Tetesi: Col Joseph Karegire wa Jeshi la Rwanda auawa huko DRC Congo

Tetesi: Col Joseph Karegire wa Jeshi la Rwanda auawa huko DRC Congo

Watutsi ni watu wa ethiopia huko,wahutu wabantu,leo msukuma,mluguru na mmafia kuongea kiswahili hakuwafanyi kuwa kabila moja
Miaka zaidi ya 500 imewafanya kuwa ndugu tu...... kinachowatofautisha ni asili tu na muonekano.

Anyway....hili suala ni debatable....
 
..tusidharau machungu waliyoyapata, na wasiwasi walionao kuwa genocide inaweza kujirudia.

..vilevile tuwahimize wasiwe sehemu ya mauaji na mateso dhidi ya jamii nyingine, na majirani zao wa DRC.
Kama kweli wanatambua atrocities za genocide wangeshirikiana na DRC kulta amani ukanda huo. Wenyewe sasa wanafanya kinyume. Wengi wamekufa Congo kuliko waliokufa kwenye genocide yao.
Hawa kama si wabinafsi waandamizi tuwaiteje?
 
Kweni FLDR ni Wahutu pekee wanaoishi Mashariki ya Kongo wengi walirudi sema hawa wao wanataka kurudi kwa nguvu.
Pk alivyoshindwa kuwaunganisha warwanda kuwa wamoja instead off akaendeleza ukabila,ipo siku fdrl wataikamata rwanda tu
 
Vita vya Katanga Shaba ni Wakongomani wengi waliopoteza maisha kwa risasi na njaa.

..watu laki 1 wanakadiriwa kuwa walipoteza maisha ktk vita vya Congo vya miaka ya 60.

..vita vya Congo vilivyoanza mwaka 1998 inakadiriwa vimesababisha vifo vya watu zaidi ya millioni 3, wengine wanakadiria vifo zaidi ya millioni 6.

..Waafrika inabidi tujiulize tumefikaje hapo?
 
Mobutu alikuwa hata kulipa mishahara kwa Wanajeshi na Watumishi wa umma alikuwa halipi anawaambia wachukue kwa wananchi Mobutu ndio aliyeliuwa Jeshi la Kongo halijaamka mpaka leo.

Kagame alipowasaidia baada akina Kabila snr wakamgeuka na kusaidia kuasisi fldr.

Kagame sasa hivi anasaidia Msumbiji dhidi ya Magaidi wa Kiislamu na Msumbiji sasa huwaambii kitu kuhusu Kagame.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Huko msumbiji kaunda kundi la waasi kama anavyofanya Congo?
 
Huko msumbiji kaunda kundi la waasi kama anavyofanya Congo?
DRC ZAIRE ndio iliyoanza Kagame akamalizia iliwatuma Wanajeshi wake kuja kupigana na RPF iliyokuwa ikiongozwa na Rwigyema ukiingilia mambo ya ndani ya Nchi nyingine na wewe utaingiliwa tu.

Kwahiyo muacheni Kagame ajinafasi.

Na wale wote wenye chuki dhidi ya Rwanda nawaambieni hivi.
VISIT RWANDA
 
zaidi ya millioni 3,
Hakuna aliyewahesabu ni uongo tu wa Wazungu ambao ndio kiini cha matatizo wao ndio wameitengeneza Kongo ili liwe shamba la mfalme wao Leopold na kukata mipaka ya falme za Rwanda na Urundi.

Kabla hawajaja kuigawana Afrika tulikuwa hatuna migogoro tulikuwa wamoja hata hakukuwa na Genocide bali walianza wao huko Namibia na kuua Waherero na Wanama kwa mauaji ya kimbari ya kwanza Afrika.
 
Pk alivyoshindwa kuwaunganisha warwanda kuwa wamoja instead off akaendeleza ukabila,ipo siku fdrl wataikamata rwanda tu
Mimi ni Dereva wa Lory la mizigo huwa naenda Kigali Kamembe Bukavu Goma Gisenyi Bralirwa pale kwenye Mutzing.

Na huwa naongea na Wanyarwanda wa aina zote Wananchi wa Rwanda wanampenda raisi wao wanaipenda Nchi yao na sio kwamba wanaogopa kusema wakati wananiona kabisa mimi ni foreigner au "Mnyamahanga" kama wanavyoniitaga.

Rwanda imetulizwa chini ya Paul Kagame.

Hao FLDR wakiingia watapigwa hata na raia wa kwaida waitwao "Waturage".
 
Hakuna aliyewahesabu ni uongo tu wa Wazungu ambao ndio kiini cha matatizo wao ndio wameitengeneza Kongo ili liwe shamba la mfalme wao Leopold na kukata mipaka ya falme za Rwanda na Urundi.

