CONFIRMED: January Makamba kugombea Bumbuli


Which makes it even more crucial, not less so, that we discuss these issues in detail and depth.

Kuna watu wanataka kutuambia kwa sababu mtu ana haki kikatiba na ni kijana tu basi anafaa, hata kama hana nia ya kuleta maendeleo kama alivyothibitisha kwa kauli zake majununi za "Watanzania ni nzi wala mavi".

Huyu huyu mjinga mjinga ndiye aliyetoa kauli zilizotaka kuleta diplomatic row na Wa-Nigeria katika jitihada zake za kitoto kujikomba kwa waarabu na JK alipoenda na muungwana Saudi Arabia.

Wakazi wa Bumbuli wakimchagua huyu watakuwa wameuziwa kanyaboya.
 

haya bwana..
 
Huu mjadala umefika mahali umepotosha na fm na gt kwa ushabiki na unazi wao na mapenzi kwa ndugu yao jm, imefika hatua wanapinga hata yale ambayo jm mwenyewe amefanya...hii ni hatari sana.

Lakini lazima tujue hapa kwamba, hakuna anayesema jm hafai kuwa mbunge au hana sifa za kuchaguliwa na wana bumbuli, anazo kila haki na ninasimamia kila taarifa niliyoifikisha hapa katika mzunguko wa bwana jm, kwa kweli hata mimi ningependa vijana tujitokeze kwa wingi sana ili kuleta mabadiliko, lakini kwa hili la jm lina mapungufu yafuatayo;

1. Anatumia ukaribu wake na raisi kujinadi kwamba ndio itakuwa sababu ya yeye kuwasaidia wananchi, na kuthubutu kusema ametumwa na raisi achukue jimbo, lakni kama raisi anamuhitaji sana anaweza hata kumteua, na hata alipoomba kuwasalimia wananchi pale soni kubwa ni hilo kwamba yey yupo sana karibu na raisi wa nchi....hata mh shelukindo aliwahi kujiita kibonyezo, kwamba naye yupo sana karibu na "jikoni"
2. January ameenda kujinadi na kujitambulisha akijua kanuni za chama haziruhusu na huu si muda muafaka, na akitambua kwamba yupo mbunge ambaye hajamaliza muda wake.

3. Kitendo cha jm kutumia nguvu ya pesa kutafuta kuungwa mkono ni kufanya wale wengine wasiokuwa na uwezo washindwe kujitokeza kwakuwa yeye ana nguvu ya pesa kutoka different sources, je watoto wa wakulima ambao wanauwezo wana nafasi gani?
Na kwanini jm atumie pesa wakati yeye kama tunavyosema ni smart na huko bumbuli ndio anakotokea na hata baba yake pia ndio kwao...

4.tunataka fair competition katika harakati hizi, jm atumie elimu yake na uzoefu wake kuwaomba wananchi wa bumbuli kura zao wakati itakapo wadia sio kuanza kutoa hongo za chinichini....

Ila hii ni kwa gt na fm, nipo tayari kuweka rehani maisha yangu nawahakikishia january makamba hawezi na hataweza kuchukua jimbo la bumbuli, nyinyi mnajua upinzani anaopata huko anakopita, sehemu anazozomewa...kwa kifupi haungwi mkono na kumbuka kwamba nyoka hazai jongoo....alwayz like father like son....

Ushauri wa bure kwa jm.....just pull out...tumia busara chambua na fikiria kuhusu safari yako ilivyokuwa na jaribu kuona inakupa matumaini gani.
 

- Ninafikiri uwezo mdogo sana ulio nao wa kuelewa ndio unakusumbua, mwanachi yoyote mwenye uwezo wa kusaidia wanachi anaotaka kuwaongoza, anayo haki ya kuwapatia anything hakuna sheria ya jamnuri inayokataza hilo, sasa utawaendeleza vipi wananchi unaotaka kuwasidia kama huwezi hata kutoa vyarahani wakajishonea nguo zao?

- Sasa kama Januari ana uwezo wa kugawia wananchi wa jimbo lake vyarahani asigawe kwa sababu eti ni mtoto wa Makamba amesoma na ni kijana mdogo? Unaelewa maana ya rushwa au unabahatisha tu?

- Wewe umewahi kuniona mimi nikija hapa JF kufuata mikumbo, huyu kijana anakuzidi sana mkuu na anao uwezo wa kuwa mbunge, tumeona magarasha mangapi kutoka huko Tanga yakiingia bungeni kulala tu usingizi, sasa vijana wanataka kuingia mnaanza wivu na majungu, hebu peleka huko muacheni kijana huyu awape mawazo mapya huko Tanga!


