Compare & Contrast: Hotuba ya Jaji Warioba v/s Rais Kikwete!

hakuna mtu asiye penda muungano, tatizo ni je upande wa pili wana utaka huo muungano, Jaji kasema upande wa pili wapo pamoja kwenye jambo hilo, iwe wa cuf au wa ccm, kwa hali akawa amekuwa limited na options anazoweza kufanya , ukitilia maanani upande wa pili mpaka katiba yao wame badili, na yeye au sisi wadanganyika/wabara machogo hatuna uwezo wa kubadili katiba yao. na zaidi ya hapo muungano unatakiwa uwe to a certain degree fair say 95%, ikiwa hatuwezi kufikia 100%, na hii inatakiwa kuonekana katika mambo mengi mfano kuchangia katika gharama za muungano, kuteuliwa kwa watu katika nafasi za muungano , mfano mambo ya nje n.k., sasa wewe muungano huu unaona upo fair? wa watu 1.5 wa upande moja kuwa sawa na watu 43 wa upande mwingine kama sio wizi? au theory ya changu ni changu chako ni changu ipo sawa?
 

..zaidi, wajumbe wa Tume wanasema wao wameangalia pia UZITO WA HOJA zilizotolewa.

..pia kwasababu muungano unahusu wananchi wa nchi mbili, basi ni lazima ktk kuchambua takwimu tuangalie kila upande unauzungumziaje muungano.

cc Pasco
 
Last edited by a moderator:
JokaKuu,

Na ni uzito huo huo wa hoja ambao CCM hiyo hiyo uliutumia kwenda kinyume na matakwa ya wengi kufuatia kazi ya tume ya nyalali ambapo 80% ya wananchi walipendelea mfumo wa chama kimoja, huku 20% wakipendelea mfumo wa vyama vingi. CCM ikachukua maoni ya wachache kutokana na nguvu ya hoja.

Ama kweli viongozi wa CCM are long in power and short in memory.

Cc Nguruvi3, FJM Mag3


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
hivi ukicompare RASIMU YA KATIBA na HOTUBA? kuna uelewa gani twapata

maana jaji warioba yeye alipitisha rasimu ya katibu na mkuu wa nchi naye alihutubia
mkuu pasco sijakulelewa ulitaka kumaanisha nini hapa?

na hapa hivi Rais wetu alisomea Ph.D au alitunukiwa?

source: Rais wetu Kipenzi, Mhe. Dokta (msomi wa Ph.D), Jakaya Mrisho Kikwete, is he credible?!, is he the man of integrity?!
Hilo pendekezo lake la kuendelea na serikali mbili kuwa licha ya kushindwa kutatua kero za muungano kwa miaka 50!, tukiendelea na serikali mbili, sasa ndio tutazitatua hizo kero inaweza kuwa kweli au ni blah blah tuu?!.
 
Kusema kweli CCM wanashangaza; wakati Kikwete anatetea mfumo wa serikali mbili akitoa ahadi kuwa matatizo yaliyopo yatashughulikiwa, anasahau kwamba under his watch kulitokea tatizo kubwa zaidi la kuibuka kwa nchi ya Zanzibar ndani ya Muungano. Muungano tulioachiwa na waasisi wetu ni serikali mbili ndani ya nchi moja na pamoja na mapungufu yake umoja wetu kama taifa haukuyumba kwani ulilindwa na Katiba ya Jamhuri hadi pale yeye Kikwete aliporuhusu ichezewe na upande moja katika Muungano. Kama tunakiri kuwepo kwa matatizo kabla, je, kuibuka kwa serikali mbili na nchi mbili zenye Katiba zinazopingana, kulipunguza tatizo?

Kikwete alianza kuonesha dalili ya hila iliyogubikwa na woga pale alipoiagiza Tume kutoruhusu maoni yanayohoji huu Muungano wetu, matatizo yake na namna ya kuyaboresha. Pamoja na kuwaacha wananchi hoi wakijiuliza hiyo nguzu na huo ujasiri wa kuwafunga midomo wananchi wasiujadili Muungano wao Kikwete kautoa wapi! Lakini baya zaidi ni ukimya wake kuhusu kitendo cha Zanzibar kutokuheshimu Katiba na badala yake kutunga Katiba yake inayopingana na ile ya Jamhuri. Kwamba mpaka sasa si Kikwete wala mwanachama yeyote wa CCM ameweza kukemea kitendo hiki cha kihaini hadharani, ni dalili tosha kuwa CCM imechoka na imekosa uhalali wa kuendelea kutawala.

Tutatengenezaje Katiba mpya wakati hatuna ustaarabu wa kuziheshimu sheria tulizojiwekea sisi wenyewe na hasa sheria mama kama Katiba. Nilitegemea kitu cha kwanza Kikwete angefanya alipopewa fursa ya kuzindua BMLK, ni kuwaomba radhi wananchi kwa kitendo hicho cha Zanzibar kutoheshimu Katiba ya Jamhuri. Baada ya hapo angetoa amri, kama Raisi wa Jamhuri na Amiri Jeshi Mkuu, Katiba hiyo isitishwe mara moja, isitumike. Halafu angehakikisha waliohusika wanawajibishwa kwa kuchukuliwa hatua kali kama fundisho kwa wale wote wenye mawazo potofu kama hayo...ndiyo, huo ndio utawala, utawala unaoheshimu sheria, utawala uliopo Kikatiba.
 
 
Last edited by a moderator:
 
Last edited by a moderator:
Na wengine huku tulishanyimwa fursa kwa kuwa tulizaliwa baada ya muungano tena kipindi cha Mwinyi so hatuna hadhi ya kuiulizia Tanganyika...........Mzee wangu alifariki nikiwa na mwezi sikumjua zaidi ya picha so sina haki ya kutumia jina lake kwa kuwa sikumjua.
 
Kama ni utafiti warioba anatisha kwanza kaja na existing situation, Analysis, na mwisho katia recomendation and suggestion. Napata shida kuuelewa mtiririko aliotumia JK

Jakaya alitumia mtiririko wa Kisanii ambao ndio mfumo sahihi wa CCM! Tatizo unaliona halafu unafungia macho ndio mtindo wa CCM. JAkaya ukimfikiria huwezi pata picha halisi sana sana utaishia kutukana tu!! Unaapa kuilinda na kuitetea katiba halafu ndani ya himaya yako anatokea mhuni mmoja upande wa muungano anasigina katiba kwa makusudi nawe unakaa kimya pamoja na kuwa unakila njia ya kuzuia kwa muda! Halafu leo unakuja na semina elekezi ambayo nayo iko kisanii sanii ni HATARI sana!!
 
Kijana naona hivyo viroba unavyokunywa bora uachane navyo maana vinakupa hangover mpaka unajisahau na kuanza kuweka povu humu ndani, jaribu kumcompare baba yako kwanza na sio JK mwehu weee
 
Hotuba za kujitetea kwa watuhumiwa!?
Ndo tatizo la ukosefu wa akili hilo linalokusumbua kiac kutofikiri, mnaropoka tu waka hamjui hotuba ndo nini, dada FaizaFoxy kaeleza vyema majibu ya hilo swali nawashanga nyie vipofu wa akili, kheri uwe kipofu wa macho kuliko kuwa kipofu wa akili poleni sana nyie vijana wa Ukawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…