Mradi sio mbaya lakini tunaamini sana katika maendeleo ya vitu wakati kuna nyanja nyingi tu tumeziacha zikilegalega na uhakika huo mradi watakao pata zabuni ni makampuni ya Kichina na yatakuja na hadi mafundi mchundo wao wakati Wabongo wataishia kuwa vibarua katika mradi kama huo tuko na safari ndefu sana mpaka kufikia nchi ya ahadi sina hakika sana kama miradi kama hii itasaidia uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika au madawa mahospitalini.Kuna zahanati(jengo) maana haijakamilika kuitwa hivyo iko kijiji cha Changalawe(Myombo),Kilosa kwa zaidi ya miaka kumi ni jambo la kusikitisha lakini eneo hilo lina viongozi wote wa mtaa na mkuu wa wilaya hiyo huwa anakwenda kukagua mradi huo sasa huduma za msingi kama hizo hazipewi vipaumbele vinavyostahili.