CONFIDENTIAL: Barua Pepe zaonesha Maafisa 62 wa Serikali ya Tanzania akiwemo IGP walihongwa Fedha na ACACIA (2008/2015)

Ndio hivo majina yatakuja tu ishamwagika hio
Sitashangaa kuona majina ya vigogo hata waliopo sasa madarakani. Takukuru ndio tunataka kuona uwezo wao maana kwanza wameshatafuniwa kila kitu wao ni kumeza tu. Kama majina makubwa yakiwemo na hawajiuzulu wala kuchukuliwa hatua ni bora Rais mwenyewe Samia Suluhu Hassan ajiuzulu yeye ili aingie mwingine atakaye chukua hatua.
 
Hili nalo litapita kama mengine lakini pia huenda ni set agenda ila wafu tuache kukaza fikra kwenye issue ya Bandari watu wafanye yao.

Huyu Mwanyika alikuwa chaguo la JPM
 
Cha mtu uliwa na mtu,chuma pekee ndiyo uliwa na kutu!
 
Hii nchi ya ajabu sana nakumbuka Shujaa Magufuli alilamikia rushwa kwenye chaguzi za CCM hivyo TAKUKURU wakafanya uchunguzi kwa wagombea wanaotoa rushwa. Cha ajabu badala ya TAKUKURU kukamata wahusika eti wanaenda kumkabidhi ripoti mwenyekiti wa CCM!! Yaani makosa ya jinai yanasubiri maamuzi ya mwenyekiti wa chama?

Tokea pale nikajua vita dhidi ya ufisadi ni maigizo tu.
 
Ukiwaona walivyovaa suti na tai na kujiita niwazalendo utafikiria ni wa maana. Hizi aibu tutaziona nyingi sana sababu ya kupenda kwetu rushwa kulikopitiliza
 
Mbona kashfa ya ufisadi wa mtoto wa Samia akishirikiana na waziri wa mambo ya ndani kila ikiletwa hapa JF unaondolewa haraka sana na hii mnaiacha iendelee? Au asali imefika mpaka huku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…