#COVID19 Corona iko maeneo gani Tanzania?

#COVID19 Corona iko maeneo gani Tanzania?

Lorenzo Samike

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2021
Posts
1,187
Reaction score
1,914
Hey,

Nawasalimu kwa Jina la Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania.

Hivi majuzi juzi tumesikia taarifa lukuki kuhusu corona. Wengine nimesikia wanasema kwa sasa hili ni wimbi la tatu — Wengine wanaita sijui DELTA kitu gani gani??

Majina yamekuwa mengi kidogo. Kuna DELTA na kuna wimbi.

Kiuhalisia huku Buza nilipo, hatujui hata maana ya corona. Achana na hayo maDELTA na manini nini mengine.

Tunajiachia vibaya sana. Hakuna cha barakoa wala sanitaiza. Na tuko fiti ajabu.

Haya makorona ya DELTA huwa nayasikia kwenye magazeti na majarida tu. Mtaani hakuna cha DELTA wala bibi yake na DELTA.

Sasa hawa wajuvi wa corona wanasemaje kuhusu hili? Hiyo DELTA iko wapi hasa hapa nchini?

Maana inawezekana mimi niko Buza huku, kumbe hiyo DELTA imejificha njombe!

Wananchi tunavurugwa. Mtaani hatuoni cha DELTA wala nini, lakini usiku kucha Televisheni zote zinazungumzia DELTA.

Which is which? Tuamini TV ama tuamini uhalisia tunaouona mtaani?

Mnatuchanganya mjue?
 
John_Heche._on_Instagram:_“Napongeza_hatua_hii_ya_haraka_iliyochukuliwa_kuongeza_mitungu_ya_ge...jpg
 
Hapo ulipo corona IPO, chukua tahadhari
 
unauliza corona iko wapi kweli? are on your senses?
Ni sawa mkuu, Hata mimi nashangaa. Huku Mtaani maisha yapo normal ila ukisikiliza kauli za viongozi unaweza dhani hali ni ya kutisha. Nafikiri viongozi wanafanya hivyo kutufanya tuchukue tahadhari,ila kiuhalisia si kiiiivo!!!.Tuendelee kuva barakoa na kusanitaizi.
 
Back
Top Bottom