Connect Dot: Nani anataka kumtisha Rais Samia na umaarufu wa Hayati Magufuli?

Malori mangapi yalitumika kujaza watu pale kwa Mkapa na barabarani mpaka Airport JNIA?? Mbona tunalishana ndula?
 
Safari hii kule Twitter pamechafuka , mkuu wa vitengo amewagusa wababe wa mlungula , let us see and wait
 
Hivi anakuwa kwenye teuzi mbalimbali kwa zaidi ya miaka 20,Na bado tu anatafuta teuzi?Inakuwa ni arosto ya madaraka ama?
 
Unapotaja kabila la mtu kwa mabaya unatengeneza immotional na spirit ya uhasama. Jamiiforum shughurikieni hawa before hakujaharibika
 
Kama mkeka umechanika sasa itakuwaje ?
 
Hakika laana ya ubinafsi haitatuacha
 
Moja ya mada fikirishi sana kwa wakati huu.

Hongera sana mkuu mirisho pm.

Nayatafakari uliyoyaandika hapa.

Ila, nitamshangaa sana Rais Suluhu akikubali kuyumbishwa.

Huu ni wakati muhimu kwake kuwa kiongozi. Lolote analolijua kuhusu uongozi, wakati ni huu kulitumia na kuonyesha uwezo wake wa kuwa kiongozi.
Asikubali kamwe kumtegemea yeyote, awe Mwinyi au Kikwete.
Awasikilize wakitaka awasikilize, lakini uongozi ni wake. Yeye ndiye atakayeamua bila kuhojiwa.

Miezi hii ya mwanzo, atapata majaribu sana, lakini namsihi asimame kidete; na watakoma.
 
inawezekana vipi kundi linaloungwa mkono na vyombo vya usalama kushinda mahala ambapo nguvu ya uungwaji mkono wa mtu husika haipo ndani ya chama?
Eeeenh, Heeee!

Hivi nimekuelewa swali lako?

"Kuungwa mkono ndani ya chama", ndio kitu gani hicho!

Huko ndani ya chama kuna nani kama siowalio na njaa ambao wapo tayari kutupiwa fupa kama mbwa?

Hicho chama bado kina mtu mwenye hadhi ya kusimamia lolote?

Ni sawa mkuu, sisi hapa JF tunajipigia tu 'story' mradi tuonekane tupo, hata uhalisia wa tunayoyasimulia haupo kabisa.

Aaaha, ni wewe mkuu 'denooJ:'?

Samahani, nilimwagika tu bila kuangalia nani kaandika hapo huo mstari niliounakili.

Hivi kweli unaamini hivyo ulivyoandika?
 
Angalia usivyokuwa na aibu.

Unapata wapi ushujaa wa kuandika upuuzi kama huo wapi. Polisi miaka mitano yote walikuwa hawafanyi siasa?
 
Kwa hiyo vyombo vya Usalama vipo vipo tu havina say yeyote na vinapokea kama dodoki maamuzi yeyote ya chama? Kama ni hivyo basi Taifa hili litakuwa ni kama genge la wahuni.
Na siyo hivyo tu.

Kama mvutano huu ni juu ya "Umakamu", si huyo atakuwa Makamu Rais, au atakuwa ndiye rais mwenyewe?

Au hata Uenyekiti watamnyang'anya mama?

Na hata wakimnyang'anya uwenyekiti, bado anaweza kuwavuruga na lichama lao hata wasijue wanakokwenda.

Sioni sababu yoyote ya kelele zote hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…