Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Kwa hiyo hilo gonjwa la town mungu alilileta kisha akasubiri aombwe ndio aliondoe?, usiniambie hakujua lilipotoka hadi likaua watu wakamuomba ndio akaliondoa.

Mungu hawezi kuzuia gonjwa kabla halijaua watu wake ama hua hajui linapotokea anakija kushtuliwa na maombi?[emoji3][emoji3].

Ukimwi, kansa bado maombi hayajamfikia ili ayaondoe kama alivyoondoa town au hajui kama yapo?

Tuendelee kuomba mkuu.

Ukimwi unamiaka zaidi ya 30 na Umeua watu zaidi ya mamilion ikiwemo mapadre na masheikh

Hapa ndio tunakuja kuelewa kua matatizo ya kihalisia hayatatuliwi kwa solution za kufikirika

It's Scars
 
Popote unaweza kuziongelea

Kumbuka ishu sio kuziongelea, ishu ni uhalisia wa kitu husika.

Kitu chochote cha kufikirika kinaweza kujadiliwa katika mazingira yeyote yale lakini hiyo haimaanishi kitu hicho ni real


Mungu unaweza kumjadili sehemu gani ambayo spiderman au kitu kingine hakiwezi kujadilika katika mazingira hayo?

It's Scars
We dogo unasoma na kuelewa kweli? Mbona unauliza kitu ambacho nishaelezea?

Nimekwambia suala la Mungu linaathiri maisha ya watu na nikaelezea kwa uchache,leo watu wanasaidia wenzao kwa imani ya kwamba Mungu atamlipa zaidi,watu wanafanya mema na kuacha mabaya kwa sababu ya suala la Mungu na mambo mengi tu ambayo yote yameathiriwa na suala la Mungu. Halafu wewe unakuja kufananisha habari za spiderman ambaye anaishia kwenye movie tu.

Habari za spiderman zimebuniwa kwenye movie na kuishia huko huko haina utata,sasa utafananishaje na habari za Mungu? Umelinganisha visivyolingana kabisa.

Wanapinga uwepo wa Mungu kila mtu anaelezea jinsi imani ya Mungu ilivyoanza tofauti na mwenzie.
 
Naweza kujadili chochote kile kwa namna ambavyo kimesimuliwa hadithini bila kujali uhalisia wake.

nikiandika kauli hapa inayozungumzia uwezo wa spiderman kupanda kwenye maghorofa marefu, pamoja na jitihada zake za kuzuia treni kwa nyuzi za buibui, hiyo itamaanisha kwamba spiderman is real and not fictional character?


Unaweza kuthibitisha huyo huyo Mungu mmoja yupo?

It's Scars
Ooh. Upo sahihi kabisa, hakuna Mungu...

Ma shaa Allah, ushaanza nusu ya shahada ya Kiislam.

Tatizo nini? Malizia tu kabisa.
 
Tujifunze kumuomba Mungu straight sisi wenyewe,turekebishe MAHUSIANO BINAFSI SISI NA MUNGU siyo kupitia majizi haya

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini mungu ahitaji maombi?

Wewe unaomba ili iweje? Na kwanini uombe kama mungu anajua kuisoma akili yako hata kabla hujamuomba?

Mbona yeye anauwezo wa kujua dhambi zako ulizozifanya kwa kufikiri tu kichwani mwako, na akazihesabu kua ni makosa?

Kwanini ashindwe kusoma hitaji lako la moyo wako bila kusubiria maombi yako?

It's Scars
 
Pap mwenyewe kapata corona hahaha, nishasema humu mara kibao dini ni upuuzi uliotungwa watu wameshika kwa sababu tu walizaliwa wakatishiwa kuchomwa moto siku ya mwisho.

Biblia ina makosa mengi mno, quran vilevile. Ila wakisoma wanatafuta kila njia kutetea upuuzi hadi watu wenye phd zao hahaha so stupid.Na waache upuuzi wa kwenda kukusanyika makanisani nchi nyingine makanisa ndiyo yamesababisha milipuko hii.
Kuna watu wauaji wanaua watu na ndiyo dhambi kubwa kwenye dini ila bado ni muumini wa dini na anaamini Mungu,sasa huyo mtu utasema anaamini dini kwa sababu katishwa atachomwa moto?

Hoja zengine za kuchekesha kweli.
 
Dhihaka katka masuala ya dini no ujuha wa kiwango Cha 5 G.. weendelea tu.
 
