Control Number imepunguza Wizi

Bado wizi upo Mkuu.....watu wanacheza sana na hizo control number.
 
Magufuli ni mwamba, wakuu, mimi nilishawaambia pesa haipotei yaani.
 
Imepunguza idadi ya wezi. Wezi wa hela ndogo ndogo wamedhibitiwa
 
Tukisema Magu ni Rais bora ukilinganisha na wenzie waliotangulia, watu hawaelewi.

Nakumbuka siku ana kikao na wafanyabiashara wa madini kuna jamaa aliongea kwa hisia sana, sasa yule jamaa ndio kielelezo cha watz wachache ambao hali iliyokuwepo field ilikiwa inawakwaza mno ila ndio hivyo hawajui wafanye kitu gani, Magu ni mmoja wao tokea akiwa waziri huko nyuma sasa amekuwa Rais.

Nimeumwa sikio, kuna mtu alitakiwa kwenda kulipa pesa kiasi fulani akafyeka kadhaa, alipoitwa kuulizwa chenji akawa amebaki na laki nne, kuulizwa nyingine ziko wapi akafa kwa pressure πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ ,wakazika.
 
Hii taaaaamu sana, Lita 10 za maziwa halafu kilo kumi ugali wa chikandanga!!
Upo hapo?
 
Kukusanya fedha ni nusu ya mlinganyo.

Nusu nyingine ni matumizi ya hizo fedha.

Kama ukusanyaji wa fedha unadhibitiwa, halafu mtu mmoja tu ananunua midege anavyotaka, bila bajeti, tenda ya wazi, wala ukaguzi wa vitabu, bado tuna tatizo kubwa sana.
Umewahi kutengeneza budget wewe? Unazijua tender wewe? Kwa kifupi: Katika budget kuna emergency cases or miscellaneous cases. Katika Tender kuna kununua direct kutoka kwa manufacturer. No dealers no competition!
 
Ufafanuzi wa nn hakuna wizi wa maduhuli ya Serikali. Vijana wafunga tai sijui CPA holder namba wanaisoma
Tatizo lako umekariri maisha bwashee, CPA holder anayejitambua vizuri hawezi kufa njaa kwa kutegemea ajira unless awe na matatizo ya mtindio wa ubongo. Kuna advantage pia za kuweka mfumo wa control number kwa qualified accountants kuliko hao vishoka unaowasema waliokuwa wanaingilia taaluma uhasibu ( CPA). Hakunaga system ambayo huwa inaua taaluma ya mtu. Inaonekana wewe ndiye ulikuwa kishoka.....ukweli mchungu lakini ndipo tunapoelekea huko mbele katika ulimwengu wa IT 100%.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…