Consession na lease agreements zinapoandaliwa muda huu, watendaji serikalini wakumbuke maana ya usiri kazini (confidentiality)

Ni Watumishi wasio na Maadili ya kazi ndio huvujisha,Hawa wakibainika wafinywe mazima maana sheria ya usalama wa Taifa na kutunza Siri za miaka 20 hazitoshi wanaweza tumia ujanja ujanja kukwepa kifungo.
 
Ni Watumishi wasio na Maadili ya kazi ndio huvujisha,Hawa wakibainika wafinywe mazima maana sheria ya usalama wa Taifa na kutunza Siri za miaka 20 hazitoshi wanaweza tumia ujanja ujanja kukwepa kifungo.
Siasa za kuutafuta urais zimeanza mapema. Hata yale maneno aliyoyasema RC Chalamila kule Kagera kuhusu mtendaji mmoja wa serikali kwenda huko nje kutafuta pesa kwa ajili ya kampeni za 2025 yana ukweli. Hakusema kufurahisha baraza tu.
 
Hawa wataalamu ndio akina professor Ossoro wamefika kwenye mahakama zinazofuata sheria na sio maagizo ya serikali, wameishia kuongea mambo ya aibu. Lakini wakati walipokuwa wanatengeneza hizo taratibu walikuwa wanalazimisha tuwaone ni watu makini sana.

Inshort hakuna lolote jipya unatuambia maana tunajua uwezo duni walionao hao wanajifanya wataalamu wetu. Na ushahidi wa uwezo wao duni tunao kwenye mikataba mingi.
 
Siasa za kuutafuta urais zimeanza mapema. Hata yale maneno aliyoyasema RC Chalamila kule Kagera kuhusu mtendaji mmoja wa serikali kwenda huko nje kutafuta pesa kwa ajili ya kampeni za 2025 yana ukweli. Hakusema kufurahisha baraza tu.
Hiyo ndio namna urais unatafutwa siku hizi, kisha wakifika hata wakati wa uchaguzi wanaishia kupora uchaguzi. Halafu watu hao wanaotafuta madaraka kwa mbinu chafu, wakiingia madarakani ndio mnalazimisha tuwaone ni watu makini. Ila nyie chawa mna vituko vya hatari.
 
Una haki ya kuwa na maoni hayo kwa uzoefu halisi wa taifa hili. Nakuhakikishia tu kuwa suala la DP World limeshughulikiwa na mikono salama sana mpaka dakika hii.
 
Kuniita chawa ni kunitukana, kwa sababu hunijui. Mpaka unakuwa na mawazo ya kuporwa uchaguzi maana yake umetengeneza mazingira ya kuibiwa, hilo ni tatizo lako binafsi sio la kitaifa.

Kumbuka hao hao wanaodaiwa kuiba kura ndio wanaotandaza umeme nchi nzima umefika. Ndio wanaojenga SGR na inakaribia kumalizika. Wanafanya mengi sana na kupata uhalali wa kuongoza nchi hata kama kuna baadhi ya matukio ya wizi wa kura.

Huo wizi hauwezi kuwa ni doa kwenye uongozi wao ambao upo karibu na shida za watu na unaziishi kila siku.
 
Yule Johari na Elimu yake ya kuungaunga ndiyo mtaalamu wa kumuamini!
Aisee,hiyo rushwa aliyotoa DPW imewalevya sana!
Kama tungezingatia weledi basi tulitarajia watu kama Professor Shivji,Jaji Warioba,Tundu Lissu et al wakihusishwa ku-negotiate hiyo mikataba na siyo hao Wahuni ambao wanaifanya nchi kuipigia magoti City-state ya Dubai!
 
Mikataba na concession za michongo! Hakuna ushindani ni mwendo wa kupeana RUSHWA na 10% basi.
Mimi ni CCM lakini wenzetu wanaokula hadi kuvembewa hawaoni hata kinachotokea Africa Magharibi!
Wananchi wakishachoka Serikali za kifisadi basi hujichukulia njia wanayojua wao!
Suala la Bandari jinsi lilivyopelekwa na Rais Samia Lina Mazingira ya RUSHWA kubwa sana!
Hakuna mtu mwenye akili anayeweza kumuunga Samia mkono kwenye hili!
Machawa wake waendelee kumdanganya!
 

