Corona imekuja kuumbua uongo wa dini


Ukimwi unamiaka zaidi ya 30 na Umeua watu zaidi ya mamilion ikiwemo mapadre na masheikh

Hapa ndio tunakuja kuelewa kua matatizo ya kihalisia hayatatuliwi kwa solution za kufikirika

It's Scars
 
We dogo unasoma na kuelewa kweli? Mbona unauliza kitu ambacho nishaelezea?

Nimekwambia suala la Mungu linaathiri maisha ya watu na nikaelezea kwa uchache,leo watu wanasaidia wenzao kwa imani ya kwamba Mungu atamlipa zaidi,watu wanafanya mema na kuacha mabaya kwa sababu ya suala la Mungu na mambo mengi tu ambayo yote yameathiriwa na suala la Mungu. Halafu wewe unakuja kufananisha habari za spiderman ambaye anaishia kwenye movie tu.

Habari za spiderman zimebuniwa kwenye movie na kuishia huko huko haina utata,sasa utafananishaje na habari za Mungu? Umelinganisha visivyolingana kabisa.

Wanapinga uwepo wa Mungu kila mtu anaelezea jinsi imani ya Mungu ilivyoanza tofauti na mwenzie.
 
Ooh. Upo sahihi kabisa, hakuna Mungu...

Ma shaa Allah, ushaanza nusu ya shahada ya Kiislam.

Tatizo nini? Malizia tu kabisa.
 
Tujifunze kumuomba Mungu straight sisi wenyewe,turekebishe MAHUSIANO BINAFSI SISI NA MUNGU siyo kupitia majizi haya

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini mungu ahitaji maombi?

Wewe unaomba ili iweje? Na kwanini uombe kama mungu anajua kuisoma akili yako hata kabla hujamuomba?

Mbona yeye anauwezo wa kujua dhambi zako ulizozifanya kwa kufikiri tu kichwani mwako, na akazihesabu kua ni makosa?

Kwanini ashindwe kusoma hitaji lako la moyo wako bila kusubiria maombi yako?

It's Scars
 
Kuna watu wauaji wanaua watu na ndiyo dhambi kubwa kwenye dini ila bado ni muumini wa dini na anaamini Mungu,sasa huyo mtu utasema anaamini dini kwa sababu katishwa atachomwa moto?

Hoja zengine za kuchekesha kweli.
 
Dhihaka katka masuala ya dini no ujuha wa kiwango Cha 5 G.. weendelea tu.
 
Hili swala lingekua linatambulika kweli na ikawa linauhalisia, tusingeona nguvu kubwa ikitumika mekka na vatican kupiga marufuku watu wasiende kwa uoga wa kufa, wakati wakifa watapata maisha maziluri ya milele..

It's Scars
 
Huku mtaani kwenye ibada ya leo unaambiwa ukifika mlangoni unaulizwa mara mbili "ulinawa na sabuni unavyotoka kwako" ukisema ndio wanakupa sabuni unawe ndio uanze misa. Yani imefikia wakati hadi mapasta hawakuamini

Halafu mwisho wa ibada mhasibu wa kanisa alivalia gloves anapoenda kuchukua sadaka ili akazihesabu

It's Scars
 
Kweli kabisa Scars] hajamjua mola kama ana sifa ya ukatili pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafikiri hao waliopitiwa na ebola hawakuomba ili waepushwe nao?

Hiyo ebola ilivyoingia kwenye hiyo nchi uliona mchungaji gani hapa akifunga safari kwenda kuwaombea wagonjwa huko ili kuqapinyesha?

Mwisho wa ebola ulikuaje? Ulimalizwa kwa maombi?

Ukimwi una miaka mingapi duniani?

Kwanini ukimwi umebaki kua tatizo zaidi ya miaka 30 katika ulimwengu ambao una waombaji ambao wakiomba wanatatuliwa matatizo yao?




It's Scars
 
Hapa unamzungumzia Mungu yule yule anaye jinasibu kuwa mkarimu au unazungumzia Mungu yupi huyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujui ukiandikacho we mbwa mwitu. Na
Usipotubu utakufa hakika.
Hata nikitubu kufa nitakufa kwasabu ni nature ya ulimwengu

Wewe ulitishiwa kufa ndio maana ukakubali kuamini mungu yupo?

Usikute aliyekutisha alisha jifia kitambo lakini bado unaendelea kumuamini na kukiogopa kifo

It's Scars
 

Humakiniki na nicho kiandika ndo maana unaoata wenge

Hapo kwenye sheikh au mchungaji unaweza kuweka mtu yeyote yule na bado kauli yangu ikawa imelenga pale pale nilipopakusudia

Kuondoka kwa hilo tatizo hapa ndipo tatizo liliko

Unajuaje kua tatizo hilo limeondolewa kwa dua/maombi na sio kwamba ni drama tu imechezwa ili kukuteka kiakili uamini majini na mapepo ni vitu vya uhalisia?

It's Scars
 
Kuna watu wauaji wanaua watu na ndiyo dhambi kubwa kwenye dini ila bado ni muumini wa dini na anaamini Mungu,sasa huyo mtu utasema anaamini dini kwa sababu katishwa atachomwa moto?

Hoja zengine za kuchekesha kweli.
Swali nikuulize wewe, huyo mungu ambaye waumini wake wanaua watu katoka wapi? Kila kitu mungu mungu hahaha, fkn waste of time
 
Wanasema shetani hufanya yale yaliyo mabaya, lakini kwenye hili janga la corona wamemuacha shetani na kusema kua ni mungu ametupa corona baada ya watu kufanya mahasi

Sasa nafasi ya shetani kufanya ubaya iko wapi kama ubaya huu umefanywa na mungu utamlaumu shetani kwa jambo lipi?

Wengine wamesema huu ni mpango wa shetani, sasa kama mpango wa shetani inamaana huyu shetani anaua hadi watu wa ovu wakati ni watu wake?

Kama shetani anaua watu waovu hiyo si itamaanisha shetani ni mzuri kwasababu kaua watu ambao wanafanya maovu yasiyompendeza mungu?

Na kama shetani kaua watu wabaya, hiyo si inamaanisha Mungu ni mbaya kwasababu ameshindwa kuwalinda watu wake wasiuliwe na shetani?





It's Scars
 
Kwa hiyo pale Vatican wanapopukutika kama nzige hakuna padri au kadinali mwenye imani pale?
Ajabu ni kwamba hiyo maana ya imani aliyoiandika imetafsiriwa na hao hao waliopiga ban safari za kwenda makwao kwa hofu ya corona

It's Scars
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…