Es!
 
..January ana haki ya kugombea ubunge popote pale Tanzania kama ilivyo kwa mimi na wewe.

..I am assuming kwamba atagombea kupitia CCM.

..ninachopenda kujua ni kwamba huko CCM January yuko ktk kundi la CCM-mafisadi au CCM-wapiganaji? hakuna aliye-neutral ndani ya CCM.

..pia si vibaya kwa January kutoa misaada huko Bumbuli. lakini pia ni vizuri tukajua vyanzo vya fedha za misaada hiyo. je, ni fedha zake za mfukoni? je, ni fedha toka kwa wachangiaji ambao ni safi? je, ni fedha za mafisadi?
 
 
Wasifu wa Januari Makamba.

1. Mr. January Y. Makamba
, Chair of the Africa Working Group at the Institute for Conflict Analysis and Resolution (ICAR), Fairfax, Virginia.

2. Recipient of the Brenda Rubenstein Scholarship at ICAR, Mr. Makamba is also an International Organization Fellow of the UN Association and Intern at the Academy for Educational Development in Washington D.C.A MS degree in Conflict Analysis and Resolution from George Mason University will be awarded in May 2004,

3. following his BA degree in Peace and Conflict Studies from Saint John's University (Minnesota) in 2002.

4. Mr. Makamba
worked for AFRICARE as Assistant Camp Manager of the Mtabila II Refugee Camp, Kasulu, Tanzania from 1995 to 1997, where he oversaw the management of a camp of more than 60,000 Burundian refugees.

5. Later he worked summers as a Protection Assistant/Intern with the UNHCR Sub-Office in KasuluThe Carter Center (2002), and as a Researcher/Intern in the Ministry of Foreign Affairs of Tanzania, researching conflicts in the Great Lakes region of Africa as they relate to national policy (2003).

6. Mr. Makamba
(2001), as an Election Observer/Human Rights Intern in Atlanta and Sierra Leone with has built an extensive network of activists in politics and civil society in East and Central Africa.

7. Asisstant to the President of Tanzania, since 2005 to this date.
 
WEWE field marshal mbon aunatumia energy nyingi sana kutetea huu mvinyo wa zamani?!do you happen to have any special interest in this fella being an MP?!

wote tunafahamu jinsi gani UTAWALA wa kikwete ulivyofail.kuna post humu watu wanajaribu hata kuonesha connection ya washauri wa kikwete na failures zake.either hawasikilizi washauri au washauri wanamshauri PUMBA.

sasa kama JANUARI ni mshauri wa RAISI kwa miaka mi-5 sasa sidhani kama angefaa kuwepo kwenye kundi la mabadiliko ambayo wananchi wa Tanzania wanayahitaji.
huyu ni more of the same,nothing new hapa.huyo shelukindo naye ni walewale,wanajisemeaga bora afadhali kuliko potelea mbali,sasa sijui yupi ni yupi hapa.

tukirudi kwa JANUARI

1.ELIMU
kila mtu anafahamu kuwa kigezo cha elimu Tanzania ni moj akati ya silaha kubwa wanayoitumia mafisadi kulaghai wananchi wakati productivity ni F.sitampa sifa kwenye hili.elimu aliyonayo naiona kama basic,sio extra-ordinary.

2.UHUSIANO na KIKWETE.
hapa ndio anapokosea,anajihusisha na FAILURE ya uongozi,100 years later wananchi wa Tanzanaia watauuchukulia utawala wa kikwete kama muda ambao TZ ilijikwaa,so far tupo chini,we don't need losers like these to continue to keep us down.

3.FEDHA& MISAADA

huyu kijana hana fedha za kutoa misaada anayotoa,tunafahamu kuwa kuna mkono wa mtu behind those grants he is giving out now,as many others before him have proved.
wananchi wa BUMBULI wajiulize,is 5 years of a mediocre leader worth a few sewing machines?!
nyie mnaokimbilia kutoa mifano ya marekani sijui,ni wapi OBAMA alitoa msaada hata wa baiskeli kwa RAIA yoyote wa marekani?!!
cha zaidi aliweka kampeni ya kuchangiwa na same people waliomchagua.hebu tazameni hili,huyu mkimuachia afanye atakavyo mkishampa huo ubunge itakuwa payback time ya hivyo vyerehani same way watanzania wanalipia Pilau za kikwete hadi kesho!!

wanajua wananchi wa TZ hawana elimu ya uraia,na watafanya kila wawezavyo waipate elimu ya uraia!!

poleni watanzania wenzangu.
 
