COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu

Mungu hachunguziki kwa akili za kawaida ndo mana wapinga Mungu wana maswali kibao bila majibu...in short majibu ya maswali hayo mpaka uwe na akili zilizovuka mipaka..kwa maana akili za kiroho ambazo mimi na wewe hatuna....jaribu kufikiri ukifa unakuwa katika hali gan na unakwenda wap??? huwez pata jibu kirahisi unless ufe ndo utakuwa na majibu...ni system flan ilishawekwa na muumba ili kuwafikirisha watu zaidi..hapo ndo utaona kuwa hata wagunduzi wa vitumbalimbali waliumiza kichwa na baadae wakaja kujua ukweli......lakin mambo yooote kumhusu mungu basi ni tone la maji against maji ya bahari....huwez nahutoweza had unakufa...bora uchunguze zaid na zaid juu ya uwepo au kutokuwepo kwake kuliko kutoa hitimisho kuwa hayupo...bado kuna mengi sana hayajagunduliwa hapa duniani ..tafta ukweli utapata
 
Suala la contradiction tulikuwa tukilijadili unalikimbia.

Nimelikimbia wapi na kivipi?

Naomba unipe post namba au quote vipi nilivyolikimbia .

Mpaka sasa swali langu la kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote a uwezo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana (contradiction) hujalijibu, utasemaje nimelikimbia suala la contradiction?
 
Mungu hachunguziki kwa akili za kawaida ndo mana wapinga Mungu wana maswali kibao bila majibu...in short majibu ya maswali hayo mpaka uwe na akili zilizovuka mipaka..kwa maana akili za kiroho ambazo mimi na wewe hatuna....

Sasa kama ni hivyo mbona huwa mnamwelezea mungu humu?, na kumpa sifa kibao kwamba ni mungu wa upendo ,amani sijui na nini.Nyie mmejuaje hayo endapo unakili kabisa kwmba mungu haelezeki wala kuchunguzika kwa akili za kibinadamu?,nikisema sisi wanadamu ndiyo tunaomuumba mungu ntakuwa wrong?.
jaribu kufikiri ukifa unakuwa katika hali gan na unakwenda wap??? huwez pata jibu kirahisi unless ufe ndo utakuwa na majibu...

Kwa nini ufikirie kitu usichokijua?,swala la nini kinafuata baada ya kufa hakuna anaejue na ndio maana hata mungu mtoto(yesu)kama mlivomtunga hakusema pia alipokufa zile siku tatu nini kilitokea ama alikuwa wapi zaidi ya kile kitabu kikubwa kusema kwamba alikuwa kuzimu(ajabu kabisa mungu kwenda kuzimu).Inawezekana na yeye hajui pia.Kule kufikiria jini kinafuata baada ya kufa ndio mwanzo wa kumuumba mungu,na kujipa matumaini kwamba mtaenda kwake mkifa kama mmetenda mema.Huu ni udhaifu mkubwa sana
ni system flan ilishawekwa na muumba ili kuwafikirisha watu zaidi..
Umejuaje hayo ndugu?una mawasiliano ya katibu na huyo mungu ?,sio kwamba unahisi tu na hisia zinakutuma hivyo?
hapo ndo utaona kuwa hata wagunduzi wa vitumbalimbali waliumiza kichwa na baadae wakaja kujua ukweli......

Safi kabisa ndiyo maana dini ilikomalia kwamba dunia ni flat,ukoma ni laana na utumwa ni halali,Lakini sisi WATU tukajua ukwel baadae kwa hiyo sisi tunaakili kuliko hao mnaodhani wapo.
lakin mambo yooote kumhusu mungu basi ni tone la maji against maji ya bahari....huwez nahutoweza had unakufa...bora uchunguze zaid na zaid juu ya uwepo au kutokuwepo kwake kuliko kutoa hitimisho kuwa hayupo...bado kuna mengi sana hayajagunduliwa hapa duniani ..tafta ukweli utapata

