MtazamoWangu
JF-Expert Member
- Apr 25, 2009
- 313
- 7
- Thread starter
- #41
Acha uwongo! mtu kwenda kwao ndio kujinadi?
Pili hebu jifunze KISWAHILI kabla ya kuja kutuandikia madudu yalojaa errors zisizoeleweka!
Hivi kwa mtu mwenye nafasi yake na aliyezaliwa kwenye familia ya Mwanasiasa na ambaye anafanyakazi ya Kiserikali kweli aende Nyumbani kwao bila kukutana na watu tena kwa nafasi yake itakuwa sawa?
Asante sana mkuu kwa ukosoaji ila kwa taarifa yako JM sio mzaliwa wa bumbuli..mama ni Mhaya na baba ndio mzaliwa wa kule, hao watu wake alioenda kuwaona unawajua wewe, lakini pia sehemu anapotokea mzee makamba (mahezangulu) ni mbali sana na soni, ipo korogwe...
Uwongo mwingine ulioegemea kwenye UDINI!
rudi tena kwa huyo anayekupa hizi taarifa kisha utuletee FACTS badala ya kuleta stori ya Kuunganisha.
Pili ukweli ni kuwa hakusubiri watu kuswali bali yeye mwenyewe aliswali na baada ya hapo waumini walimuomba kama ana lolote la kusema na akasema kuwa nafasi hiyo si yake bali ni ya Imam na baada ya Imam kuinsist na kwa mila na desturi za watu wa Pwani Mdogo kwa Mkubwa hakui na hubishi hivyo alisimama na kusalimia waumini mle ndani
Inaonekana kama unamtetea, mimi ndio nipo hapa, huyu bwana alitaka atake advantage ya kukutana na watu wengi ndio alisubiri swala ya ijumaa kwa taarifa yako hakuswali na swala ilipoisha walipoomba awasalimie waumini aliporuhisiwa alitaka kuingia na viatu diwani wa soni ndio alimzuia,ndipo alipopaa nafasi ya kuongea na wachache, kwakuwa wengi walikuwa wameshamsikia na waipangakutokumuunga mkono hata kabla hajafka.....
Na pia alisema wazi kuwa SALAM ZAKE ZISITAFSIRIWE KAMA KAMPENI yeye kaja kuswali kama waislamwengine na mindhali leo ilikuwa Ijumaa sasa tatizo liko wapi?
Una uhakika kama JM ni Muislamu au unamsemea??
Unazungumzia Piki Piki..hivi le mtu Kama ES au Mwanakijiji au Pasco akienda Kijijini kwao akatoa Computer au Baiskeli ndio atakuwa ana kampeni? kama kutoa kusaidia kwenu ni kampeni basi wengine tusingejenga zahanati na shule mbili tatu ili wananchi wapate matunda ya sie wengine kutafuta na kutumia nafasi tulizopata kuwanufaisha!
Pikipiki alizotoa amesema kabisa ni kw ajiri ya kampeni na wat aliowapa wamshindwa hata kuzitumia, tatizo JM hata watu anaotumia kwenye kampeni awaju vizuri, wengi hawamkubali naweza hata kukupa majina yao,na mtu anayemtegemea sana anafanya kampeni za kihuni hakubaliki.
Once again umerudi na WAISLAM! lakini pamoja na hayo kutoa au kuchangia ujenzi ni jambo la kawaida...na kwa Musilam ni sawa ni kutimiza moja kati ya NGUZO 5 za uislam na pili tofauti ha huyo aliyekutuma hapa kuleta huu UDAKU, JM katoa kuchangia elimu bosi wako yeye anatoa kwa Ajili ya KIMADA WAKE pale mtaa wa ALLY KHAN!!!
Umesema amekumbwa na vikwazo vingi lakini ungeturahisishia ukatupa orodha ya Vikwazo...kwa utaratibu ufuatao:
1. JM ameambia sio mkazi wa bumbuli
2. halijui hata jimbo lake
3. haongei hata lugha yao...
4. hajawahi kushiriki katika shughuli yoyote ya maendeleo ya jimbo hilo
5
6
7
8
9
10
Pili Mapokezi Mabovu yepi? Mbona Jezi na mipira zimechukuliwa? na si hivyo tuuuu infact jamaa wanalalamika kuwa JEZI za RANGI za YANGA zimekuwa nyingi kiasi cha kuwa wanataka Jezi rangi Mchanganyiko...sasa wewe hapa linalokuudhi nini?
Hivi unataka vijana waendelee ku piga NDIMU kuhu wako vifua wazi?
wewe unaongea ushabiki sana,ni nani alipokea jezi hizo,na kwa taarifa yako leo kuna mashindano ya kata yanaanza hapa Soni, nani kasema hawana vifaa??