Hata wakificha huwa wanaumbuka tu kwenye mahakama za kimataifa na kuliingizia gharama taifa letu,bora wa weke wazi ili vipengele vibovu vijadiliwe wapate kurekebisha.
 
Upumbavu NAO Ni kipaji.
 
Kama hao unaowaamini wewe wanawakilishwa na mawazo ya Wakili Mwabukusi basi mmeshindwa vibaya na hili la kushindwa mliambiwa siku nyingi kabla ya hukumu.

Mnaleta ujuaji wa kutaka kuandama nchi nzima, mtaumia sana.
 
Hata wakificha huwa wanaumbuka tu kwenye mahakama za kimataifa na kuliingizia gharama taifa letu,bora wa weke wazi ili vipengele vibovu vijadiliwe wapate kurekebisha.
Kule mahakamani ilikuwa ni sehemu sahihi ya kujenga uhalali wa hoja za wanaopinga uwekezaji lakini kushindwa kwao mbele ya sheria ni kielelezo cha ukosefu wa hoja za maana zenye haki ya kujadiliwa.
 
Johari aliwashinda wanasheria wa Malawi kwenye suala zima la haki ya kumiliki Ziwa Nyasa, amefanya mengi ya maana.

Johari amekuwa kwenye timu za serikali za majadiliano mengi ya kisheria na wenye elimu na uelewa wanaujua mchango wake.

Usitishwe na hayo majina ya kina Shivji na Lissu hao ni maarufu tu lakini yapo mengi yenye kuwazidi vimo.
 
Hili gazeti ulioleta hapa halina maana yoyote, maana hata mkataba wa gas kuna waliokuja na porojo kama zako. Leo hii tunaambiwa gas sio yetu!
Ati anadai wanaochakata HGA wakikosea walaumiwe. Kweli? Yaani waingize nchi kwenye crisis afu itoshe mulaumiwa badala ya kunyongwa? Anyway, sikujua kama kuna timu inaendelea na HGA huko hadi baada ya kuhabarishwa na huyu mdau stevin Joel. Kumbe ndo maana humu siku hizi akina The Boss Na faiza foxy wameadimika hapa JF kumbe wanacharaza HGA kati ya Tz na Dubai? Kweli nchi inachezewa.
 
Changamoto ni kwamba watumishi wengi wa serikali hawana ownership ya fikra zao, hii Ina maana wanaazima akili za wanasiasa katika kuamua kitaalamu.
Bahati mbaya siasa zaweza kumpa madaraka mtu ambaye ana uwezo mdogo sana wa fikra na hivyo wataalamu kutumia uwezo huohuo.
Ni watumishi wachache sana, hata wanasiasa kwenye serikali, hayati Magufuli akiwa mfano wa kuigwa, wenye uthubutu wa kutumia akili zao kwa uwazi katika kuamua. Wengi wakiwa na madaraka makubwa hutumia vyombo vya dola ambavyo navyo huongozwa na watu wa aina hiyo hiyo ya kuazima fikra katika kutekeleza majukumu yake ya siku kwa siku.
Wageni wengi wanajua utamaduni huu na hivyo kutumia kufanya lobbying na kufanikisha wizi wao dhidi ya taifa letu kiulaini.
Kinachotakiwa ni kila raia na watumishi wa uma kutumia akili zao kwa mantiki katika nafasi zao kwa maslahi mapana ya taifa ambapo maslahi yao binafsi yapo ndani.
 
Uelewa wetu mdogo unatufanya tuamini kwamba nchi inachezewa ukweli ni kwamba nchi inakwenda kuwafagia wapigaji wa pale TPA ili pesa halali na nyingi iweze kuingia kwenye uchumi mkuu.

Ili mzigo mwingi unaotoka DRC na Rwanda uweze kusafiri kwenda nje ya nchi kwa haraka zaidi na tusipoteze soko la ushoroba huu.

Mungu aliyeiumba Tanzania na kuiweka hapa ilipo kijiografia alishamaliza wajibu wake siku nyingi inabakia wajibu wetu wa kiserikali wa kuitumia faida hiyo ili igeuke kuwa pesa nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…