Nashukuru umegundua hilo.Ndiyo maana miaka mingi ijayo wanadamu wakihamia sayar ya Mars inabidi watunge biblia na koran na kusema ""mungu aliipenda mars na kuiumba ili sisi tuhamie""
 
Mungu hachunguziki kwa akili za kawaida ndo mana wapinga Mungu wana maswali kibao bila majibu...in short majibu ya maswali hayo mpaka uwe na akili zilizovuka mipaka..kwa maana akili za kiroho ambazo mimi na wewe hatuna....jaribu kufikiri ukifa unakuwa katika hali gan na unakwenda wap??? huwez pata jibu kirahisi unless ufe ndo utakuwa na majibu...ni system flan ilishawekwa na muumba ili kuwafikirisha watu zaidi..hapo ndo utaona kuwa hata wagunduzi wa vitumbalimbali waliumiza kichwa na baadae wakaja kujua ukweli......lakin mambo yooote kumhusu mungu basi ni tone la maji against maji ya bahari....huwez nahutoweza had unakufa...bora uchunguze zaid na zaid juu ya uwepo au kutokuwepo kwake kuliko kutoa hitimisho kuwa hayupo...bado kuna mengi sana hayajagunduliwa hapa duniani ..tafta ukweli utapata

Kama mungu hachunguziki kwa akili za kawaida wewe unatumia akili gani kujua hizo?

Nisipopata jibu la swali kama nikifa nakuwaje ndiyo uthibitisho kwamba mungu yupo?
 
Bado hujajibu swali langu...(kama unaamini uwepo wa mungu) Je unaweza kunithibitishia kama mungu aliumba dunia yenye " mema na mabaya" tu?...au aliumba "ubaya" tu?...au "wema" tu?...au huamini uwepo wa mungu?
Naomba nijue msimamo wako ktk hili ndio niendelee kujibu swali lako vizuri.Kwa sababu,kila mfano wa huo " ubaya" unaouona wewe,unaona kwa wanadamu tu!..ilihali unajua kabisa kwamba kuna mamilioni ya viumbe hai nao wapo ktk dunia hii hii wakijaribu kuishi.
Suala la kuchukulia huyo MUNGU ni wa binadamu tu,to me that's a big LIE!.

Kwa nini unafikiri naamini katika kuwepo kwa mungu baada ya post zangu zote hizo za kupinga kuwepo kwa mungu?
 
ha ha ha Free ideas ntakujibu natafta namna nzuri ya kuyaweka majibu yangu pia nakwepa sana kutumia vitabu ambavo wewe huviamini lakin mwisho wa siku najikuta siwez kukwepa kutovitumia...naamin wewe umeshavisoma na ukaona huko ni chai tu..sasa nikirejea huko tena hutonielewa....ila all in all Kiranga na Free ideas nawakubali sana mnajua kujenga sana hoja japo siwaungi mkono upande mliopo mpaka dunia inaisha ila ki ukweli mnajua coconceptualize mambo katika mantiki za uelewa wa juu na ufasaha wa kufafanua mambo..thumb up
 
Last edited by a moderator:

Sawa ndugu Doyi nadhani hata Kiranga amekuelewa.
Cc Kiranga
 
Last edited by a moderator:
Nimelikimbia wapi na kivipi?

Naomba unipe post namba au quote vipi nilivyolikimbia .

Mpaka sasa swali langu la kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote a uwezo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana (contradiction) hujalijibu, utasemaje nimelikimbia suala la contradiction?

Unang'ang'ania kusema ni contradiction lakini hadi sasa umeshindwa kuthibitisha ni contradiction kwa misingi ipi?

Na pia umeshindwa hata kutuonesha ni vp contradiction yako hiyo iwe ndiyo kigezo cha kutokuwepo uwepo wa mungu.
 
Contradiction ni kitu kimoja kuwa na natures mbili zinazopingana, kujipinga chenyewe kabla hakijapingwa.

Nimetoa mfano wa "pembetatu duara" in Euclidean geometry kuwa inherently contradictory, kwa sababu pembetatu haiwezi kuwa duara, na duara haiwezi kuwa pembetatu.