Imani katika Mungu Mwenyezi haifanyi kazi kama unavyofikiri, wacha Mungu hawana kinga ya kuugua na kufa ila wana kinga ya kufa kifo cha milele. Maana yake wanaweza kufa katika mwili lakini wanaishi milele katika roho. Ila shetani na mawakala zake wanasubiriwa na adhabu ya kifo cha milele
Hili swala lingekua linatambulika kweli na ikawa linauhalisia, tusingeona nguvu kubwa ikitumika mekka na vatican kupiga marufuku watu wasiende kwa uoga wa kufa, wakati wakifa watapata maisha maziluri ya milele..

It's Scars
 
Dini ni aina ya siasa lengo lake mama ni kumtawala mtu
Mimi niliacha kuamini dini miaka karibu 7 iliyopita angalia sasa hivi hivi wanavyotapata ombeni mtapewa ombeni basi wagonjwa wa corona wapone wakina gwajima mwamposa wezi wakubwa na kodi inaitwa sadaka
Huku mtaani kwenye ibada ya leo unaambiwa ukifika mlangoni unaulizwa mara mbili "ulinawa na sabuni unavyotoka kwako" ukisema ndio wanakupa sabuni unawe ndio uanze misa. Yani imefikia wakati hadi mapasta hawakuamini

Halafu mwisho wa ibada mhasibu wa kanisa alivalia gloves anapoenda kuchukua sadaka ili akazihesabu

It's Scars
 
Sasa nani amekwambia amewaachia Madaktari,wakati yeye ndio ameruhusu ugonjwa huo uwepo na uwadhuru watu.

Yeye ndio ameuleta na yeye ndio wakuuondoa,hakuna mwanadamu mwenye kuweza kuuondoa ugonjwa wala kuleta ugonjwa.

Maelezo yako yote yanaonyesha ni kwa namna gani humjui Mola muumba wa mbingu na ardhi.
Kweli kabisa Scars] hajamjua mola kama ana sifa ya ukatili pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao Viongozi wa dini pia Usisahau walikemia ebola haikufika nchini sijaona uzi wako ukipongeza dini kufanya maombi kuzuia ebola.

Kama siyo unafiki nini? Watu wanafiki utawajuwa kwa maneno yao.

Dini zimetabili siku za mwisho Kuna majanga yatatoke, janga lazima litoke ili maandiko yatimie. Unaanza kukashifu dini.
Unafikiri hao waliopitiwa na ebola hawakuomba ili waepushwe nao?

Hiyo ebola ilivyoingia kwenye hiyo nchi uliona mchungaji gani hapa akifunga safari kwenda kuwaombea wagonjwa huko ili kuqapinyesha?

Mwisho wa ebola ulikuaje? Ulimalizwa kwa maombi?

Ukimwi una miaka mingapi duniani?

Kwanini ukimwi umebaki kua tatizo zaidi ya miaka 30 katika ulimwengu ambao una waombaji ambao wakiomba wanatatuliwa matatizo yao?




It's Scars
 
Dunia yote imesalander! Hakuna mwenye nguvu, hakuna mwenye utaalamu, hakuna tajiri, hakuna teknolojia, hakuna silaha kali, hakuna usalama wa taifa, hakuna hakuna hakuna chochote. Kila nchi inalilia hali yake. Kila nchi inafunga mipaka yake, haijulikani tena nani anamfungia nani. Hakuna nchi inayohurumia nchi nyengine, kila moja inapambana kivyake... yote yamesababishwa na kidudu kidogo-virus.. wala hakionekani kwa macho!!!! Unahitaji nini kukubali kuwa Mungu yupo? ambaye akitaka lake hakuna nguvu yeyote inayoweza kulizuia?!!
Ameleta corona akitaka ataiondoa hakutaka ataiacha iendelee kutia adabu watu. Hapangiwi ampe nani na nani ni maamuzi yake tu!!! Watu wa dini yeye ndo anawajua zaidi kuliko wewe kama ni wa kweli au waongo! Sisi tunaomuamini uwepo wake na nguvu zake tunamuomba atunusuru na hili lkn hatuna haki ya kumlazimisha. Tunaomba, anaweza akatukubalia au akatukatalia! Hakuna mwenye guarantee ya maamuzi ya Mungu!
Hapa unamzungumzia Mungu yule yule anaye jinasibu kuwa mkarimu au unazungumzia Mungu yupi huyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujui ukiandikacho we mbwa mwitu. Na
Usipotubu utakufa hakika.
Hata nikitubu kufa nitakufa kwasabu ni nature ya ulimwengu

Wewe ulitishiwa kufa ndio maana ukakubali kuamini mungu yupo?

