CONFIDENTIAL: Barua Pepe zaonesha Maafisa 62 wa Serikali ya Tanzania akiwemo IGP walihongwa Fedha na ACACIA (2008/2015)

CONFIDENTIAL: Barua Pepe zaonesha Maafisa 62 wa Serikali ya Tanzania akiwemo IGP walihongwa Fedha na ACACIA (2008/2015)

"NTF inadaiwa kuundwa na maafisa kutoka Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa, na Jeshi la Wananchi."

Hakuna sehemu iliyobaki salama kila mtu ni mwizi hakuna hbr ya uzalendo
Nimeshangaa sana. Ikiwa idara nyeti hizo ambazo wananchi tunaamini zina watumishi wenye weledi na uzalendo wa hali ya juu zimefikia hatua hiyo, maana yake tupo mahali pabaya sana.
 
Acacia, kampuni ya uchimbaji madini iliyokuwa na shughuli zake nchini Tanzania kabla ya kuingia kwenye mgogoro mkubwa na Serikali, inadaiwa kutumia takriban Shilingi bilioni tatu (Dola za Kimarekani milioni 1.2) kwa mwaka kulipa maafisa waandamizi wa Serikali kati ya 2008 na 2015,
Hebu kaa ukatafakari kuhusu hawa "Baadhi" ya maafisa Wandamizi.

Kipindi cha nyuma, aliyekuwa Raisi wa JMT, Hayati John Magufuli akiwa Ikulu Dr-Es-salaam akiongelea kuhusu makinikia, alisema
"...Siwezi nikasimama pale mbele nione wizi huu unafanyika nikakaa kimya"
akaongeza
"..Nitaulizwa siku ya mwisho wangu"

Baraza likakaa kimya kwa sekunde nyingi tuu

Hakuaishia hapo, bali alielezea kuhusu wabadhirifu kuwa

"hawakujali maisha ya Watanzania....walijali maisha yao"

Utakumbukwa kwa kweli.

View: https://m.youtube.com/watch?v=LSHd5P_azXE&pp=ygUhTWFndWZ1bGkgYWthdGFhIFJ1c2h3YSB5YSBBY2NhY2lh
 
Na ndio maana wakisikia katiba mpya wanatamani kuuwa watu wanaohitaji hiyo katiba, kumbe kuna mrija wa asali huko kwao kuanzia polisi, jeshi na usalama...

Maana nchi ingekuwa inaoongozwa na serikali imara uchunguzi ungeanza rasimi, kuna rushwa kwenye kampuni hizi za kigeni na hawa watu wanajiona wazalendo kumbe wazalendo uchwara
Na hiyo ndio Deep State Sasa.
 
"NTF inadaiwa kuundwa na maafisa kutoka Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa, na Jeshi la Wananchi."

Hakuna sehemu iliyobaki salama kila mtu ni mwizi hakuna hbr ya uzalendo
Kumbe na wao walikuwa kwenye mrija na ndio maana wanapata kigugumizi kuiadabisha ccm Kama wenzao wa Niger na kule Kwa Ali Bongo.

Haya madai kwamba maafisa wa vyombo vyetu walikuwa wanapokea mgao, ni makubwa sana kuyanyamazia. Chochonde- vyombo vyetu mliotajwa toleeni hizi kauli za madai hayo Kama ni kweli au sio kweli. Mkikaa kimya tutajua ni kweli…
 
Sijakiona cha maana hapo, aulizwe IGP wa wakati huo.

Kila kitu kipo wazi hapo, kuna hongo inawekwa wazi na vikao namna hiyo?

Majungu tu hayo.
 
Na uzuri huyo Deo Mwanyika bado yupo hai- sasa na atutajie - yeye Kama ceo wa acacia- hayo malipo, alikuwa anawapelekea nani huko kwenye vyombo- polisi, jesho na usalama?
Sasahivi ni mbunge,,usione licha ya kuchafilia na Magufuri Barrick hawakukimbilia mahakani kwani walijua madudu mengi magufuri alikuwa nayo..ikabidi watulie
 
Back
Top Bottom