Kuna tatizo LA msingi ambalo Kama lisipotibiwa huu mjadala hautakuwa na mwisho.
Wewe unaye mungu uliyemtegeneza kichwani mwako then umempa Sifa na unatumia hizo Sifa za mungu wako kukana uwepo wa Mungu aliyeumba ulimwengu na kuanzisha uhai duniani.
Hutaki kuamini ni hoja ambayo inatolewa na binadam asiyefikiri vizuri, kwa binadamu anayefikiri Imani ndiyo msingi na chachu ya kupata ujuzi. Maana Kama huamini chochote huwezi tumia chochote kujifunza ama kugundua kitu. Ni budi uwe na Imani hata na utulivu na ukweli wa kile kidanywacho na ubongo wako na hata kile ambacho ubungo unakupa taarifa zake pasipo wewe kupanga.
Ujuzi huja baada ya kuamini kila utumiacho kuutafuta ujuzi husika.
Unaandika hapa JF ukiamini kuwa kile unachokiandika kitatokea kwenye mtandao ambao unaamini utafikisha kwa members na imani kuwa members wa JF watasoma na Unaamini kuwa wanaweza angalau kudecode lugha uliyotumia wakakuelewa na kukujibu. Hataka kuto taka Imani Bali ujuzi umetumia imani wala sio UJUZI.
Huna uwezo wa kujibu maswali hili Mimi nimejua kutokana na majadiliano nawe ya Mara nyingi.
Uliamini kuwa wewe ni smart na kudhani hoja zako hazijibiki na kwa "ulimbukeni" tu unakuwa hauko tayari kupokea changamoto za vitu vipya ambavyo viko kinyume na unavyoVIAMINI.
Mungu ninayemuamini ni yupi?
Na kwa nini unafikiri kusema sitaki kuamini kunapingana na falsafa ya kwamba imani ndiyo chachu ya ujuzi?
Unaelewa convergence ya kutoka kwenye imani na kwenda kwenye ujuzi ikoje?
Unaelewa kwamba bila kukataa kubaki kwenye imani na kukumbatia kuelekea kwenye ujuzi huwezi kuendelea kwenye ujuzi?
Wapi nimesema siamini chochote? Unajua tofauti kati ya kusema sitaki kuamini, nataka kujua na kusema siamini chochote? Naona kama unafanya assumption kwamba nikisema sitaki kuamini, nataka kujua ni sawa na nimesema siamini chochote. Assumption hii inatokana na kukosa kuelewa kwamba kuna vitu sina uwezo wa kuvijua (kwa mfano, sijui kama jua litachomoza kesho, linaweza kupata supenovae usiku wangu wa leo na kusiwe na kesho tukafa wote). Lakini logically speaking, the probability of this happening is miniscule. So I have no justification for postponing my meetings tomorrow because the sun might extinguish itself in a supernovae tonight .
Sasa kwa nini unione mtu kama mimi ambaye nitataka kujua exactly how much energy does the sun have left before it extinguishes itself in a supernovae, huku nikikubali kwa imani inayotathminiwa na mantiki kwamba jua litachomoza kesho kama mtu nisiyekubali kuamini katakata?
Kusema kwangu sitaki kuamini does not mean I will throw the baby with the bathwater. Ni kama mtu anayesema hataki nyumba chafu. Hilo halina maana ataichoma moto nyumba ili kusiwe na nyumba chafu. Akifanya hivyo atakosa pa kulala. Mtu mwenye reason ataisafisha nyumba chafu ili iwe safi. Na mimi vivyo hivyo, sitaki kubaki kwenye imani, nataka kujikwamua kutoka kwenye imani na ku converge kwenye ujuzi. Ukibweteka kwenye imani hata ujuzi huwezi kupata. Utapataje ujuzi wakati definition ya imani ni kukubali vitu bila uchunguzi? Ukishaanza uchunguzi unatoka kwenye imani na unaelekea kwenye ujuzi.
Unafanya assumption kubwa sana bila hata ya kuniuliza.
Kwa nini unaandikia mate na wino upo?
Ushafahamu tofauti ya kusema sitaki kuamini nataka kujua na kudhani kwamba mimi sikubaliani na ku entertain imani yoyote hata kwa sekunde moja?
Ukisema hutaki imani yoyote hata kwa sekunde moja, hata hesabu inayokuwa solved kwa kuanza na "let a = b" huwezi kui solve.
Because that involves a leap of faith.
Matatizo yangu si na imani per se, bali kwanza ni imani mbovu ambayo inakubali contradiction, halafu kubweteka katika imani.
Kati yangu niliyetoa hoja ambazo mpaka sasa hujazijibu na wewe unayefanya assumption ya kutokana na kufikiri nafikiri nisivyofikiri, bila hata kuniuliza, nani ni limbukeni hapa?
Wewe ni limbukeni kwa sababu una nafasi ya kuniuliza kama nina entertain imani in any format, lakini umekurupuka na assumption bila hata kuniuliza.
Ungekuwa unanisoma ungeshaona nilishawahi kuandika hapa haiwezekani binadamu asiwe na imani kabisa, kwani hata kitendo cha kuamka kutoka kitandani asubuhi kinahitaji imani kwamba sakafu haitapasuka na kukumeza mzima mzima.
Sasa utaandikaje kuhusu mimi kama mtu ambaye si entertain imani 100%? Kwa kuwa nimesema sitaki imani nataka kujua?
Mtu akisema hataki maginjwa, anataka afya, ni sawa na kusema hajawahi na hatawahi kuumwa hata mafua?
Unajua tofauti ya kusema sitaki imani nataka kujua na kusema sina chembe ya imani?
Inaonekana unachanganya mawili haya ambayo ni tofauti kabisa.
Limbukeni nani sasa hapa?