Vivyo hivyo, mungu wenu anajipinga.

Kivipi?

Mungu wenu mnasema ana ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote.

Mwenye ujuzi, uwezo na upendo hawezi kuacha mabaya yawafike anaowapenda kama anaweza kuyazuia.

Mungu wenu aliweza kuzuia mabaya yasiweze kutokea katika ulimwengu huu.

Lakini hakufanya hivyo, kwa muji u wenu, aneumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.

Mungu mwenye uwezo wite, ujuzi wote na upendo wote kama akitaka kiwa consistent na sifa hizo anatakiwa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani. Kwa sababu uwezo anao, ujuzi anao na upendo anao.

Ana kila sababu ya kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani na hana sababu ya kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.

Hata mwanadamu anapojenga nyumba tu, huwa anajitahidi kwa uwezo wake kujenga nyumba ambayo haitabomoka na kuua watoto wake.

Hawezi kusema "najenga nyumba itakayoporomoka dari na pengine hata kuua wanangu ili niwafundishe kuruka dirishani". Akisema hivyo, huju ana uwezo wa kujenga nyumba isiyoporomoka dari, atakuwa hana upendo kwa wanawe.

Sasa imekuwaje mungu mwenye upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote kaumba ulimwengu ambao ubaya unawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao ubaya hauwezekani?

This contradicts his nature.
 
Sawa ndugu Doyi nadhani hata Kiranga amekuelewa.
Cc Kiranga

Mkubwa kashakubali.

Translation hapo naona anasema anatumia "cognitive dissonance" tu, kwa hoja katukubali.

Ndiyo maana anasema habari za kutupinga mpaka mwisho kabla hata hajajua kesho tutakuja na argument gani.

Jamaa anaweza kupinga vitu ambavyo hata hajavisikia bado.

Hatari.
 
Ni hatari,lakini bora huyu amekiri na kukubali kwamba maji ni marefu.Kuna ambao wanang'ang'ania hoja huku waki-comment nje ya mada huku wakidhani wako sahihi.
 
Mkubwa kashakubali.

Translation hapo naona anasema anatumia "cognitive dissonance" tu, kwa hoja katukubali.

Ndiyo maana anasema habari za kutupinga mpaka mwisho kabla hata hajajua kesho tutakuja na argument gani.

Jamaa anaweza kupinga vitu ambavyo hata hajavisikia bado.

Hatari.

Tatizo wanashindwa kupata ujasiri wa kuhoji juu ya kile wanachokiamini!.Ukizingatia walishaambiwa kwamba ni dhambi kubwa kuhuji juu ya muumba wao.

Hawa jamaa ni wepesi sasa,ukiwauliza sababu za mungu kutuumba utasikie eti ili tumwabudu na kumtumikia! So what?,

.Huwa najiuliza huyu mungu muweza wa yote na mwenye mamlaka yote anahaja gani ya kuabudiwa na mwanadamu?.Kwa nini ahitaji kuabudiwa na wakati yeye ana mamlaka yote,?Jwa maana hiyo mungu(kama yupo)kamgeuzwa mwanadamu mtumwa wake.

Aisee hii ni hatar sana.Lakini sio mbaya tuendelee kuwasaidia watoke ndani ya box.
 
Nilishauliza hayo maswali, hakuna aliyetoa jibu la kueleweka.
 
Kuabudu ni sehemu ya maisha ya mwanadamu kama kufanya kazi, kula n.k . Kuabudu kunaleta hali ndani ya mtu kujisikia safi, usalama na burudiko moyo. kama humwabudu Mungu kuna kitu utaabudu tu maishani mwako. Hivyo mwanadamu alikuwa designed kuabudu.
 
Alikuwa designed kuabudu na nani?

Kuabudu ni nini?
 
Kuabudu ni sehemu ya maisha ya mwanadamu kama kufanya kazi, kula n.k . Kuabudu kunaleta hali ndani ya mtu kujisikia safi, usalama na burudiko moyo. kama humwabudu Mungu kuna kitu utaabudu tu maishani mwako. Hivyo mwanadamu alikuwa designed kuabudu.