Usikute aliyekutisha alisha jifia kitambo lakini bado unaendelea kumuamini na kukiogopa kifo

It's Scars
 
Kijana naona umekariri ndiyo maana unashindwa kunielewa,narudia tena mie sizungumzii masheikh wala mapadri bali nazungumzia dua na dua hufanywa na muumini yeyote sio suala la masheikh wala mapadri hapa. Na kuhusu kupona kweli ni kuondoka kwa hilo tatizo,maana kama hilo tatizo haliji tena maana yake ugonjwa umepata tiba.

Humakiniki na nicho kiandika ndo maana unaoata wenge

Hapo kwenye sheikh au mchungaji unaweza kuweka mtu yeyote yule na bado kauli yangu ikawa imelenga pale pale nilipopakusudia

Kuondoka kwa hilo tatizo hapa ndipo tatizo liliko

Unajuaje kua tatizo hilo limeondolewa kwa dua/maombi na sio kwamba ni drama tu imechezwa ili kukuteka kiakili uamini majini na mapepo ni vitu vya uhalisia?

It's Scars
 
Kuna watu wauaji wanaua watu na ndiyo dhambi kubwa kwenye dini ila bado ni muumini wa dini na anaamini Mungu,sasa huyo mtu utasema anaamini dini kwa sababu katishwa atachomwa moto?

Hoja zengine za kuchekesha kweli.
Swali nikuulize wewe, huyo mungu ambaye waumini wake wanaua watu katoka wapi? Kila kitu mungu mungu hahaha, fkn waste of time
 
Nilishaandika hivi haya myaonayo sasa ya kuabudu, kuamini kuwa kuna ulimwengu wa kiroho mara Mungu na mpinzani wake shetani,hapo baadae vizazi vijavyo watakuja kusoma hiyo historia huku wakitucheka! Watakuja kufundishwa jinsi tulivyokuwa wapuuzi tukiamini hayo mambo...
Dini ni project zilizoshiba na zinatusua fedha haswa kwa wakuu wanaohodhi hayo mambo,wanaoamini hawawezi kuelewa maana ndio washatekwa akili,wao wanajiona ni watumishi wa Mungu kumbe ni wateja wa watu fulani fulani[emoji23]
Mungu wanavyomfikiria sivyo alivyo!!
Wenyewe waendelee kupiga sala tu but wajue wanafanya kazi ya bure!!
Haya nilioandika wataona nimekufuru ati mimi nimejawa na ushetani na wakati huohuo wanaamini Mungu aliumba kila kitu it means na shetani aliumbwa na Mungu sasa linapokuja swala la tabia mbaya za shetani wanasema muanzilishi ni shetani!! Wakati shetani nae aliyakuta mambo hakuna tabia ambayo shetani kaianzisha bila kuirithi kwamaana Hakuna ambacho hakijatoka kwa baba!![emoji23]
Mungu wamemvesha joho la tabia nzuri tu sasa sijui mbaya zilitoka wapi maana yeye ndo muanzilishi wa kila kitu!!

Hakuna cha Mungu wamaombia atakusaidia sahau maana maisha ni uhalisia na sio maombi.
Wanasema shetani hufanya yale yaliyo mabaya, lakini kwenye hili janga la corona wamemuacha shetani na kusema kua ni mungu ametupa corona baada ya watu kufanya mahasi

Sasa nafasi ya shetani kufanya ubaya iko wapi kama ubaya huu umefanywa na mungu utamlaumu shetani kwa jambo lipi?

Wengine wamesema huu ni mpango wa shetani, sasa kama mpango wa shetani inamaana huyu shetani anaua hadi watu wa ovu wakati ni watu wake?

Kama shetani anaua watu waovu hiyo si itamaanisha shetani ni mzuri kwasababu kaua watu ambao wanafanya maovu yasiyompendeza mungu?

Na kama shetani kaua watu wabaya, hiyo si inamaanisha Mungu ni mbaya kwasababu ameshindwa kuwalinda watu wake wasiuliwe na shetani?





It's Scars
 
Kwa hiyo pale Vatican wanapopukutika kama nzige hakuna padri au kadinali mwenye imani pale?
Ajabu ni kwamba hiyo maana ya imani aliyoiandika imetafsiriwa na hao hao waliopiga ban safari za kwenda makwao kwa hofu ya corona

It's Scars
 
Back
Top Bottom