Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Kosa la kuruhusu mkataba kuvuja na wasiotakiwa kuuona limeshafanyika na gharama ya kujitetea zimekuwa kubwa kwa upande wa serikalini. Mijadala imekuwa ni mingi kutoka kwa watu wa kada mbalimbali juu ya masuala ya kisheria.
Nani alivujisha siri za serikali? Wahusika wanajuana na wameshaiona gharama ya walichokifanya. Serikali imepoteza ule usiri uliokuwepo kuanzia awamu ya Hayati Benjamin Mkapa kurudi awamu ya pili na ya kwanza. Kuwepo kwa watu wanaotumia anwani ya Kigogo 2014 na Kigogo 20014 kumekuwa ni mwiba kwa mipango ya kiserikalini.
Kuzungukana ni kwingi sana kuanzia kwa watendaji wa ikulu yenyewe mpaka huko kwenye mawizara mbalimbali. Makundi ni mengi na yanatafuna ufanisi mzima wa baadhi ya maazimio na miradi ya kiserikali. Aliyeuvujisha huu mkataba wa bandari anaweza kuwa ni mmoja wa wale wenye nia ya kutafuta urais wa mwaka 2025 au 2030 hivyo akadhani kuwa kuichimba serikali ya SSH ni njia ya kujirahisishia kazi ya kwenda ikulu.
Niliuelewa ukimya wa Rais na wasaidizi wake hata pale mbinu za wapinzani wake zilipomtaka afungue mdomo aongelee suala la bandari. Alifahamu mtego wa wapinzani wake na akaamua kuendelea na masuala mengine ya kiserikali kama vile hahusiki na suala zima la bandari. Alijua ni kwa kiasi gani wapigaji wa TPA walikuwa wakiumia mioyo yao kutaka kujua msimamo wa serikali ni upi.
Bahati mbaya sana Mababa Askofu wenye kuheshimika kwenye jamii zetu wakarekodiwa zile video fupi na zikarushwa mitandaoni ilimradi tu kuigawa jamii ya kitanzania. Huko kanisani mapadre wakaanza kuhubiri kuhusu bandari bila ya kuwa na uelewa mpana wa hicho wanachokiongelea mbele ya waumini wao.
Adui pia akawatumia wazee wenye ushawishi na umaarufu ndani ya CCM lengo likiwa kauli yao iwe ndio rejea ya wanajamii wanaofuatilia suala zima. Kwamba Profesa Shivji au Profesa Lipumba akitoa maoni yake kuhusu bandari sisi wengine tulifanya makosa kuwakosoa na kuhoji juu ya maadili mazima ya wao kulikosoa lengo zima la uwekezaji!
Utanganyika na uzanzibari vikaanza kuongelewa kama vile ni hatua njema kabisa kwa mustakabali wa Tanzania. Watu wakasahau kuwa yapo maisha baada ya kuwepo kwa Tanganyika kama nchi mpya, wakasahau kuwa ule umaskini wetu upo pale pale hata baada ya kujitenga na kuwa nchi mbili kamili.
Yote haya yamesababishwa na wale walioshindwa kutunza siri za serikali na wakaamua kuisaliti ofisi inayowalipa mishahara!. Wapo wengi hata hawakutaka kujiuliza hiyo bandari imekuwa ni yetu tangu siku bendera inapandishwa pale uwanja wa Taifa iweje leo eti ndio iuzwe!
Mbegu ya ubaguzi iliyotaka kupandikizwa miongoni mwa watanzania imeshindwa rasmi kule Mbeya baada ya hukumu iliyotolewa na majaji juu ya suala zima la uwekezaji bandarini. Mbegu ya wao na sisi imepoteza kabisa mashiko baada ya DP World kuruhusiwa kisheria kufanya uwekezaji katika bandari yetu.
Ombi maalum kwa wanasheria wanaoandaa mikataba ya kibiashara muda huu katika sehemu fulani ya dunia, ni kutorudia kosa kama lililoufanya mchakato mzima wa uwekezaji kuchukua muda na kuzusha maneno mengi kutoka kwa wanasheria uchwara wa mitandaoni.
Nadhani ni wazoefu kiasi cha kufahamu maana ya kutunza siri haswa katika suala nyeti na lenye maadui wengi kama hili la uwekezaji pale TPA. Wamejifungia wakiumiza vichwa vyao ili waje na vifungu vyenye maslahi kwa wafanyabiashara wazalendo.
Iwapo biashara nzima ya uwekezaji itakwenda kuharibika mbele ya safari na Tanzania ikalazimika kulipa mabilioni ya pesa basi wao wakiwa ni wanasheria wa taifa hawataweza kukwepa lawama zozote zile zitakazoibuka, ni muda wa kuwa makini kadri wawezavyo wakati wa uandishi wa vifungu vyote vitakavyokuwemo katika hiyo mikataba miwili muhimu iliyobakia.
Uwekezaji huu ukikaa sawa na kuzaa faida kwa upande wa TRA watakumbukwa na majina yao yataingizwa kwenye zile kurasa maalum za mashujaa wa Taifa, wakishindwa kuweka uzalendo mbele na weledi wao ukaliangusha taifa maana yake majina yao yatakwenda kupoteza kabisa heshima ambayo wameipata mpaka muda huu.