Tetesi: Col Joseph Karegire wa Jeshi la Rwanda auawa huko DRC Congo

Aibu.

Ipo wazi sasa.
 

..kuna kipindi James Kabarebe, afisa wa RDF, alikuwa ndio Mkuu wa Majeshi ya DRC.

..sasa huyu bwana alimkorofisha nini Mzee Kabila mpaka yeye na wenzake wakatimuliwa?

..Wacongo walishawapa Rwanda usukani wa jeshi la DRC, na free pass ya kuwauwa Interahamwe vile watakavyoona inafaa.

..Rwanda ingeishi vizuri na Mzee Kabila sidhani kama leo tungekuwa tunazungumzia hii vita, na watu zaidi ya millioni 6 kuuwawa kinyama.
 
Wacongo hawakutaka nchi yao na jeshi lao kuongozwa na wanyarwanda ndio maana Mzee Kabila aliamua kumtimua Kabarebe baada ya kelele kuwa nyingi, hilo liliukera Sana utawala wa Kigali, ndio chanzo cha kuivamia upya Drc na kuanzisha vita vya pili vya Drc.
 
Nilikuwa namuangalia James Kabarebe akihojiwa na TV moja ya Ufaransa alikuwa anasema kuwa walipofika Kinshasa alimpigia Kabila na kumwambia kuwa kazi ilikuwa tayari wameshaiteka Kinshasa yote.

Kabila akafurahi sana akaruka na Ndege hadi Kinshasa na kuapishwa kuwa raisi wa Zaire baada ya muda Kabarebe akwa anataka kurudi nyumbani lakini kabila akakataa na kumwambia abaki awe Mkuu wa majeshi ya Zaire kiasi anatafuta CDF mwingine.

Nitaitafuta hiyo clip niiweke hapa.

Please msikilize mwanzo mwisho ina subtitles za English

View: https://youtu.be/mECN7JSsnxY?si=LttxtXb-YglaedgN
 

..huyu Kabarebe anastahili lawama.

..Kabarebe alikuwa katika nafasi nzuri ya kujenga mahusiano mema kati ya Rwanda na DRC but he dropped the ball.

..muda wote Kabarebe alipokuwa Mkuu wa Majeshi ya DRC alishindwa nini kuwamaliza Fdlr na Interahamwe?

..Eneo la maziwa makuu liko vitani kwa uzembe wa huyu jamaa.
 
Weka Chanzo cha habari Sasa.


Tresor Mandala imhotep
Kwa kirundi lakini 🤔
...
R.I.P colonel joseph karegire Yari ayoboye igitero cokuja gufa ikibuga cindeg ca kavumu gusa ntivyamuhiriye kuko urugendo rwiwe rwagarukiye Aho ikibazo koyari ingabo yurwanda yaguye muri Congo arigukorayo iki kotuzi nomubari gutabaara Congo ingabo zurwanda zitarimwo
 
..muda wote Kabarebe alipokuwa Mkuu wa Majeshi ya DRC alishindwa nini kuwamaliza Fdlr na Interahamwe?
Fdlr iliasisiwa na Kabila snr. baada ya kupingana na Rwanda na kudai Majeshi ya Rwanda yaondoke Kongo.

Wakati Kabarebe yuko Kinshasa kulikuwa hakuna Fdlr kulikuwa Interahamwe tu wa kawaida lakini hawakuwa organised.
 
Fdlr iliasisiwa na Kabila snr. baada ya kupingana na Rwanda na kudai Majeshi ya Rwanda yaondoke Kongo.

Wakati Kabarebe yuko Kinshasa kulikuwa hakuna Fdlr kulikuwa Interahamwe tu wa kawaida lakini hawakuwa organised.

..what strategic mistakes Rwanda walifanya mpaka kusababisha Kabila Snr avunje urafiki nao?

..RDF imeuwa askari wa Tanzania nchi ambayo inasifika kwa kutunza amani.

..RDF imeuwa askari wa FADRC jeshi iliyoliasisi na lililopaswa kuwa rafiki.

..RDF imeuwa askari wa UPDF ambao waliwahifadhi na kuwafadhili mpaka wakatwaa madaraka ya Rwanda.

..RDF imeuwa askari wa Burundi taifa masikini majirani wa Rwanda.

..RDF imeuwa askari wa majeshi ya nchi zote majirani zake.

..Naanza kupata hisia kwamba huenda tatizo ni uongozi ulioko Rwanda na RDF.
 
..RDF imeuwa askari wa Tanzania nchi
Tuseme na ule ukweli mchungu Askari wetu hawakuwa walinda amani bali walikwenda kupigana na Waasi na kwenye Vita ni ua nikuue.
 
Tuseme na ule ukweli mchungu Askari wetu hawakuwa walinda amani bali walikwenda kupigana na Waasi na kwenye Vita ni ua nikuue.

..Rwanda pia ameuwa askari toka Burundi, Congo, na Uganda.

..Je, nchi zote hizo ni mashetani, Rwanda ndio malaika?

..Kuna shida katika uongozi wa serikali na jeshi la Rwanda.

..Wanyarwanda as a people ni watu wazuri. Shida ni uongozi wao.
 
Kuna shida katika uongozi wa serikali na jeshi la Rwanda.
Kuna kipindi Gari liliniharibikia Nyungwe haikuchukua hata nusu saa Askari wa RDF wakatia timu na kuniambia uko salama.

Na siku nyingine nikiwa katikati ya Nanga na Ziba gari lilisumbua kidogo usiku nikavamiwa na kupigwa mawe mpaka nilipopiga risasi mbili juu ndio wakakimbia.

Sasa kati ya hizi Nchi mbili ipi ina usalama zaidi?
 
Si urudi tu kwenu Rwanda kwani tatizo liko wapi?

Kwa nini usiende kwenu?
 
Si urudi tu kwenu Rwanda kwani tatizo liko wapi?

Kwa nini usiende kwenu?
Mimi niko Africa rudi wewe Mwarabu uliyekuja na Jahazi kwenye Bara letu Misri muliivamia Libya muliivamia haziwatoshi tu?!
 
Mimi niko Africa rudi wewe Mwarabu uliyekuja na Jahazi kwenye Bara letu Misri muliivamia Libya muliivamia haziwatoshi tu?!
Kumbe wew ni mrundi! Ndo maana ulkua humpendi chuma,jiwe,mzilankende Anko Magu…
 
Mfano wako ni irrelevant
 
Hayo yote ya Genocide- intarahanwe-FDRL ni chaka la kufichama kutimiza malengo makuu.
Rwanda anayo malengo tofauti na anachokisema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…