Alikuwa designed lini wapi na nani?,na kisha uthibitishe kwamba kweli mwanadamu alikuwa designed !.Tofauti na hapo unachokisemema hakina tofauti na story za vijiweni
 
Contradiction ni kitu kimoja kuwa na natures mbili zinazopingana, kujipinga chenyewe kabla hakijapingwa.

Nimetoa mfano wa "pembetatu duara" in Euclidean geometry kuwa inherently contradictory, kwa sababu pembetatu haiwezi kuwa duara, na duara haiwezi kuwa pembetatu.

Vivyo hivyo, mungu wenu anajipinga.

Kivipi?

Mungu wenu mnasema ana ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote.

Mwenye ujuzi, uwezo na upendo hawezi kuacha mabaya yawafike anaowapenda kama anaweza kuyazuia.

Mungu wenu aliweza kuzuia mabaya yasiweze kutokea katika ulimwengu huu.

Lakini hakufanya hivyo, kwa muji u wenu, aneumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.

Mungu mwenye uwezo wite, ujuzi wote na upendo wote kama akitaka kiwa consistent na sifa hizo anatakiwa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani. Kwa sababu uwezo anao, ujuzi anao na upendo anao.

Ana kila sababu ya kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani na hana sababu ya kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.

Hata mwanadamu anapojenga nyumba tu, huwa anajitahidi kwa uwezo wake kujenga nyumba ambayo haitabomoka na kuua watoto wake.

Hawezi kusema "najenga nyumba itakayoporomoka dari na pengine hata kuua wanangu ili niwafundishe kuruka dirishani". Akisema hivyo, huju ana uwezo wa kujenga nyumba isiyoporomoka dari, atakuwa hana upendo kwa wanawe.

Sasa imekuwaje mungu mwenye upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote kaumba ulimwengu ambao ubaya unawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao ubaya hauwezekani?

This contradicts his nature.

Kila mara unabadilisha tafsiri kila unapoona udhaifu wa hoja yako kupitia tafsiri uliyotoa,na mie kama kawaida yangu nakupeleka utakavyo.

Ningependa uniweke sawa jambo moja,unasema mungu anajipinga na umetoa tafsiri ya kujipinga. Pia umeeleza upande mmoja kati ya pande mbili ambazo unaona ndiyo zinatengeneza contradiction,na upande mmoja huo uliyoueleza ni upendo,uwezo wote na ujuzi wote.
Hizo ni sifa upendo,uwezo na ujuzi.Lakini huu upande wa pili umeeleza tukio tu lakini haujaeleza tukio hilo linabeba tafsiri gani? Tunajua ni yapi yanayobeba tafsiri ya upendo,na ni yapi yanayobeba tafsiri ya uwezo na mwisho tunajua ni yapi yanayobeba tafsiri ya ujuzi.

Hivyo upande wa pili tukio uliyoeleza hatujui limebeba tafsiri gani ili tuweze kulinganisha na tuone hiyo contradiction katika hivyo vitu viwili. Mungu alipoumba huu ulimwengu hakusema kwamba watu wataishi kwa raha(kwa maana kuishi bila shida yeyote) kwa sababu ya hizo sifa. Ila tunaona mungu ameyafanya maisha ya ulimwengu kuwa ni safari ili tufike ktk makazi aliyoyaanda kwa ajiri yetu sie wasafiri,iwe shida au raha vyote ni sehemu ya changamoto za safari.

Na ktk ulimwengu huu yapo mambo yenye kuonesha tafsiri ya upendo wa mungu,yapo yenye kuonesha ujuzi wake na uwezo wake. Sasa tukio unalolieleza wewe hatujui limebeba tafsiri gani na linatengua vp hizo sifa za mungu na kuondoa uwepo wa mungu?
 
First thing first, kila mara nabadilisha tafsiri vipi?

Wapi nimetoa tafsiri ya contradiction iliyo tofauti na hii?

Tukio la mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana ni contradiction inayobeba tafsiri ya kwamba kuna kitu uongo hapa.

Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote nature yake haiwezi kumruhusu kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.

Huyu mungu ataumbaje ulimwengu ambao mabaya yanawezekana? Kwa sababu gani aumbe ulimwengu huo?

Huyu mungu ana kila sababu ya kuumba ukimwengu ambao mabaya hayawezekani. Kwa sababu uwezo anao, ujuzi anao ma upendo anao.

Kama nilivyosema hapo mwanzo, mwenye uwezo hawezi kuacha mabaya yatokee wakati anaweza kuyazuia. Kwa nini baba ajenge nyumba ambayo anategeshea ianguke dari wakati ana uwezo wa kujenga nyumba ambayo dari haliwezi kuanguka na kuumiza wanawe?

Ikiwa baba wa kibinadamu mwenye akili za kibinadamu timamu, uwezo wa kawaida na upendo wa kibinadamu tu hafanyi hivyo, sembuse mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?
 
Maelezo yako hayajagusa majibu yangu na kuyatengua,ulichofanya ni kurudia maelezo yaleyale.

Labda kipya ktk hayo maelezo yako ni huko kueleza kuwa tukio ulilolieleza kwamba linabeba tafsiri ya uongo,sasa uongo na kujipinga ni vitu viwili hivyo tofauti .
 
Naufananisha Uumbaji wa MUNGU(kama yupo),na mfano huu ambao kwangu ni fumbo na halijapata jibu la kuridhisha.Please mfano huu hauna maana mbaya wala tafsiri yoyote mbaya ni mawazo yangu binafsi tu.

Twende sasa.................

Wote mnaijua Computer,na Virus pia mnajua maana yake.

Em tuanzie hapo,nitatumia mifano hiyo,MWANADAM,COMPUTER na VIRUS

MUNGU,(kama yupo),amemuumba

MWANADAM (Computer ),ambayo alitaka imfanyie kile alichoiagiza kufanya na imtii kwa kila alisemalo, na daima Computer hii ifuate maagizo yake.

Lakni kwa upande mwingine pia MUNGU(kama yupo),aliumba SHETANI(kama yupo)(VIRUS).virus hiz ni maalum kwa kuharibu System ya Computer na kufanya isiweze kufanya kaz vizur.Virus hawa huingia katika Computer na kufanya mwenendo wa utendaji wa Computer kuwa mbaya na mbovu.Virus huyu husababisha Computer isiweze kufanya kile ambacho ilikusudiwa kufanya kwa umakini.

Imefikia wakati sasa aliyeitengeneza Computer,kaingia vitani na kifaa chake mwenyewe alichokitengeza (Virus ),na kukilaumu kwamba kinamuharibia COMPUTER yake et kwa kuwa kinaisababisha kufanya yale asiyoyataka.Lakini kbuka Fundi alijua kabisa kabla kwamba Computer yake itahatibiwa na kifaa hicho(Virus ).

Computer (mwanadam),anaonywa na mtengenez wake kwamba asifuate yale ambayo pacha wake VIRUS,anataka bali Computer ifuate yale ambayo mtengenez anasema ifuate.

Computer (Mwanadam) inabaki njia panda kwa kuwa sasa mtengenezi wake anashindana na kifaa chake mwenyewe kuigombania Computer.Kila upande kuvutia kwake na kuulaum ipande mwingine.

Maswali mazito ambayo Computer(binadam)inajiuliza ni 1.Je kulikuwa na Umuhimu gani wa kutengeneza Virus(shetani),na kuiweka pamoja na Computer(mwanadam)

2.Iweje fundi ashindwe kuisambaratisha Virus(shetani ) anaona haina faida zaidi ya kumuharibia Computer(mwanadam) yake??.

3.Kwa nini Fundi,anaahidi kuichukulia hatua kali Computer(mwanadam) baadae,et kwa sababu haikufanya kile alichotaka??,je nikwel kwamba hakujua kwamba virus itaharibu Computer System ??

NB.,,ni mawazo huru tu,unaruhusiwa kukosoa ama chochote.
 
Back
Top Bottom