Unang'ang'ania kusema ni contradiction lakini hadi sasa umeshindwa kuthibitisha ni contradiction kwa misingi ipi?
Na pia umeshindwa hata kutuonesha ni vp contradiction yako hiyo iwe ndiyo kigezo cha kutokuwepo uwepo wa mungu.
Contradiction ni kitu kimoja kuwa na natures mbili zinazopingana, kujipinga chenyewe kabla hakijapingwa.
Nimetoa mfano wa "pembetatu duara" in Euclidean geometry kuwa inherently contradictory, kwa sababu pembetatu haiwezi kuwa duara, na duara haiwezi kuwa pembetatu.
Vivyo hivyo, mungu wenu anajipinga.
Kivipi?
Mungu wenu mnasema ana ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote.
Mwenye ujuzi, uwezo na upendo hawezi kuacha mabaya yawafike anaowapenda kama anaweza kuyazuia.
Mungu wenu aliweza kuzuia mabaya yasiweze kutokea katika ulimwengu huu.
Lakini hakufanya hivyo, kwa muji u wenu, aneumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.
Mungu mwenye uwezo wite, ujuzi wote na upendo wote kama akitaka kiwa consistent na sifa hizo anatakiwa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani. Kwa sababu uwezo anao, ujuzi anao na upendo anao.
Ana kila sababu ya kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani na hana sababu ya kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.
Hata mwanadamu anapojenga nyumba tu, huwa anajitahidi kwa uwezo wake kujenga nyumba ambayo haitabomoka na kuua watoto wake.
Hawezi kusema "najenga nyumba itakayoporomoka dari na pengine hata kuua wanangu ili niwafundishe kuruka dirishani". Akisema hivyo, huju ana uwezo wa kujenga nyumba isiyoporomoka dari, atakuwa hana upendo kwa wanawe.
Sasa imekuwaje mungu mwenye upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote kaumba ulimwengu ambao ubaya unawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao ubaya hauwezekani?
This contradicts his nature.