Confession: The hurting truth -- natamani kurudi kwenye ushirikina

Confession: The hurting truth -- natamani kurudi kwenye ushirikina

Ushirikina ni dhambi mbaya sana na ngumu suna kutoka unapokua umezama kwenye hilo dimbwi, Kwa mujibu wa uislamu ndio dhambi kubwa kuliko zote, Na Mungu kaahidi hatomsamehe mshirikina isipokua yule atakaeacha mwenyewe na kuomba toba kwake.

Jitahidi kukomaa mkuu achana na vishawishi.
 
😳😳😳😳😳 ukishaonja Nyama ya mtu ni ngumu sana KUCHEZA nayo mbali. Once a MCHAWI ALWAYS a MCHAWI. Rudi tu ukaendelee kuwadhuru binadamu wenzio ambao hawakukosea lolote. SAD!

Niliachana kabisa na mambo yote ya kishirikina miezi kadhaa iliyopita, na kuthibitisha hilo niliweka uzi rasmi hapa JF na kumrudia Mola wangu mazima.. Na kuna hili ambao sikuwahi kulisema hapa lakini wale ambao niliwaumiza na roho ikaniongoza tusawazishe nilifanya hivyo.. Na nikapata amani kubwa moyoni

Naamini nanyi ni mashuhuda wa hili kwakuwa nilipunguza mada za ushirikina kwa asilimia 80 ama 90 hivi.... Na kila nilichomiliki chenye viashiria na viasili vya ushirikina ama niligawa au niliviharibu na kuviteketeza kwa moto kwa mikono yangu mwenyewe! Nilihakikisha naishi maisha ya ukamilifu na usafi wa kiroho

LAKINI wapendwa shetani ana nguvu sana sana... Unapokuwa umevaa koti jeupe la mshika dini na asiyependa mambo ya ulozo lakini ndani u mchafu kupitiliza wala sheatani hawezi kukusumbua kabisa lakini once unapomkataa kwa roho na kweli ...VITA HUANZIA HAPO! atakujia na washirika wengine SABA kuhakikisha wanakurudisha kwenye himaya yao...!

Juzi kati nilikuwa maeneo ya mikwambe Kigamboni kibada mpaka saa tatu usiku hivi wakati naondoka nikagundua kuna watu walikuwa wameniungia body na nilienda nao mpaka Tuangoma halafu wakapotea kusikojulikana

Tangu hapo nimejiwa na msisimko wa ajabu kabisa ... Msisimko wa kutafuta zile nguvu za giza tena.. Najitambua kiimani na kiroho niko vizuri mno.. Lakini sasa naona viashiria vya kunirudisha kilingeni vinazidi kupata nguvu kila uchao!
Tafadhalini naomba msije mkanishangaa in case mkisikia nimerudi Msata Kilingeni penye shina langu.. Lakini pia ukiweza na ukipenda kwa utashi wako pls niombee.. Kuna shida nyingi huko vilingeni basi tuuu[emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
 
Ushirikina ni dhambi mbaya sana na ngumu suna kutoka unapokua umezama kwenye hilo dimbwi, Kwa mujibu wa uislamu ndio dhambi kubwa kuliko zote, Na Mungu kaahidi hatomsamehe mshirikina isipokua yule atakaeacha mwenyewe na kuomba toba kwake.

Jitahidi kukomaa mkuu achana na vishawishi.
[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Mshana jr. Tatizo mi nadhani sio wewe kuacha ulozi

Tatizo lipo hapa kabla hata hujaacha ulozi ulikuwa unajua neno la Mungu na ukuu wa kristo. Hapa kosa lako ni kwamba hukuwa na sababu y ndani ya moyo ya kuamua kuacha, shida ilianza baada ya wewe kutka kulinganisha nguvu. Yani hukutaka kuwa kama mtoto kwa Mungu umeenda kama unahama chama cha siasa.

Nadhani baada ya hapa utakuwa umepata wapi pankufaa,
Yani ni hatari muumini anamzidi elimu ya dini mtumishi wa Mungu.

Yani umezidi kulinganisha nguvu sasa umeanza kujua wapi pana nguvu.
 
Kwenye Mahakama ya mnyonge mahakim wameanza kujiuzuru
Sasa wanyonge watapata haki wapi? Na kwenye mahakama za kawaida huwa hawatoboi
 
Back
Top Bottom