Sasa hapo mbona hata huonyeshi kuwa Mungu kaumba huu ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kwa sababu alishindwa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Maana mwenyewe unasema kabisa "kaumba ulimwengu mabaya yanawezekana licha ya kuweza kuumba ulimwengu mabaya hayawezekani".
Pia umeshindwa kuonesha kuwa amejipinga, kwa sababu kama haujaonyesha kuwa huu ulimwengu wenye mabaya ni kwa sababu ameshindwa kuumba ulimwengu usio na mabaya,kwahiyo ulimwengu huu ambao mabaya yanawezekana haukuumbwa kwa sababu ilishindikana kuumbwa usio wezekana mabaya hivyo ni suala la uamuzi wake, na tukiangalia sifa zake zinathibitisha hili. Kwahiyo sioni alipojipinga.
Huelewi argument yangu.
Argument yangu ni kwamba, mungu wenu hawezi kuwapo kwa sababu anajipinga yeye mwenyewe.
Anajipinga yeye mwenyewe kwa sababu wenye uwezo, upendo na ujuzi hufanya mazuri yote wanayoyaweza kwa wawapendao na kuwaepusha na mabaya yote wanayoweza.
Mungu wenu mnasema ana uwezo, ujuzi na upendo wote. Angeweza kukiepusha kila kiumbe chake na mabaya, lakini hakufanya hivyo.
Kwa nini? Hujajibu kuondoa contradiction hii.
Swali lako la kwamba la kwamba sioneshi mungu kaumba ulimwengu huu wa mabaya kwa sababu kashindwa kuumba usio mabaya linaonesha logic ya argument yangu imeku challenge uwezo wako wa kuelewa vibaya sana.
Kama ningeonyesha kwamba mungu kaumba ulimwengu huu wa mabaya kwa sababu kashindwa kuumba usio na mabaya, kusingekuwa na contradiction. Nisingeweza kusema simuelewi mungu kwa nini kaumba ulimwengu huu wa mabaya. Kwa sababu sababu yake ingekuwa ndogo tu na rahisi kuielewa, alitaka kuumba ulimwengu usio na mabaya lakini hakuwa na uwezo huo.
Ni kama umkute baba mwenye ulemavu wa miguu na mikono, hawezi kufanya chochote, yuko mbali na watu, kaachiwa kitoto kichanga kinakufa kwa njaa. Umemkuta huyu baba hawezi hata kujiinua kukisaidia kichanga hiki. Huyu baba huwezi kumlaumu kwa nini laachia kichanga kinakufa, hana uwezo wa kukisaidia kichanga hiki, hata kama anataka kukisaidia.
Kwa hiyo swali lako sielewi limeyokana na fikira gani, lakini kimsingi no kutoelewa argument yangu.
Kama mungu wenu mngesema ana upendo wote lakini hana uwezo wote, halafu kaumba ulimwengu huu wenye mabaya kwa sababu kashindwa kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya, kwa sababu uko nje ya uwezo wake, hapo ungeweza kusema mungu hajipingi. Kwa sababu alitaka kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya, ila hana uwezo.
Ninaposema kwamba mungu anajipinga maana yangu ninkwamba mungu wenu mnamsema kwamba ni mungu wa uzuri na neema. Ana uwezo wote, ana ujuzi wote, ana upendo wote.
Ningemtegemea mungu huyu wa neema zote na asiyeshindwa kitu aumbe ulimwengu ambao mabaya hayawezekani. Hususan kwa sababu ana uwezo wite wa kufanya hivyo, ana ujuzi woye wa kufanya hivyo na ana uoendo wote qa kufanya hivyo.
Kwa nini hakuumba ulimwengu huo na kaamua kuumba ulimwengu huu?
Mimi binadamu tu sina uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote lakini nikienda kununua gari nikikuta mawili hapo, moja lina kila mushkeli wa kuweza kusababisha ajali na jibgine lenye kila kituge cha kupunguza ajali, nitanunua lile la kupunguza ajali.
Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, upendo wote na ujuzi wite achague ulimwengu ambao ajali haziishi wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao ajali haziwezekani?
Unapotoa jibu la "uamuzi wake tu", kimsingi unasema hujui jibu.
Unaposema hujui jibu, kimsingi unasema humuelewi vizuri mungu unayemuamini.
Unaposema humuelewi vizuri mungu unayemuamini, kimsingi unasema inawezekana kabisa ni mungu wa kanyaboya, unaamini katika mapoleo na utamaduni tu, lakini kiuhalisia mungu huyu hayupo.