Kabla hawajaja kuigawana Afrika tulikuwa hatuna migogoro tulikuwa wamoja hata hakukuwa na Genocide bali walianza wao huko Namibia na kuua Waherero na Wanama kwa mauaji ya kimbari ya kwanza Afrika.

..tusibishe tu kwasababu tunaweza kubisha.

..waliotoa hizo data ni mashirika yenye wataalamu wenye uzoefu wa kuchunguza mauaji wakati wa vita.

..mashirika hayo hayo unayopinga data zake ndio yaliyotoa takwimu za genocide ya Rwanda na hatukuzibishia.

..genocide au mauaji yoyote yale yanapaswa kulaaniwa.

..tunalaani genocide ya Watutsi ambayo ilisababisha watu wanaokadiriwa millioni 1 kuuwawa.

..tulaani mauaji ya Wacongomani zaidi ya millioni 6 ambao wameuwawa tangu mwaka 1998 vita vilipoanza.

..Waafrika tufike mahali tukatae unyama na aibu hii.
 
Habari za hivi punde ni kuuwawa kwa kiongozi wa mapambo wa jeshi la Rwanda nchi Congo.

Majeshi ya Rwanda yapo nchini Congo yakisaidiana na majeshi ya M23.

Mara kadhaa Paul Kagame amekuwa akikanusha kuhusika kwa nchi yake katika machafuko nchini Congo.

Kufuatia kifo cha Col Joseph Karegire ambaye alikuwa kiongozi mkuu wa operesheni nchini Congo sasa ni wazi tena pasipo shaka kabisa Jeshi la Rwanda limekuwa likishirikiana na M23 bega kwa bega.
RDF imeiteka Goma kwa gharama kubwa tu.

Tresor Mandala FRANCIS DA DON inamankusweke imhotep
 
..waliotoa hizo data ni mashirika yenye wataalamu wenye uzoefu wa kuchunguza mauaji wakati wa vita.
Usiyaamini sana hayo mashirika ni mara ngapi yanakutwa yakisafirisha silaha kama ile scandal ya msf.
 
mashirika hayo hayo unayopinga data zake ndio yaliyotoa takwimu za genocide ya Rwanda na hatukuzibishia.
Takwimu mara walikuwa wanasema 800000 na wengine wanasema ni millioni moja ukweli ni kwamba idadi kamili huenda hata ni zaidi.
 
genocide au mauaji yoyote yale yanapaswa kulaaniwa.

..tunalaani genocide ya Watutsi ambayo ilisababisha watu wanaokadiriwa millioni 1 kuuwawa.

..tulaani mauaji ya Wacongomani zaidi ya millioni 6 ambao wameuwawa tangu mwaka 1998 vita vilipoanza.

..Waafrika tufike mahali tukatae unyama na aibu hii.
💯 %
 
Takwimu mara walikuwa wanasema 800000 na wengine wanasema ni millioni moja ukweli ni kwamba idadi kamili huenda hata ni zaidi.

..sasa hebu fikiria idadi tunayoambiwa wamekufa DRC uhalisia unaweza kuwa ni zaidi ya kinachoripotiwa.

..fikiria watu wote wa jiji la Dsm wauwawe, halafu Waafrika tuko kimya, viongozi wanaingia wanatoka.
 
Sio Kongo hata mauaji ya Kimbari Viongozi wote wa Kiafrika walikuwa kimya bila Kagame kupambana huenda hata hao Watutsi kidogo wa Rwanda waliopona mauaji wangeuwawa wote.

Na Mobutu alituma hadi majeshi kuingilia mgogoro wa Rwanda badala ya kuwa msuluhishi.

Nyerere pia hakusikilizwa ndio maana alipokwenda Kigali alilia sana wakati wa mazishi ya wahanga wa Genocide.
 
..Nyerere angekuwa hai asingekaa kimya huku Wacongomani wakiuwawa kinyama.

..kama Nyerere alilia kwasababu ya genocide ya Watutsi millioni 1 nadhani angelia zaidi na kulaani vikali vifo vya Wacongomani millioni 6.
 
Nyerere pia alisema Watutsi wa Kongo no Wakongomani.
 
Nyerere pia alisema Watutsi wa Kongo no Wakongomani.

..Watusi ambao ni wazawa wa Drc hawapaswi kubaguliwa, au kujibagua.

..pia ni kipengele gani katika makubaliano ambacho M23 wanakilalamikia kuwa hakijatekelezwa?

..pia ni vipengele vipi katika makubaliano vimetekelezwa?

..pande hizo mbili zingekuwa wazi jumuiya ya kimataifa ingekuwa katika nafasi nzuri ya kusaidia.

..Watu millioni 6+ kupoteza maisha isichukuliwe kama jambo la mzaha. Tufike mahali Waafrika tuseme imetosha.
 
Back
Top Bottom