 
 
 
Hii thread yanikumbusha ile thread ya kijana mwingine iliyowahi kuanzishwa humu ndani - Lawrence Masha. Maswahiba wetu wanapoguswa swala haliwi tena nguvu za hoja bali hoja za nguvu lakini pamoja na yote mwishowe ukweli hufichuka. Pia kwa mbali nakumbuka mwaka 2005 - sitasahau yaliyotupata tuliokuwa na ujasiri wa kuhoji huyu bwana katufanyia nini hadi tumpe Uraisi. Bahati mbaya sana ni kuwa Watanzania siku zote tunakuwa na matumaini ya kuvuna tusichopanda. Kawaida yetu ya kukumbatia viongozi wa kufinyangwa inavyozidi kukomaa ndivyo na taifa linavyozidi kudidimia na bado hatujifunzi, inasikitisha.
 
- Nilitetea background ya Masha ambayo ninaifahamu sana pale ilipotaka kupotoshwa kwa makusudi, lakini sikutetea uwezo wake wa kazi kama waziri, na besides mengi yalikuwa ni majungu kuliko facts kama hii thread, lakini unaweza kuanzisha mjadala wa Masha huu ni Januari Makamba.

- Kuhusu Mtandao nilikuwa wa kwanza kule BCS kuwatahadharisha wananchi na hili kundi, lakini nikatukanwa sana kwamba wananchi wa Tanzania wanataka viongozi vijana, na matokeo yako very clear ya viongozi vijana.

- Sasa hapa sitetei mtu, ninatetea principle, kwamba mtoto wa Makamba au wa mwananchi yoyote wa Tanzania ana haki ya kugombea nafasi yoyote Tanzania, kama ana makosa kiuongozi yasemwe hapa tuyaone lakini sio kuleta chuki, wivu, na fitina na kujaribu kulazimisha majungu kwa nguvu kwamba wote hapa tuwachukie watoto wa viongozi hayo ni mawazo finyu sana na ni umasikini ambao binadam anauruhusu kumuingia mpaka kwenye ubongo, yaani unaanza kuwachukia watu wengine kwa sababu wamezaliwa na watu wenye uwezo kuliko wako,

- Au kwa sababu wana uwezo wa akili na wamefanikiwa makubwa sana kwenye maisha wakiwa na umri mdogo kuliko wako, basi unageuka kua na chuki wee halafu unajaribu kutumia kila njia kulazimisha na wengine wawe na sumu kama zako kwa visingizio vya ajabu ajabu ambavyo wala huwezi kuvitolea ushahidi, huo ni umasikini wa akili na ni hatari sana kwa taifa ndio maana hili taifa limekwama, watu wenye uwezo wa kuongoza siku zote hutengenezewa majungu na fitina kama haya kwenye hii thread!

- Eti ni wapi Januari aliwahi kuongoza taifa kwamba sasa unaweza kumuhukumu? Fitina fitina tu na roho za kimasikini mnajaribu hata bila aibu kuzihalalisha hapa, kama hamuwezi kugombea nafasi waachieni wanaoweza kina Januari, lakini sio kuja hapa na kutaka kutulazimisha wote hapa tuwe na chuki na watu wengine bila sababu, ni mawazo mufilisi na ya hatari sana na ni lazima kuwaogopa sana wale wote wenye haya mawazo ya chuki na watu!

Respect.

FMEs!
 

ndugu yangu fmes....hiki kiapo cha kumlinda na kumtetea jm kama kingetumika pia kwa viongozi wa nchi yetu basi tungekuwa mbali sana....lakini kinachonishangaza katika hoja zako ni kulazimisha kwamba kuna chuki na wivu na roho mbaya juu ya jm....you are very wrong.....tulichofanya hapa ni kutoa taarifa kwamba jm ameenda kujitangaza jimboni bumbuli na kwa taarifa yake alikuwa ameweka ahadi ya kufanya hivyo kabla kwani sio kwamba ndio ameanza kampeni...kwani hata pikipiki alishapeleka kule jimboni zaidi za mwezi sasa umepita....
hakuna asiyetaka vijana wajitokeze na hakuna aliyempinga jm so far, ila tunaangalia namna anavyofanya shughuli na kuangalia kama je ni katika mwenendo ambao unaleta matumaini kwa demokrasia ya nchi yetu....

nakushangaa unapopinga kwamba:
1. Jm hakwenda bumbuli kujitambulisha
2. January hajawahi kuchangia ujenzi wa shule
3.jm hakuchangia vijana
4. Jm hakutoka pesa kila alipopita....
5. Jm hakutoa pikipiki.....

