Coming soon: New Kawe City (Uptown Kawe)

Coming soon: New Kawe City (Uptown Kawe)

Nashauri pia wayaangalie na majengo yaliyopo yanakarabatiwa ili yadumu. Wataalam watumike majengo yasijeanguka tena
Nasikia maghorofa ya Chang'ombe (pale kwenye mafundi wa fenicha) yanakarabatiwa soon. Huenda wapangaji hawajaambiwa lakini tetesi zinadai pataboreshwa na hata hao mafundi wa fenicha ambao wameingia hadi milangoni watahamishwa (panaweza kuchimbika kiasi chake) lakini baadae huenda wakajengwa Furniture Mall eneo hilo hilo.

The future is promising, endapo siasa hazitaharibu
 
Lakini mkuu ni usomi gani huu haswa?

Maendeleo ya nchi ni miradi kama hii kweli, ambayo mingi inakuja kigiza-giza, unaweza shangaa rais wa China hakuja bure (hata Kova alisema wasiandamane mazuri yaja ingawa alisema hajui ni yepi lol ? Vipi kuwa na plans za miradi ya maana kwanza, huduma za jamii, hospitali kubwa, umeme usio wa matone ( plz isijekuwa fweza aliyovuta Rostam Dowans ndo anawekeza huku). Je wale wa mfaranyaki, mchambawima, mkosamavi n.k ambao bado wanapiga teke km kadhaa kupata huduma za afya, maji n.k au msimu wa mvua wanapigana vikumbo na boko wao utawaeleza nini?

Je, zile ndoto na ahadi za meli kubwa ktk maziwa yetu, na vivuko vya uhakika vipi?

I swear to god, hii lazima itakuwa kama kigamboni, Bush hakucheza kiduku bure wabongo wakadhani anafurahia amani na ulofa wetu bali alijua dili ishakamilika na sasa atapeta tuuu..!

At least, mradi mmoja mkubwa kila kanda, then usafiri, viwanja (sio kulazimisha kusipostahili) ect then waendelee na miardi yao otherwise ipo siku haya madudu yataanguka hata kama ni kwa kuwakodisha akina Rodman na yule rafiki yake dogo rais wa N.K ambaye kila akilamba kilaji anaamrisha wanajeshi wale kwata kutishia nyau Jaluo, bila kujua anaweza pigwa kisago cha uhakika akiwa amelala !!

Mi nataka tuanze kuongea kisomi mkuu wangu, hujanikwaza. Ni challenge ambayo tunayo kwa sasa kama taifa. Sasa, tukomae tujue status za miradi hii na kama fedha kwa ajili ya miradi hii zipo. Tunaweza kuanza kutembea vifua mbele (hata kama hatuna stake katika projects zenyewe) endapo hii miradi itafanikishwa bila kuvurugwa.

Ikitokea huu ukafanikiwa, wa Kigamboni ukafanikiwa na mingine zaidi, basi kuna afueni tutaiona angalau ukilinganisha na majirani zetu
 
Sasa umesema mwenyewe New Kawe City na picha umeweka kwa upembuzi wako yakinifu..Mwisho unauliza tena kwa anayejua progress hiyo....
A%20S%20angel.gif
Pa warum
 
Nowadays Tanzania is only Daslam....everything is expected in Dsm....!! Ardhi ipo kibao mikoani bt only and only in Dsm,mengine yanajengwa mengine yanaanguka!!
 
nataka kujua chanzo cha fedha juu ya mradi huu kama ni kutoka serikalini basi sahau kama kumkuta changudoa bikra
 
Adamjee alipewa eneo la kiwanda tu, eneo jingine lipo chin ya kiwanda mfu cha TP ambacho ni mali ya Serikali. Hadi leo waliokuwa wafanyakazi wa TP wapo kwenye nyumba za TP hawajalipwa mafao yao. Kimsingi ni kama wametelekezwa, so nadhan ujio wa picha hizi utaibua hisia mbalimbali kwa washahafishwa wale.

Haya ngoja tusubiri taarifa zaidi...
 
Mkuu n00b, tukumbushe na mapicha ya mchikichini eti mchikichini project....
Walisema phase1 itakamilika mwaka huu, bado nasubiri kila siku napita hapo mchikichini nahifadhi kicheko/kilio changu tu!

Halafu Mkuu keko mi ndo maeneo yangu ya kujidai, hzo hadithi za maghorofa ya NHC hapa nadhani zimeshakamilishwa kwa kupaka rangi na kuzibua mitalo. Labda hlo jingine kama litakuja na sura ya New Keko Project My Foot.....

