Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Mkuu, sijataka kuanzisha mjadala katika hili ndiyo maana sijazungumza kwa kina. Kama hujasikia, dunia haiko kwenye giza bado. Unaweza kujitafutia taarifa mwenyewe.
Weka chanzo cha ulipoyatiwa ukiyoandika au u muongo na mzushi tu hauna kingine.

Uongo uuzuwe wewe halafu mimi nikakutafutie ushahidi?

Fikra za kijinga hizo.
 
Allah/ Mwenyezi Mungu alivyoleta manabii na mitume ni kwa ajili ya Kuonya na Kubashiri sio kuleta maombi watu wasife, na lau kifo kingekuwa na auheni basi wangelipewa hao mitume na manabii umri mrefu hadi leo wangekuwepo ili waendelee kutubashiria na kutuonya.

Hivyo kuwepo kwa viongozi au waumini si ishara ya kuzuia yale atakayo Allah yatendeke. Sisi ni kuendelea kumuomba na kumtumainia yeye (kwa maana dua na ibada zinapunguza au kuondosha mabalaa na mitihani) na kuchukua asbabu (ushauri kutoka kwa mamlaka na wataalamu wa afya) tu ndio wajibu wetu.
 
Weka chanzo cha ulipoyatiwa ukiyoandika au u muongo na mzushi tu hauna kingine.

Uongo uuzuwe wewe halafu mimi nikakutafutie ushahidi?

Fikra za kijinga hizo.
Sawa, mimi nina fikra za kijinga. Hivyo siwezi kusema lolote mbele yako ewe mwenye fikra za kisomi na werevu.
 
Naamini Mungu yupo lakini hainizuii kuhoji

Mimi sio mtumwa wa dini kama wewe
That is the difference between me and you



Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa mie mtumwa ila wewe utakuwa mjinga,kwa sababu huyo Mungu haonekani wala hakuna njia ya kuwasiliana nae kwa kuweza kumuhoji. Sasa huko kuhoji unamuhoji nani? Au mwenzetu unaonanae huyo Mungu ndio maana unajisifu kuhoji?

Kwa sababu kama unaamini Mungu(mtumwa wa Mungu) na hauamini dini(sio mtumwa wa dini) basi huko kuhoji kwako inatakiwa umuhoji Mungu mwenyewe na sio kuhoji dini halafu unajisifu kuhoji.

Unajitia misifa ambayo mwenyewe unajiona una akili sana upo huru kumbe ni ujinga,huwa unanifurahishaga kweli.

Ushawahi kumhoji Mungu hata jambo moja tu?
 
Kwahiyo umetaja spiderman kwa sababu spiderman ni kitu cha kufikirika ?

Sasa nani alikwambia kuwa Mungu ni kitu cha kufikirika tu kama spiderman? Mfanano hapo ni upi?

Mungu ni hadithi zilizo nje ya uhalisia na ndio maana uwepo wake hauthibitishiki nje ya masimulizi yakufikirika

The same goes with Spiderman

It's Scars
 
Teh...ukishashiba ugali wa matembele lazima uwe na mentality za dizaini hii, kuna magonjwa hatari ya tauni yamewahi kuangamiza mamilioni ya watu huko nyuma achana na hii korona, watu waliomba na Mungu akaingilia kati. Najua kwa akili yako fupi utafikiri yalitokomea tu by chance..
 
Unajuaje kua wanapona na sio kwamba ni script iliyochezwa na padre/sheikh ili kuwateka watu kiakili?

It's Scars
 
Viongozi wengi wa dini wa zama hizi ndo wanaofanya Mungu atukanwe kwa wayatendayo na uongo wao,
Lkn nafsini mwangu iwe iwavyo,corona iwepo isiwepo,dini ziwepo zisiwepo naamini Mungu yupo maana binafsi nilishayaona matendo yake kwenye maisha yangu,
Binafsi huwa natamani Mungu awaumbue viongozi wachumia tumbo wa dini za sasa wanaofanya atukanwe,
Waafrika tujifunze kuomba wenyewe,kumuambia Mungu haja zetu wenyewe,tusitegemee hawa matapeli waliopotoka,
Sent using Jamii Forums mobile app
 
nadhani kwa vizazi viliyopita Mungu/Allah alikuwa anasikiliza maombi ya wanadamu na kuyafanyia kazi haraka.

ila kwa kizazi hiki cha wachungaji wanzinzi(kama gwajima), matepeli(kama wale mashehe wa instagram),Mungu kaamua kula pozi kidogo ili tunyoke.

Mungu kazia hapohapo ili hawa manabii na wachungaji feki wa kizazi hiki wapate kuumbuka.
 
Kwa hiyo hilo gonjwa la town mungu alilileta kisha akasubiri aombwe ndio aliondoe?, usiniambie hakujua lilipotoka hadi likaua watu wakamuomba ndio akaliondoa.

Mungu hawezi kuzuia gonjwa kabla halijaua watu wake ama hua hajui linapotokea anakija kushtuliwa na maombi?😀😀.

Ukimwi, kansa bado maombi hayajamfikia ili ayaondoe kama alivyoondoa town au hajui kama yapo?

Tuendelee kuomba mkuu.
 
Asante mkuu,
Mm kwa uwazi kabisa huwa nasema hawa watu ni chanzo cha uvivu,upofu,ujinga na umaskini wetu,
Wanafanya watu mateka wao,kwa faida za matumbo yao,
Ndugu Mungu ni Baba yetu,kwa nini sasa umtumie jirani yako kukuombea kwa Baba yako,
Mungu hawezi sikia maombi ya hawa maana wamechanganya Maombi na njaa kwa pamoja,
Hapo hakuna cha mtume wala nabii nacho kiona hapo kuna wawekezaji tu walio wekeza kwenye dini

Mitume na manabii haya ni majina ya kijasiliamali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunawaamini wanasayansi,madaktari n.k halafu wewe unasema hizi sio zama za kuamini? Au wewe huamini wanasayansi na madaktari?
Mi sifungamani na imani

Wewe kama unawaamini wanasayansi mimi niko kinyume kwa kuikubali sayansi na wanasayansi kupitia tafiti zake ambazo zinathibitishika

It's Scars
 
Tusipime nguvu ya Mungu kupitia hawa wachumia tumbo wanaojiita mitume na manabii wa sasa,
Nguvu ya Mungu ipo lkn tatizo tunadhani wanachosema hawa wachumia tumbo ndo nguvu ya Mungu,
Mungu hawezi jibu haya maigizo yanayoitwa maombi kwake yanayofanywa na watu ambao azma yao ya kwanza ni umaarufu na pesa,Mungu hashirikishwi na nia ovu za kitapeli za hawa matapeli,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tujifunze kumuomba Mungu straight sisi wenyewe,turekebishe MAHUSIANO BINAFSI SISI NA MUNGU siyo kupitia majizi haya
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imani katika Mungu Mwenyezi haifanyi kazi kama unavyofikiri, wacha Mungu hawana kinga ya kuugua na kufa ila wana kinga ya kufa kifo cha milele. Maana yake wanaweza kufa katika mwili lakini wanaishi milele katika roho. Ila shetani na mawakala zake wanasubiriwa na adhabu ya kifo cha milele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…