

Kabla ya yote unaweza kuthibitisha mungu yupo?

Maana isije kuwa unakariri hadithi tu zisizokuwa na ukweli wala kuweza kuthibitika.
 
Mungubwenu anajipinga.

Huku tunaambiwa ana uwezo wote, ana upendo wote, ana uwezo wa kufanya chochote anachotaka.

Huku kwingune tunaambiwa kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.

Kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Unaona jinsi ulivyokosa uhuru? huwezi kueleza imekuaje ukaacha ukristo na kuwa Atheist. Katika hali kama hiyo unajionaje kuwa una uhuru wa mawazo?

Halafu mnakuja humu na kusema ukristo na uislamu ni sawa tu,acha kupotosha wenzio waambie watafute ukweli huko mliko ni kuzidi kujitia mashaka.
 
Habari za mungu uzushi.

Kupinga ni jambo rahisi.

Unaweza kunithibitishia kuwa kusema hakuna Mungu si uzushi?

Nakushauri sasa uchunguze na imani yako badala ya kuchunguza mambo ya Pope kuwa ni Atheist,au chunguza zaidi kuhusu huyo pope.
 
Minyororo ipo huko mnaposhindwa kumuelewesha mtu mnachoelewa na kuishia kutoa jibu jepesi tu kuwa huyo mtu hana elimu.

Kati yako wewe ambaye umeshindwa kuthibitisha mungu yupo, umeshindwa kuondoa contradiction ya mungu mwenye uwezo wote na upendo wote kuunba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana na mimi ninayekuuliza maswali nani kashindwa kumuelewesha mwenzake?

Na inakuwaje kushindwa kumuelewesha mtu kuwe ni minyororo?

Kama mtu ni mjinga kupita kiwango cha kuweza kueleweshwa, nikishindwa kumuelewesha hapo nani yupo kwenye minyororo?
 
Kupinga ni jambo rahisi.

Unaweza kunithibitishia kuwa kusema hakuna Mungu si uzushi?

Nakushauri sasa uchunguze na imani yako badala ya kuchunguza mambo ya Pope kuwa ni Atheist,au chunguza zaidi kuhusu huyo pope.

Tunarudi kule kule. Tatizo la elimu ndogo.

Kuthibitusha ni suala linalohusika na vilivyopo. Kama mungu yupo, mimi naweza kukuuliza wewe uthibitishe. Kama hayupo, huwezi kuniuliza mimi nithibitushe kwamba hayupo. One cannot prove a negative.

Ni sawa na mimi nokuulize uanze kuthibitisha kutokuwepo kwa taa ya dhahabu inayoelea sebuleni mwako.

Kama hii taa gaipo, utaanzia wapi kuthibitisha kwamba haipo?
 
mkuuu kiranga labda jibu ni hili kaumba yote hayo mabaya kuwezekana kwa sababu ndo alivotaka na tafsiri ya kitendawili hicho anaijua yeye na hakuna mwanadam atakaeweza kukitegua......tafsiri ya kwamba hili ni baya ni kwa maono yako na yangu ya kibanadamu......kama unakataa basi tuambie wewe vilivyopo duniani vizuri na vibaya vimetokea wapi au vimeletwa na nani??at least utushawishi kuamini uyatakayo.....usiseme sijui mana hata katika mtihani ukiwa hujui basi unafeli mtihani pia usitoe mfano wa maumbo ya geometry au square root ya mbili...tuliosoma hesabu ndo tunakuelewa ..wasiopita huko unawachanganya...tafuta mfano rafiki kwa wootee
 
Bora kuwa na elimu ndogo kuliko kuwa na upeo mdogo.

Hujaelewa swali.
 
mkuuu kiranga labda jibu ni hili kaumba yote hayo mabaya kuwezekana kwa sababu ndo alivotaka na tafsiri ya kitendawili hicho anaijua yeye na hakuna mwanadam atakaeweza kukitegua......tafsiri ya kwamba hili ni baya ni kwa maono yako na yangu ya kibanadamu......kama unakataa basi tuambie wewe vilivyopo duniani vizuri na vibaya vimetokea wapi au vimeletwa na nani??at least utushawishi kuamini uyatakayo.....usiseme sijui mana hata katika mtihani ukiwa hujui basi unafeli mtihani pia usitoe mfano wa maumbo ya geometry au square root ya mbili...tuliosoma hesabu ndo tunakuelewa ..wasiopita huko unawachanganya...tafuta mfano rafiki kwa wootee

Hilo si jibu.

Hapo umekubali hujui jibu.

Ukikubali hujui jibu umekubali humuelewi huyo mungu.

Ukikubali humuelewi, huwezi kumuelezea na inawezekana hayupo kabisa, kwa sababu unaamini kitu usichokielewa.
 
Upeo mdogo zaidi ya kutoelewa swali ni kusema swali halijaeleweka bila kuelewesha halijaeleweka wapi na vipi.

Swali langu linauliza kama unaweza kuthibitisha madai ya kwamba hakuna mungu si uzushi?
 
Unawezaje kusema hakuna Mungu kwa uhakika kabisa halafu ukashindwa kuthibitisha ni vp hakuna Mungu? Unakimbilia kusema Mungu kajipinga wakati umeambiwa uthibitishe kutokuwepo kwake.
Wahanga wa ukristo mnatabu sana.
 
Mungu yupo kimacho nifanya niamin haya..Ni the way Ulimwengu ulivyo umbwa katika namna y ajabu nay a kushangaza, Ukiangalia mimea kwa namna zake, wanyama mbalimbali, mito na mabonde, bahari maziwa na mito ilivyotandazwa kwa ustadi wa hali ya juu….huwez ni ambia kwamba vyote hivi vilifanyika bila ya kuwepo Muumbaji nyuma yake, Vitu kama Upepo, Hewa havionekani lakini twajua vipo as tunavifili na kuvisikia…katika hali ya namna hii….Hata kama simuoni huyu Mungu nina mwamini,

Naamini katika Biblia, Inasema katika Isaya, “It is I who made the earth, and created man upon it. I stretched out the heavens with My hands and I ordained all their host. (Isaiah 45:12)” Watu amabao walikuwa hawamwamini Mungu walikuwepo hawakuanza leo na Biblia inawatammbua hapa ina sema. “Only fools say in their Hearts,There is no God.” (Psalm 14:1)

Personal unaweza kumu exppirience Mungu nah ii ndio njia Bora zaidi ya Kuelezwa na watu, hatua za awali ni Mtu kwanza kuamini kwamba Mungu yupo, Biblia pia inagusia kuhusu hili, “Anyone who wants to come to Him must believe that there is a God” (Hebrews 11:6). Na pengine inasema “Mithali 8:17. "Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona"
 
Unawezaje kusema hakuna Mungu kwa uhakika kabisa halafu ukashindwa kuthibitisha ni vp hakuna Mungu? Unakimbilia kusema Mungu kajipinga wakati umeambiwa uthibitishe kutokuwepo kwake.
Wahanga wa ukristo mnatabu sana.

Mungu ninayemsema hayupo nishaeleza kwa nini hayupo.

Anajipinga mwenyewe kama "pembetatu duara".

Usichoelewa kwamba "pembetatu duara" haipo, na mungu wenu anajipinga mwenyewe kama pembetatu duara ni kipi?
 
Back
Top Bottom