Umezungumzia Keko Furniture Mall, hzo Mall watakaa hawa hawa wakina Kushaba na Makelubi au kuna wachina wanakuja?
 
Mwaka gani huo? Katika nchi hii ya Tz? Au ni baada ya Yesu kuja kuuhukumu ulimwengu?
 
Shukrani kwa serikali ya awamu ya nne. Stay tuned! Mambo mazuri yanakuja na yataendelea kuja chini ya serikali ya CCM.

Kama hutaki maendeleo wewe utakuwa ni mchawi na ukatafute nchi ya kuishi.

hebu badilisha hata jina lako basi
nani alikwambia maendeleo ya maana ni ya vitu kama hivyo ? wazungu leo kwao hawakutaki wewe unaona hayo ndo maendeleo?
 
Mkuu,

Si ndoto. Na nikufahamishe ni kuwa tayari eneo la Kawe pale Tanganyika Peckers pamesharejeshwa ardhi kwa asilimia nadhani zaidi ya 50.

FYI, kuna project nyingine inakuja. Tanzanite Mall na itakuwa inaonekana kama inavyoonekana hapa chini (nimefuatilia Brela, naona kuna kampuni imesajili 2011 inaitwa "Tanzanite Mall Ltd" nahisi ndio wenye hii project):

attachment.php

kila jambo linawezekana ktk hii dunia,ni swala la maamuzi tu,mbona wanazijenga sana wenzetu tena ndani ya mwezi tu unakuta kitu kimesimama na kinaonekana,yawezekana ni swala la muda tu
 
Sasa umesema mwenyewe New Kawe City na picha umeweka kwa upembuzi wako yakinifu..Mwisho unauliza tena kwa anayejua progress hiyo....
A%20S%20angel.gif
Pa warum[/QUOTE
Huyu ni CEO wa NHC aliyeweka huu Mchoro. Maana aliingia na Gia ya kudanganyaya watu kuwa angejenga huo mradi Mwaka jana. Sasa baada kuchemsha kwenye jingo lililoporomoka ameanza kudanganya watu na Mchoro wake huo.
 
Haya mambo yanawezekana, tatizo ni ufisadi, si unaona mradi wa Kigamboni ni kama umekufa?
 
Hii ingekua nzuri sana...wasi wasi wangu ni kwamba kila eneo tutajenga sasa hata maeneo ya kukusanyikia watu kama pale au kwa ajili ya kupata ile green yanaisha...
 
ule mradi wa police oysterbay nao umeshaanza?
au ndio habari za kupewa picha kisha hutoweka
kama wana nia ya kweli ya kujenga hayo majengo nawapongeza
vijana watapata ajira
 
Nchi yetu imejaa wezi sana, naona sasa umezuka ufisadi wa aina mpya wa kutuchorea picha/city plans na kupiga hela za walipa kodi. Ukiuliza ni TZS ngap zimetumika katika kudevelop hiyo plan unaweza ukazimia. Kama kweli serikali imedhamiria kuendeleza nchi, kwanini isimalize plan ambayo tayari ipo???? Au kigamboni project imeshaisha???? Pia hiyo ni mbinu tu ya kutuibia lile eneo maana bila mapichapicha ya hivi pale hapaingiliki.

Kama nguvu ya kuendeleza eneo hilo ipo, pls tumalizieni kwanza Kigamboni project kisha tuamie Kawe. Hizi ni namna ya kutuibia hela kwa kujifanya wamelipa mabilioni kwa hao wanaodevelop hizo plan. Wiiiiizi mtupu. Hii serikali ilishajitoaga kwenye uwekezaji, kiherehere tena cha nn kwenye kugharamia maplan ya mabilion haya??? Wapelekeeni madawa na maendeleo bibi zangu vijijini.

I like this comment
 
Thread za kuwatafutia watu ban ndio hizi, ngoja tu niendelee na harambee ya mtaani kwangu kuchangisha pesa za vifusi maana mitaani hakupitiki sasa hivi.
 
hii miradi kwa tanzania ya sasa haiwezekani maana wateja wenyewe hakuna, ba ndio hao wameacha kuja bongo licha ya miaka 20 ya kuvutia wawekezaji, sasa hao makarani wa barclays ndio watakao kuwa wapangaji na wanunuzi wa hizo bidhaa hapo
 
Back
Top Bottom