lakini unatetea kwamba jm ni kijana mwenye uwezo....smart...hapo hapo unasema anasaidia jamii yake.....ndio maana nimesema humsaidii jm kwa hili kwa kukanusha kila alilofanya....unaweza ukawa au ukahisi kwamba wewe ni mjuaji sana lakini kumbe sivyo....unapinga hata kwamba jm anataka kugombea ubunge bumbuli.....
nimekuwekea hata namba za simu za watu wa kupigia kama unataka ushahidi..piga uulize kila sehemu anayopita jm anasema nini na anataka nini na jaribu pia kuchukua mawazo ya watu kuhusu mtizamo wao kuhusu jm.......

at my own humble conclusion, i think u have done more harm to jm than u think u helped....so long....

sijui na wewe unagombea wapi ndugu yangu....i wish u all the best....
 

January ni mzalendo kama kweli ameamua kwenda kugombea mimi binafsi nampongeza kwa nia yake, nampiga mwandishi huyu juu kwa maneno yake ya kukatisha tamaa vijana walio na mwiyo ya uthubutu ninatamani vijana wengi zaidi wasomi na walio na mtazamo mpya wajitokeze . katika kusoma kwangu naona alie andika habari hii anamtazamo hasi kwa Januari na siyo mwelewa wa haki za kiraia na historia ya za siasa nyumbani na dunia ajipange. Mtu hawezi kuhukumiwa kwa nia yake nzuri kwakuwa eti baba yake au mama yake hakufanikiwa kitu fulani kama anachuki na mzee makamba adeal na huyo huyo asihamishie deni la chuki kwa mwanae, usitende kitu ambacho hungependa kutendewa. EJR
 
january ni mzalendo anahaki zake binafsi za kirai, ninampongeza kwa uthubutu wake kama kweli anayo nia ya kugombea jimboni kwao. nivema kuunga mkono vijana wasomi na wenye mitazamo kushiriki katika maamuzi ya maendeleo ya nchi yetu kuliko kusambaza maneno ya kuvuja mwiyo ya vijana eti kwasababu baba zao na mama zao walishindwa kufanikiwa. Mwamndishi wa habari hii ni wazi kuwa anamtazamo hasi kwa January na siyo mwelewa wa historia za siasa nyumbani na duniani kama ana deni la chuki kwa mzee makamba asihamishie kwa kizazi chake. Vijana wengi jitokezeni tubadili mwelekeo wa taifa letu. EJR
 
Muacheni kijana wa watu apigane kuingia bungeni. He is smart and prepared to enter this politics game na nina uhakika jimbo lolote nchini litamtaka, tuache fikra za chuki na wivu kwa watoto wa viongozi au vibosile wa TZ.

Uwepo wao na elimu zao ni matokeo ya wazazi wao ambao waliukimbia umaskini na kufanikiwa ktk siasa na biashara. I don't care how. Isn't this young man the model of what every Tanzanian should be? In terms of wealth of knowledge!

The fact that wewe (an elite Tanzanian) unasoma JF sasa ni kielelezo tosha kuwa nawe watoto wako watakuwa na nafasi ya kuwa na potential kama ya au zaidi ya J Makamba, na watoto wasomi wengine wa vibosile wa TZ.
 
Hv kwani ukitaka kugomea ubunge au kiti chochote cha kisiasa ni lazima uanze kwa kutoa misaada kwa nguvu zote.... mantiki iko wapi... mi nafikiri hapa ndipo tunaokosea.... ikiwa ww ni jimbo lako..... iweje unapotaka kugombea ndio utoe misaada (mi naona ni takrima a.k.a rushwa ya kificho) kwani ulikuwepo wapi mwanzo na hukuona matatizo yao.... hii ni aina ya kasumba iliyojaa vichwani mwetu (viongozi na waongozwaji) sijasikia wenzetu(wazungu) japo sijatembea.. kuwa na staili hii... kuna njia flani za kujifikisha kwa wananchi sio lazima utoe mali... ukiwa una strong FACTS watu watakupa tu... kwa wneye akili ndefu ukianza kutanguliza hivyo wanakuwekea doubt kama utaweza kuleta mabadiliko......

SIASA za BONGO NI ZA KIPEKEEEE.... wote hawajielewe wapiga kura na wapigiwa kura... ndio mtajua kuwa nchii hii ilipaswa kuwa eneo la makaburi(no offence) haiwezekani mijitu iko kama mazezeta haielewi na haitaki kubadilika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…